Pinda awasimamisha katibu mkuu wa wizara ya afya na mganga mkuu

Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.


SIO RAHISI,PiNDA HUYU HUYU ANAELIA LIA BUNGENI,MMMHH

STORI ZA KWENYE KAHAWA HIZI
 
habari hii ni yakweli kabisa, sisi tuko karibu kabisa na hapa inako toka, lakini nawaambieni wana jf , mama nyoni na wizara ya afya hawana kosa lolote kuhusu sakata hili la madakitari, hili ni tatizo la serikali kutothamini madakitari, madai ya madakitari hayajazuiwa na katibu mkuu, yamekwama utumishi na hazina walikataa kwa gigezo kwamba hawana pesa na pm anafahamu hili, sasa nawafukuza km, pesa watatoa wapi za kuwalipa madakitari hii ni daganya toto na distruction ya credibility ya watumishi wa uma. anapaswa yeye kujiuzulu kabla ya walio chini yake kujiuzulu.
 
cjui leo nimeamkaje! Nimeenda mahala asubuhi kufuatilia ela yangu nkapata na ziada,nkafungua tv nkakutana na bunge linakubali marekebisho yaliyowatoa wanacdm na ncrr bungeni,nafungua tbc nkaona pinda kwa niaba ya jk amewatimua dkmkuu na katibu mkuu nyoni ili madaktari wawe na amani ktk magumzo...nadhani leo ni siku njema kwangu...eeh na uyu mdada aliyenikataa hata hapokei cmu ,sasa naona anabip sasa ivi, mh mungu ni mwema leo. Ngoja nikamalizie kazi...leo ni furaha kwangu...jk nisaidie uwatimue na mawazir

huyu dada anayekubeep sio habari njema. Anataka kuchukua hizo hela zako.
 
Makatibu wakuu wasiyo na Uweza wa kutawala watu wako wengi ambao Mhe Rais anatakiwa afanye maamuzi magumu ya kuwasafisha katika Serikali, wamefanya nchi imekuwa maskini kwa utendaji mbovu na hawana mawazo yoyote ya maendeleo zaidi ya kuvuruga mazuri waliyoyakuta na wataalamu waliyo chini yao kama huyo alivyofanya. Hata nia njema za mawaziri wanazivuruga na wanajifanya miungu kutokana na mamlaka makubwa mno waliyonayo katika sheria ya utumishi. Tangu wameteuliwa hadi sasa hakuna jambo moja la maendeleo kwa umma wanaloweza kutaja kuwa wamefanya sanasana wamevuruga mazuri waliyoyakuta na kudhalilisha wataalam ambao ndiyo viini vya maendeleo na idea mpya za maendeleo.
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

Katibu mkuu anachaguliwa na Rais sio waziri mkuu! kimamlaka pinda hana ubavu wa kumsimamisha nyoni. Acha propaganda zako hapa
 
Mganga Mkuu Bw. Deo na KM wizara ya afya wasimamishwa Kazi kufuatia mgomo Wa madaktari! Sosi radio clouds breaking news
 
Inakuwaje Pinda ashindwe kumchukulia hatua Jairo kwa kile alichokisema kuwa hakuwa na mamlaka, haya mamlaka ya kumsimamisha Blandina Nyoni ameyapata wapi?
 
Hbr nilizosikia hivi punde toka kwa reporter wa clouse fm aliyeko eneo la tukio ni kwamba,katibu blandina nyoni na mganga mkuu wa taifa kusimamishwa kazi. SOURCE:Clouse fm
 
Ndo maamuzi magumu na muhimu yanayotakiwa, but why kwenye sakata la Jairo alisema kama angekuwa na mamlaka angemsimamisha DJ, leo kayapata wapi hayo mamlaka
 
Kwanini imechukua muda hivi.. Ila mimi kwa maoni yangu.. Waziri ndio alitakiwa kuwajibika kwanza
 
Mtoto wa mkulima anatuchanganya, siku ile amekaa na akina PS, CMO, na Mawaziri wa Afya, alisema atawafukuza kazi madaktari, leo anawageukia walewale aliokuwa nao akitangaza nia ya kuwatimua madaktari kazi!
 
Dai la kwanza la madaktari nalokumbuka lilikuwa ni kuitaka serikali kuelezea mustakabali wa afya ya Mtanzania, kuwapatia vifaa vya vya matibabu na vitanda kwa wagonjwa sambamba na kuboresha mazingira ya kazi. Sina hakika kama hilo lilishatekelezwa.
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

amewasimamisha,vyipi kuwafukuza?
!
 
hizi tetesi kuwa waziri mkuu amewasimamisha kazi katibu mkuu na mganga mkuu kama ni za kweli basi zinanishangaza sana.

Uwajibikaji unatakiwa uanzie ngazi ya juu na sio ya chini. Tunakumbuka wakati madaktari waliopogoma walimtaka waziri mkuu kuja kuwasikiliza. Lakini waziri mkuu yeye aliamua kwenda kuongelea suala la mgomo sehemu ambayo madaktari hawakuwepo. Waziri mkuu alitoa tamko la ubabe akiwataka madaktari kurudi kazini kwa nguvu na kama wasingefanya hivyo wangekuwa wamejifukuza kazi wenyewe. Hili tamko la waziri mkuu halikukubaliwa na madaktari. Kufuatia hili tamko badala ya madaktari kurudi kazini mgomo ndiyo ulikolea zaidi na mpaka leo imekuwa sio mgomo tena bali criss kwenye sekta ya afya hapa nchini.

Leo hii waziri mkuu anakuja na tamko la kuwafukuza kazi katibu mkuu na mganga mkuu. Hii sio sahihi. Waziri mkuu kama kiongozi wa ngazi ya wa serikali ndiye alishindwa kushughukia mgomo wa madaktari hivyo basi anatakiwa awajibike. Watu wengi wameshakufa katika hospitali mbalimbali hapa nchini kutokana na kushindwa kwa waziri mkuu kutumia busara tangu mwanzo wakati alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Badala yake yeye alitumia ubabe na kutoa majibu mepesi kwenye masuala magumu yanayohusu kufa ua kupona kwa wananchi.

Kimsingi hili sakata limeshinda. Ameshindwa kuwahudumia wananchi. Hivyo anatakiwa kuwajibika. Hasiwatuwe wenzake kafara. Kama alikuwa makini basi siku ilipotoa tamko la kibabe ndiyo siku angewasimamisha kazi badala ya kutoa lile tamko. Tamko lake limechochea mgomo na maafa yametokea. Sasa basi arudi kwenye tamko lake la kibabe na kupima kama kweli alitumia busara.
 
Back
Top Bottom