Pinda ashindwa kupelekea madaktari wanajeshi ktk hospitali za DSM

Najiuliza hao madaktari kutoka jeshini huwa wapo tu hawana kazi?what i know wanatumika ktk hospitali za huko/jeshini. Sasa ukiwaondoa what next?na ni wengi kiasi hiko? kauli nadhani ilitoka kwa jazba

Shida ni hivi kaka, viongozi wetu wanadhania madaktari wanapatikana kwa kura baada ya kampeni ndio maana hakuna anayefikiri umuhimu wao. Wanadhania wapo kama wao ambapo unaweza kumfanya Said Meck Sadiq kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi na hapo hapo akakaimu ukuu wa mkoa wa Dar. Kwa hiyo alifikiri madaktari wa lugalo nao watakaimu muhimbili huku wanaendelea kuhudumia lugalo.
 
mkuu bora umeturudisha kwenye hoja ya msingi, maana PM yeye anaongea tu kuwa anaweza kureplace doctors wote wakati serikari hiyo hiyo imeshindwa kupeleka hata madawa kutoka MSD lakini haisiti kuja na ahadi kubwa within 24hrs!!!

Kama kuna mtu anayeweza kutathmini hasara iliyosababishwa na mgomo mpaka sasa ndio atajua kuwa kuondoka kwa Mh. Mponda, Nyoni, Mtasiwa nk ilikuwa ni nafuu sana kwa taifa.

Namshauri PM (japo mimi ni mtu mdogo sana na siwezi hata kumkaribia) aache porojo na ku-victimize viongozi wa mgomo badala yake ashughulikie madai kama ni ya kweli na kama sio ya kweli basi atwambie maana yeye ni juzi tu wakati wenzie wanaenda Apollo India yeye alienda London kucheck afya yake!

Hawa wakubwa wana lugha za kilaghai na maneno ya kijanja tena wanafiki kabisa, mtu anazungumza utafikiri jambo analozungumza ni rahisi tuu!!! Mipango yao mingi ni ndoto za Alinacha, kujenga hekalu mwezini. Sasa nimeamini Tanzania hakuna mzima tuna viongozi wasanii kwelikweli, tunamuomba mheshimiwa PM Pinda akae chini apange mipango mizuri ya kutatua madai ya Madaktari. Yeye ni mtu mkuu tunamuheshimu aache porojo!!!! Kama hajui kuna kipindi nchini USA walitoa tangazo kuwa wanahitaji madaktari 400 toka hasa TANZANIA!!!!!!!!!!

 
This is getting out of hand! huwa nina heshima za dhati kwa Pinda maana namuona kama mwenzetu,hana makuu, ila kwa jinsi alivyohandle ishu hii ya madaktari..inaonekana kabadilika sana!

1. Madaktari walianzisha mazungumzo na wizara mapema..ikakataa kuwaskiliza.

2. Wamefanya vikao mara kadhaa kuomba kuonana na Dr. Haji, ila mara zote anawatreat kwa dharau

3. Baada ya kuona dharau zake, wakakosa imani nae. Wakaomba kuonana na Pinda, yeye akakataa kuonana nao kidharau kwa hoja kwamba madai yao yako ndani ya wizara!

4. Wakarudi wizarani na kumwita waziri, yeye akawasakizia Naibu waziri. Wakamwambia wanakutana Don Bosco, yeye akawajibu kwa kejeli hawezi kukutana nao vichochoroni..waje kwenye ukumbi wa serikali..Arnatoglue!

5. Wakamjibu Anatoglue ukumbi mdogo, aje Don Bosco, yeye anaenda na kuita vyombo vya habari Ilala ili viripoti kwamba madaktari wamekataa kuja kuonana nae.

6. Baada ya kuona serikali haina nia ya kuwasikiliza, wakatangaza mgomo rasmi. Wizara ikawa inapinga kwamba hakuna mgomo uliotangazwa na yenyewe "haina taarifa"

7. Siku ya pili mgomo umeshika kasi, wizara bado inacheza na propaganda za magazeni na TV, kuonesha wodi chache na kusema hakuna mgomo!!

8. Baada ya kuona inakua ishu, ndo Pinda akasema atakutana nao! huyu huyu ambaye walimkimbilia mwanzoni akakataa kuonana nao!

9. Wao toka ijumaa wamemwambia jumapili ni siku ya kupumzika kama kuonana nao aje jumamosi au jumatatu. Badala yake, yeye jumamosi katuma ujumbe, na jumapili kaenda ukumbini ilhali akijua kwamba hatakuta mtu!

10. Sasa anasema JKT ihakikishe hakuna sehem yoyote ambayo madaktari wanakutana. Anasahu kwamba revolution za Misri na Tunisia hazikuhitaji mkutane face to face kupanga maandamano au migomo. Age hii Social Networks ni kumbi tosha za watu kukutana! au ndo kupitwa kwa kasi ya maendeleo ya dunia kwa viongozi wetu?

Nabaki najiuliza cheo kimempanda kichwani!
 
Nani anakubali watanzania wafe? Kama ni hukumu, basi huwa kuna hukumu 1st hand murder & 2nd hand murder. Hapa nadhani 1st-hand murders ni nyinyi madaktari msiowahudumia hao wagonjwa na 2nd-hand murders ni hao wengine. Wekeni ubinadamu mbele ..

Unaongea kama baba yako na mama yako kijijini wanaishi nyumba ya ghorofa na wakiumwa ambulance inawafata kuwawaisha airport kuelekea Apollo India.
 
