Pinda ashindwa kupelekea madaktari wanajeshi ktk hospitali za DSM

Kusema tunamadaktari wa kutosha Jeshini ni sawa na kusema Jeshi letu lina ndege kibao za kivita zinazoweza kuruka wakati wowote.

Hii inaitwa Wishful Thinking.

Tatizo la watu kaa Pinda ni kutumiwa kama ya Ndani jeshini kuna MA na RMA kibao ambao wenyewe wanawaita Madaktari.
Jamaa kaletewa idadi kwa ununda wake wa kushindwa kudadisi hoja kadhanimadkari jeshini ni kibao huyo kaenda kuropoka kwenye vyombo ya habari.

Hivi hao madaktari wa jeshi wakitolewa huko jeshini na kuletwa Muhimbili ni nani atahudumia katika hospitali za jeshi walizoziacha bila madakitari??

Ni siasa zinazo mtuma kuropoka au ni ubabe wa kijima?
Na hilo jeshi likiwa na madaktari wengi kiasi hicho basi jeshi zima ni madaktari. Kweli kiazi hakiwezi kuwa nazi kitaendelea kuwa kiazi tu.
 
Bila shaka Pinda aliamua kutumia approach ya JK kwa WALIMU "eti asiyeripoti kazini kazi hana". Aliamini hiyo ndo suluhu ya mgomo huu. Hakujua kuna utofauti mkubwa sana wa ki-msimamo kati ya walimu (waoga) na madaktari.
 
Ifike mahli Serikali itambue umuhimu wa afya za watanzania!

1. Hivi ni Watanzania wangapi wamefariki tangu kuanza kwa Mgomo huu?
2. Kwa vifo hivyo hasara ni kwa nani? Wananchi au Serikali, nini maana ya Serikali?
3. Hivi watanzania tunafahamu kuwa Serkali inafanya mzaha huu kwa vile tu inafikiri hakuna mtanzania atakaye ikemea?
4. Kwa vifo hivi vya raia wasio kuwa na Hatia, serkali inawajibu gani?
5. Dhana ya kulindana Serkalini itaisha lini?
6. Nani awajibike kwa vifo vya watanzania na hasara nyinginezomfano kuuguza, kusafirisha/kuhamisha wagonjwa??

IFIKE MAHALI WATANZANIA TUTAMBUE HAKI NA WAJIBU WETU KWA KUSIMAIA SERKALI!!!!! MAANDAMANO KILA KONA YA NCHI SERKALI IACHE KUCHEZEA ROHO ZETU KWA KUENDELEZA NYIMBO ZILE ZILE ZA KULINDANA[/COLOR]
KAMA SERKALI HAITARUDISHA MADAKITARI WETU TENA TULIOWAPATA KWA KUWASOMESHA KWA KODI ZETU ZA KUBAHATISHA, WATANZANIA WOTE TUANDAMANE KULAANI KITENDO HICHO. SERIKALI ITATUE MGOGORO HUU MARA MOJA NDANI YA SIKU 2 MWISHO JUMATANO.

TAHADHARI: WABUNGE MUISHINIKIZE SERKALI VIONGOZI WA WIZARA WALIOPELEKEA HALI HII KUFIKIA ILIVYO SASA WAWAJIBIKE IKIWA NI PAMOJA NA KUFUKUZWA KAZI X 1. TUACHE KUCHEZEA ROHO ZA WATANZANIA. SERIKALI ISIPOWASIKILIZA IFANYENI KAMA MLIVYO UNGANA KUWATIMUA KIRAZA NA MSHIRIKA WAKE WIZARA YA MADINI..Alaah!!

POSHO ZA VIGOGO ZIONGEZEKE X DUFU NA WALA HILO HALINA MJADALA LAKINI KWA WATU WENGINE NONGWA? KWA NINI? KODI WALIPE WENGINE TENA KWA LAZIMA WAO HAPANA KWA NINI? MBONA VIONGOZI WANAJENGA MAZINGIRA NA KUFANYA MAAMUZI YA KUJILINDA WAO NA SI YA KULETA TIJA KWA WATANZANIA?

HIVI SERKALI INAFIKIRI WATU HAWAFANYI TATHMINI YA JINSI INAVYO ENDESHA MAMBO NCHI HII???
 
chonde chonde busara itumike katika kutatua mgogoro huu vinginevyo raia wa kawaida wataumia sana. Kumbuka uhai wa mtu ukitoweka hakuna wa kuurudisha. tafadhalini sana mliopewa dhamana ya uongozi angalieni sana msije mkaulizwa mbele ya muumba kwamba hamkucheza karata zenu vizuri
 
wanajeshi wenyewe wemelemewa na vitambi kwa kuwa hawakuzoea kuhudumia watu 90 kwa siku na zaidi, acha waje muhimbili kama nao hawatagoma baada ya nusu siku.
 
