ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 610
- 1,540
Julai 11, 2023, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa ziarani mkoani Simiyu, alitoa ruhusa rasmi kwa madaktari nchini walioajiriwa na Serikali kufanya kazi binafsi kwanye hospitali za umma baada ya muda wao wa kazi kwisha. Waziri Ummy alitoa maelekezo hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu. ACT-Wazalendo kupitia Ofisi ya Wasemaji wa Kisekta tumefanyia tafakuri ya kina maamuzi haya na athari zake kwa lengo la upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote.
Ufinyu wa mishahara na maslahi kwenye sekta ya afya hasa kwenye vituo vya afya vya Umma husababisha wafanyakazi wachache wa sekta hiyo kulazimika kufanya kazi za ziada kwenye vituo vya afya vya binafsi ili kuweza kujiongezea kipato. Hali hii inaongeza upungufu wa wafanyakazi wa afya kwenye vituo vya afya vya umma, anayeumia ni mwananchi mwenye kipato kidogo.
Muda wa kazi kwa wafanyakazi wa afya hususani madaktari na manesi ni kwa mfumo wa zamu za kazi. Wafanyakazi hawa wanapomaliza zamu zao wanapaswa kupumzika kusubiri zamu nyingine badala ya kuhangaika kujipatia kipato. Uchovu wa wafanyakazi wa afya ni kigezo kikubwa kwenye utoaji wa huduma bila ufanisi na kwa ubaguzi, wenye nacho wakipewa kipaumbele zaidi ya wasionacho; hali inayoongeza matabaka katika upatikanaji wa huduma za Afya.
Baada ya saa za kawaida za kazi kuna wagonjwa wanaoenda kutafuta huduma kwenye vituo vya afya vya umma, kugeuza vituo hivyo kama sehemu ya binafsi ni kumnyima huduma mwananchi asie na fedha za kulipia huduma binafsi. Hii si haki kwani mwananchi analipia huduma hizo kupitia kodi mbalimbali.
Kiini cha huduma mbaya za afya nchini ni mfumo usiofaa uliopo wa kugharamia huduma za afya; mfumo unalaozimisha wananchi walipie huduma kutoka mifukoni mwao. Huu ni mzigo kwa mwananchi hasa aliye kwenye kundi kubwa la wenye kipato kidogo waliojiari katika sekta isiyo rasmi. Aidha, mfumo huu unaikosesha Serikali mapato ya kutosha kuendeleza huduma za afya. Serikali imeacha mzigo wa gharama za huduma ya Afya kwa mwananchi.
Agizo la Waziri wa Afya litakwenda kuharibu kabisa mfumo wa utoaji huduma za Afya kwa Umma. Mfumo mzima wa utoaji wa huduma za afya umegubikwa na changamoto za upungufu wa wataalamu, mazingira duni ya kufanyia kazi, upungufu wa miundombinu na uhaba wa dawa na vifaa tiba. Changamoto hizi zitaweza kutatuliwa kwa urahisi zaidi pindi tukiwa na mfumo bora wa kugharamia huduma za afya na usimamizi wa fedha.
Mapendekezo ya ACT Wazalendo.
Serikali isitishe maramoja utaratibu huu mpya wa wafanyakazi walioajiriwa na Serikali kutoa huduma za afya binafsi kwenye vituo vya afya vya Serikali. Badala yake ije na mbinu za kuboresha huduma za afya na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa sekta ya afya kwa Umma.
ACT Wazalendo tumependekeza mfumo wa kufungamanisha bima ya afya na mfuko wa hifadhi ya jamii, ambapo kila mwanachama atapata Fao la bima ya Afya. huu ni mfumo wa kugharamia huduma za afya kwa kujiwekea akiba, tofauti na mfumo uliopo wa matumizi pekee. Mfumo tunaoupendekeza unakidhi vigezo vya mfumo unaopendekezwa kimataifa wa kuwezesha kuboresha afya ya jamii sambamba na kupunguza umaskini, kuongeza ajira na kukuza uchumi ili kufikia lengo la Afya kwa wote.
Mfumo wa Kufungamanisha Bima ya Afya na Hifadhi ya jamii utaondoa matabaka katika upatikanaji wa huduma za Afya kwa makundi yote; kundi la wenye Ajira Rasmi, kundi la wasio na ajira Rasmi kama vile wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na kundi la wasio na uwezo kabisa kama wazee na wenye ulemavu Makundi yote yatachangia kwenye Skimu ya hifadhi ya jamii kulingana na uwezo wao na watapata huduma kulingana na mahitaji yao bila ubaguzi wala matabaka.
Hitimisho
ACT Wazalendo inaamini katika kuzingatia haki na usawa kwa wote katika kupata huduma za Afya ili kufikia lengo la Afya kwa Wote na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi wa afya kufanya kazi katika mazingira wezeshi, kupata mshahara wa kutosha, na mapumziko ya kutosha kabla ya kubadilisha zamu za kazi, ili kuwewawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi. Haya yatafanikiwa kwa kuwepo na mfumo bora wa kugharamia huduma za afya.
Mfumo tunaoupendekeza ACT Wazalendo ni wa kuunganisha Hifadhi ya Jamii na Bima ya Afya. Mfumo huu utamwezesha kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya itakayompa uhakika wa matibabu, afya bora na kumuinua kiuchumi. Halikadhalika mfumo huu utawezesha kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa afya.
Imetolewa na;
Dr Elizabeth Sanga
Twitter: @DrBSanga
Waziri Kivuli wa Afya - ACT Wazalendo.
Julai 15, 2023