Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Mayor Quimby

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
2,754
5,838
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”

Pia soma:
 
Back
Top Bottom