Dr ...Kwanini msiwaulize wale wengine wa mikoa 17 iliyobaki wanafanya nini na kwa niaba ya nani? Hivi kama leo Serekali ikawatimua ninyi mliionyesha njia ya kutafuta haki na kwasababu yenu wale wanafiki wa kule mikoani maisha yao yakaboreshwa ...kwaajili yenu ....mimi sipati picha ..lakini tokea mwanzo wa tetesi za mgomo huu mimi niliuliza Dr are you serious? why some of your members still they are attending to office? ......wapi umoja hapa....ni kweli mmejitahidi kuonyesha njia lakini kwa nnchi hii safari ya kutafuta haki bado ni ndefu sanaaa....I doubt ....cjui Watz wamerogwa? Kazi kwelikweli
 
Serikali inasema haina pesa za kuweza kutimiza madai ya madaktari [SAWA]
Serikali inasema inashughulikia madai mengine [SAWA]
Serikali inasema madai mengine hayawezekaniki [SAWA]

Je; Mh. Nyoni, Mponda, Nkya nk haiwezekani wakaondoka??? ....maana hili sidhani kama linahitaji fedha za kigeni kutekelezeka.

Na ikumbukwe kuondoka kwao haina maana kwamba hawawezi lolote bali inamaanisha kuwa hawajawatendea haki Watanzania kwa kushindwa kutatua mzozo wa madaktari mapema mpaka hali imekuwa mbaya hivi!
chonde chonde busara itumike katika kutatua mgogoro huu vinginevyo raia wa kawaida wataumia sana. Kumbuka uhai wa mtu ukitoweka hakuna wa kuurudisha. tafadhalini sana mliopewa dhamana ya uongozi angalieni sana msije mkaulizwa mbele ya muumba kwamba hamkucheza karata zenu vizuri
 
tuko kwenye wakati mchungu ambao unafichua ubwege wa kundi letu zima la kuiweka madarakani serikali isiyosikiliza na isiyo na dira madarakani!watanzania wenzangu tunaotibiwa muhimbili kurudi chini tujiandae kwa kifo na kama unaamini dini ufanye toba maana mauti ni juu kwa juu siyo ya kubahatisha.Ania ya PINDA sitaki kuiongelea maana ni kuchefuchefu hata kumsikiliza,maana utaona hata machoni haamini anachokitetea,maskini mtoto wa mkulima aliyepata kheri uzeeni,ya kumfupishia uhai na kumuumbua
 
Shida ni hivi kaka, viongozi wetu wanadhania madaktari wanapatikana kwa kura baada ya kampeni ndio maana hakuna anayefikiri umuhimu wao. Wanadhania wapo kama wao ambapo unaweza kumfanya Said Meck Sadiq kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi na hapo hapo akakaimu ukuu wa mkoa wa Dar. Kwa hiyo alifikiri madaktari wa lugalo nao watakaimu muhimbili huku wanaendelea kuhudumia lugalo.

Hahahahahaaaa...nimeipenda hiyo
 
katika mazungumzo kati ya waziri mkuu na balozi wa sudan hapa tanzania mnamo juzi, balozi wa sudan alikubali kuwa nchi yake iko tayari kuleta madaktari mabingwa kuja kuwafundisha madaktari wetu.....

Wasudan wanasubiri list ya waliogoma ili walete madaktari wao...

Nani atawalipa? Kwa wao kuwa na ujuzi wakuweza kuwafundisha madaktari wetu inaonyesha their more qualified. Sasa fungu lakuwalipa hao walio qualified litatoka wapi?
 
Tunasubiri labda wapo wa kichina si wao wameona ni mzaha sasa tutakapo choka na khari hii kuna namna ambavo tutawauliza hao tuliowakabidhi madaraka!
 
Pinda aende sasa muhimbili akasaidiane na mapolisi wake kuwatibu wagonjwa...godamn it......na bado...manesi nao wanaanza mgomo....shitless government....
 
