Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,648
.......hapo penye red, maneno yale yanawafaa wabunge maana ndiko watu wanachukulia reference/s!!!!!
Kwani wabunge wana ubinadamu gani?
.......hapo penye red, maneno yale yanawafaa wabunge maana ndiko watu wanachukulia reference/s!!!!!
Unaongea kama baba yako na mama yako kijijini wanaishi nyumba ya ghorofa na wakiumwa ambulance inawafata kuwawaisha airport kuelekea Apollo India.
Kila siku nasema nchi hii imejaa Ubinafsi na Uoga. Hii ndiyo ilikuwa nafasi kwa wananchi, wafanyakazi wote kugoma na kuandamana mpaka mabadiliko yatokee
kweli kabisa kwasasa ilikuwa kwa kila mtanzania kujitokeza na kuwaunga madaktari bila kujali itikadi za chama kwasababu tunaotibiwa ni wananchi na tunatibiwa bila kujali itikadi zetu. Hivyo tungewaunga mkono, kwani wanatutetea ili huduma ziwe bora pamoja na kuwa wanataka posho, mishahara yao iongezwe lakini hapohapo wanataka hospitali ziwe na huduma nzuri madawa yawepo, vitanda vya kutosha. Na wanaostahili kupewa huduma bure wapate bila kuambiwa labda dawa hakuna kanunue mwenyewe. Madaktari wanatutetea sisi wananchi lakini umbumbu wetu na bila kujali tunawaona hawafai. Hao viongozi wanaonekana wanafaa wao wanatibiwa nje. Tungeamua kuandamana nchi nzima japo kwa siku moja kuwaunga madaktari wetu. Pinda hana lolote ukifuatilia historia yake tangu apate uwaziri mkuu ameongea mengi ya uongo na anaposhindwa uanza kulia ili aonewe huruma ooh nilikuwa na uchungu sana(kumbuka kuhusu albino) kama alikuwa nauchungu sana na albino na kutoa amri kuwa atakayepatikana na kosa la kuua albino auwawe, iweje leo anashindwa kutekeleza madai ya madaktari. Ili raia zaidi ya 10-20 wasife kila siku. Ina maana alikuwa na uchungu sana na albino wawili kuliko raia 10?
Huko jeshini wataenda kuimport madaktari wengine tokea China...labda wanathani itakuwa cheap labour kama walivyozoea.
katika kuthibitisha ukosefu wa umakini ndani ya serikali, mchana huu mwandishi wa Clouds Redio ameripoti kuwa wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili hawakupata huduma yeyote ikiwemo kushuhudia zaidi ya ambulance 7 zikileta wagonjwa toka hospitali mbali mbali na kulazimika kuondoka na wagonjwa wao kutokana na kukosekana kwa huduma katika hospitali hiyo. Hii inashiria kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshinde kutekeleza ahadi yake kupelekea madajatari toka JWTZ na JKt akama alivyoahidi jana wakati akitoa kauli za dharau dhidi ya madakatari wanaogoma.
My take: Tukumbuke kiini cha mgogoro huu ni madakatari walioko mafunzoni yaani interns katika hospitali ya Muhimbili kunyanyaswa na uongozi wa Wizara ya Afya hivyo kutakiwa Waziri Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa kuondolewa mara moja kwa kuishawishi serikalim kuchukua hatua za kionevu dhidi ya madakatari hao waliokuw akatika mafunzo. Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe katika kuwalinda wazembe watatu?
Ni imani yangu watatu hao wakiondolea hata leo madakatari walioko katika mgomo watakuwa tayari kuzungumza na serikali kuhusu madaia yao.
wewe ni mgonjwa au la wewe ni Gamba,unasemaje?hiyo mizigo iliyoko huko wizara ya afya huioni?na kinachofanya Nyoni aonekane kama ndio mmiliki wa wizara ya afya ni nini?na hao mawaziri wanafanya nini hapo,huyo mganga mkuu juzi tu katoka kufanya madudu ya Reagents za HIV bado havijapoa kalizua jingine na bado mnakinga kifua,kwanini huangalii chanzo cha tatizo?Nani anakubali watanzania wafe? Kama ni hukumu, basi huwa kuna hukumu 1st hand murder & 2nd hand murder. Hapa nadhani 1st-hand murders ni nyinyi madaktari msiowahudumia hao wagonjwa na 2nd-hand murders ni hao wengine. Wekeni ubinadamu mbele ..
Kazi kwelilkweli embu tuambiane ukichukua madaktari kutoka China ambao hawajui Kingereza wala kiswahili si ndio tutaongeza tatizo.
Hakuna suala la udogo au ukubwa hapa mtu ukiwa kiazi ni kiazi tu kwa mfano hapa PM ni kiazi wa hakuna kuogopa PM ni Kiazi
Haaa..!!!! Kumbe hawakutii AGIZO la kuwataka kurejea KAZINI? Aliyetoa hilo agizo anasemaje?