Nianze kwa kusema: Ninaogopa sana kama kweli madactari watarudi kazini kwa vitisho kwa necha ya taaluma yao na kazi wanayoifanya kwa sababu moja tu ya “hofu ya kupoteza kazi” Hili likitokea Madactari hawa watakuwepo kazini lakini morali yao ya kufanya kazi itakuwa imepotea kabisa na hili linaweza kupelekea “Mgomo baridi” ambao kwangu nauona ni hatari zaidi kuliko mgomo unaoendelea sasa.
Athali za matumizi ya ubabe katika mambo ya msingi

Tumeona mfano mara baada ya kuzuwia kwa vitisho kwa mgomo wa waalimu hapa nchini, matokeo yake ni kwamba walimu wanakwenda shuleni kama wajibu lakini hawatekelezi kazi ipasavyo na kimsingi huu ni mgomo baridi ambao bado unaendelea matokeo yake wanafunzi wanamaliza elimu ya msingi lakini hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu. Wapo wanafunzi wa darasa la tano lakini hawawezi kujibu mtihani wa darasa la pili. View Uwezo Study Report at Uwezo.net

Serikali imechukua hatua gani juu ya tatizo la kufeli kwa wanafunzi?

Naamini wote hapa ni wafuatiliaji wazuri wa habari, zifuatazo ni baadhi ya hatua ambazo serikali imezichukua ambazo si kati ya kelo zinazolalamikiwa na walimu: 1. 1.Matumizi ya simu za mkononi yamepigwa marufuku
2. 2. Waziri wa elimu anasema wanafunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza watapimwa tena kabla hawajaanza sekondari na atakayefeli mkuu wake wa shule atawajibishwa ilhali anafahamu wasahishaji ni baraza na si mwalimu mkuu
3. 3. Mtihani wa kidato cha pili umerejeshwa
4. 4. Michango ya masomo ya ziada imepigwa marufuku

NOTE:

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 kati ya wanafunzi 353840 waliofanya mtihani huo ni wanafunzi 40,388 tu ndio waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu.
Kwa upande wa Madactari

Sasa tujiulize, kama madactari nao watarudi kazini na kuendesha mgomo baridi watanzania tutakuwa kwenye wakati gani? Ni bora ya sasa kila mtu anajua wamegoma hivyo anakwenda kwenye hospitali binafsi lakini katika mgomo baridi hatutajua madactari wanaweza wakawepo na wakatupa matibabu tofauti yatakayopelekea athari mbaya kwa wananchi. Lakini pia Tanzania haina madactari mbadala wa kujaza nafasi za madactari hawa ikiwa wataondolewa kazini kama inavyosemwa. Siamini kama matumizi ya mabavu yatalete suluhu katika jambo hili na mwisho wa siku wanaokuja kuumia ni masikini waliopewa jina “WATANZANIA WA KAWAIDA”

Nini maoni yako?
 
Hili mtoto wa mkulima halijui kuwa waweza kumpleka mbuzi mtoni ila huwezi kumlazimisha kunywa maji
 
Kwani serikali ingeamua kuwasimamisha kazi hao wakina Blandina pending uchunguzi kuwa wao ni chanzo cha Tatizo lililo sababisha huo mgomo na vifo vya wagonjwa na madaktari hao wakarudi kazini nchi ingeathirika wapi kwa wao kusimamishwa? Tatizo pekee ni kulindana tuu na kushindwa kutoa maamuzi magumu.
 
Ingekuwa sekta nyingine serikali ingeweza kukaa kimya hoping kwamba wagomaji wakiwa nje ya ajira kwa muda mrefu na wakishaanza kukosa mshahara basi pengine watarudi kazini. Lakini kwenye afya madaktari wakiendelea na mgomo maana yake idadi ya vifo nayo inaongezeka. Serikali, next time pick your battle more wisely!
 
Mambo magumu kote kote Serikali haitaki kugeuka jiwe na madaktari wakitunisha misuri ,wakupoteza zaidi ni serikali wananchi watakosa imani na serikali.Yaonekana madaktari wamejipanga vizuri kuliko serikali.Serikali kuwa makini kwa hilo.
 
Pinda vitisho anavyompaga mkewe wake anadhani na madaktari wako hivyo? Mimi naona hali ikiendelea kuwa mbaya raia na sisi tukusanyike tuishinikize serikali yote kujiuzuru
 
Unajua mgomo huu umekuja kwa sababu madaktari (hata na wananchi wa kawaida) wanaona pesa zote za nchi hii zinakwenda wapi!!! ingekuwa tofauti, yaani maisha yetusisi watumishi wote hayatofautiani sana nina uhakika mgomo huu usingekuwepo. Sasa basi kwa serikali kutumia ubabe, serikali yenyewe inajua matokeo ya ubabe huo, lakini kwa sababu wao wakuu wenyewe na familia zao hawatibiwi kwenye hospitali zetu hawawezi kujali, lolote litakalotokea halitawaathiri. Ila ipo siku mungu atasikia kilio chetu.
 
Rais akitoka ADIS ABABA nadhani kesho kwani hali ilivyo Hawezi kwenda nchi nyingine ATAANZA NA PINDA WAKE KWANI HANA USHAWISHI MKULIMA HUYU then atamalizia na wakina BLANDINA.....TATIZO LA PINDA ANATUMIA HISIA KWENYE MAAMUZI BAADA YA KUTUMIA AKILI NEXT TIME ATATUMIA SABULI LAKE LA UKULIMA
 
Canada na Australia wanahitaji madokta kutoka Tanzania.

Wakiwafukiza tu basi - wananchi tunaingia barabarani
 
hivi tuna waziri mkuu nilimshangaa alivyosema ataki uraisi hivi anaona watanzania
hawana akili mpaka wakampe uraisi uwaziri mkuu awezi au wenzake awamwambii
ukweli
 
Serikali ya kijambazi ya CCM ni dhaifu na legelege na ndiyo mana huwa wanamawazo legelege na dhaifu!
 
Back
Top Bottom