Unamaanisha sababu ya msingi ya mgomo wenu "interns" ni uongozi wa Wizara ya Afya (Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa)!! Mbona Mh. Waziri Mkuu aliposoma na kuyatolea maelezo madai ya hao interns inaonesha msingi mkuu wa mgomo ni madai ya mshahara mnono na posho nono kama za wabunge wa bunge la Tanzania!
 
Mimi siamini kuondoka kwa hao jamaa mambo yatabadilika hapo wizarani. Kama mnauhakika wanatenda isivyo haki na chini ya kiwango na bado wapo jua kuwa tatizo ni mfumo wala sio wao. madaktari wafikiri mara mbili , suala si kuwaondoa hao bali ni kubadili mfumo mzima.
 
Madakatari hawapatikani kama walimu walimu wa " vodafasta" na ninafikiri ni hatari kuwalazimisha madaktari kurejea kazini kwa ubabe bila kutatua matatizo yao. Wanaenda kushughulikia uhai na maisha ya watu wala sio vyuma.
 
katika kuthibitisha ukosefu wa umakini ndani ya serikali, mchana huu mwandishi wa Clouds Redio ameripoti kuwa wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili hawakupata huduma yeyote ikiwemo kushuhudia zaidi ya ambulance 7 zikileta wagonjwa toka hospitali mbali mbali na kulazimika kuondoka na wagonjwa wao kutokana na kukosekana kwa huduma katika hospitali hiyo. Hii inashiria kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameshinde kutekeleza ahadi yake kupelekea madajatari toka JWTZ na JKt akama alivyoahidi jana wakati akitoa kauli za dharau dhidi ya madakatari wanaogoma.

My take: Tukumbuke kiini cha mgogoro huu ni madakatari walioko mafunzoni yaani interns katika hospitali ya Muhimbili kunyanyaswa na uongozi wa Wizara ya Afya hivyo kutakiwa Waziri Dr Haji Mponda, Katibu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Ngd Deo Mtasiwa kuondolewa mara moja kwa kuishawishi serikalim kuchukua hatua za kionevu dhidi ya madakatari hao waliokuw akatika mafunzo. Ni kwanini Serikali inakubali watanzania wafe katika kuwalinda wazembe watatu?

Ni imani yangu watatu hao wakiondolea hata leo madakatari walioko katika mgomo watakuwa tayari kuzungumza na serikali kuhusu madaia yao.

Tatizo nikulindana mkuu.hakuna mwanagamba aliyemwema so lazima walindane
 
Acheni kushabikia ubumbavu.tunatakiwa kuwa wazalendo kwa suala nyeti kama hili tuwasii madaktari kurudi kazini ili kuokoa maisha ya ndugu zeti.tuache ushabiki wa kisiasa unaliangamiza Taifa.
 
Mi nilivyosikia wanajeshi watahudumia ilinibidi niende kwa baba yangu mkubwa ambaye anafanya kazi ya jeshi pale Lugalo nikaanza kumuuliza maswali ya kizushi, swali la kwanza kumuuliza lilikuwa, wanajeshi mmejipangaje kutuhudumia pale mhimbili na ocean road maana nimesikia MP anaongea na media kuwa madaktari hawamsumbui na dawa yao ni kupeleka madaktari wanajeshi hospitali zote za dar, jibu lake lilikuwa ni fupi "Hizo ni hisia zake tu" nikahoji tena unamaanisha nini unaposema ni hisia zake kusema vile, akasema "MP anakumbukumbu vizuri sana tu kuhusu hospitali za jeshi kuwa zenyewe tu zina madaktari pungufu, sasa hao madaktari wanajeshi watatoka jeshi lipi au kuna jeshi lingine la madaktari limeundwa ambalo yeye halijui?"
 
KUNA VIONGOZI WANATUMIA JESHI VIBAYA,JAMANI UDAKTARI SI KAZI YA NGUVU(HAIHITAJI NGUVU).
INGEKUWA NI UJENZI WA DARAJA,KUBEBA TOFALI,KUCHIMBA NA KUOPOA WATU WALIFUNIKWA NA VIFUSI HAPO NINGEAMINI JESHI WANGEWEZA,
ILA HILI LA udaktari,LINAHITAJI MTU UWE NA PROFESSION HUSIKA,AMBAPO NAAMINI KWA ELIMU ZA PERSONEL WALIOKO JESHINI NI WACHACHE SANA WATAWEZA KUWA NA HIYO PROFESSION.
SO KWA KAULI YA SERIKALI,NI CHANGA LA MACHO KWA WALE WASIOJUA UDHAIFU WA JESHI LETU
 
Back
Top Bottom