Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Wakati unaendesha gari kuelekea Loliondo au kutokea huko bila kificho mlima huu utauona bila kificho unaitwa Mount Oldoinyo Lengai, kwa kimasai wao wanamaanisha ni mlima wa Mungu!
Lake%20Natron03.jpg
du asante kwa picha
 
nimetoka huko juzi.shemeji yangu mke wa kaka yangu alikuwa na kisukari kwa zaid ya miaka 6......amepona mkuu wangu ..amepona kabisa.....

mkuu??? Sukari yake ilikuwa ngapi kabla na baada ya tiba?anaendelea na dawa za hospitali au kaacha?acheni porojo wakuu,acheni upotoshaji.
 
Ni tiba tu hamna kinga? Kwetu tunakisukari,nami najua in due time ntakipata. Ingependeza sana kama ingekua ni kinga pia. Coz BABU hatakuwepo yakinisibu.
 
Mimi nilipata dawa siku ya jumamosi tarehe tano mwezi Machi.
Hali ni mbaya na ya kutisha. Wagonjwa mahututi ni wengi na wangine wamefia pale na maiti zao kufungwa na mikeka na kupakiwa juu ya carrier ya gari kama mzigo.
Niliona askari wawili tu na mgambo wengi ambao walikuwa wanawatandika wagonjwa waliojaribu kukiuka utaratibu. mgambo walikuwa na madaraka kuliko mkuu wa kituo cha polisi.
Serikali ichukue hatua haraka kupunguza mateso makubwa wanayopata watu.
Kuwekwe kituo kila mkoa ambacho kitaratibu watu wanaotakiwa kwenda kutibiwa ili idadi hiyo iendane na uwezo wa babu kutibu kwa siku.
waafrika tunamapungufu makubwa katika kutumia karama tulizopewa na Mungu hata sasa askofu Kakobe ametamka kuwa huyu babu akanyagwe na kusambaratishwa kwa kuwa anatumia mashetani.
 
mkuu??? Sukari yake ilikuwa ngapi kabla na baada ya tiba?anaendelea na dawa za hospitali au kaacha?acheni porojo wakuu,acheni upotoshaji.

Hii ni time bomb. Kuna siku hapa watu watajuta kama wameacha kutumia dawa. Hii inayoitwa miujiza au maajabu si mara ya kwanza. Na hapa ndio ignorance yetu inapopatikana. Hivi ni dawa ya aina gani ili iwe administered basi inabidi mtu akajifiche maporini! Ni dawa gani hiyo isiyo transferable hadi mgonjwa apelekwe huko? Ni dawa gani hiyo inakuwa single dose then mtu anapona? Ni dawa gani hiyo ambayo ni lazima mtu mmoja tu ndio aitoe? Ni dawa gani hiyo.......................... Tutaulizana hapa muda si mrefu. Kwa ushauri tu, wale wanaotumia special dose wasiache unless wawe scientifically tested na hata huyo mtu dawa zake ziwe tested pia.
 
Mimi nilipata dawa siku ya jumamosi tarehe tano mwezi Machi.
Hali ni mbaya na ya kutisha. Wagonjwa mahututi ni wengi na wangine wamefia pale na maiti zao kufungwa na mikeka na kupakiwa juu ya carrier ya gari kama mzigo.
Niliona askari wawili tu na mgambo wengi ambao walikuwa wanawatandika wagonjwa waliojaribu kukiuka utaratibu. mgambo walikuwa na madaraka kuliko mkuu wa kituo cha polisi.
Serikali ichukue hatua haraka kupunguza mateso makubwa wanayopata watu.
Kuwekwe kituo kila mkoa ambacho kitaratibu watu wanaotakiwa kwenda kutibiwa ili idadi hiyo iendane na uwezo wa babu kutibu kwa siku.
waafrika tunamapungufu makubwa katika kutumia karama tulizopewa na Mungu hata sasa askofu Kakobe ametamka kuwa huyu babu akanyagwe na kusambaratishwa kwa kuwa anatumia mashetani.
Ona sasa habari kama hizi. Watu wanaenda pale kufuata umauti na taabu zisizo na msingi. Tunaweza kuilaumu serikali kwa kila jambo lakini mengine mengi tunajitakia.
 
Kama anatumia nguvu za giza kama alivyoropoka askofu Kakobe basi tusubiri kufa moja baada ya mwingine baada ya muda fulani kwa sababu dawa hii inatibu lakini inaweza kugeuka sumu kali ndani ya mwili baada ya muda. Sawa na mlevi wa pombe ambaye huona raha sana baada ya kunywa lakini siku inayofuta hulalamika hang over. Tumwombe Mungu atuepushe kwa hili.
 
Mwanzo wa mwaka huu niliamua baada ya tafakari ya muda mrefu niliamua kuwa na uhusiano na msichana niliyejihisi kuwa nampenda. Tumekuwa na urafiki wenye matumaini mazuri sana. Ni mtaratibu na mstaarabu sana, ana kazi yake nzuri na anaonekana anajiheshimu. Bado hatujaingia katika mapenzi ya kitandani, lakini tunatoka wote mara nyingi na rafiki zangu waliozoea kunitania na ubachela wangu wameshaanza kufikiria tofauti, kuwa kuna dalili nzuri hapa na wananiambia hivyo.

Habari ya babu wa Loliondo ndiyo imekuja kunichanganya. Huyu dada hajawahi kuniambia kuwa ana ugonjwa wowote ule. Cha ajabu, siku ya jumanne last week kanitumia ujumbe ghafla kuwa anaenda Loliondo, ati anapeleka ndugu yake mgonjwa akapate ile dawa ya miujiza iliyovumishwa kupatikana huko. Nimeulizia kwa rafiki zake wa karibu wamenihakikishia kuwa aliunga kwenye kundi la wenzie ofisini kwao waliokodi landcruiser waende huko na amechanga pesa yake mwenyewe wala hakuna mgonjwa mwingine wala nini. Karudi jana usiku. Saa hizi ninapotoka hapa kazini nataka nikamuulize mambo yalikuwaje huko, lakini jamani nina wasiwasi. Hiyo dawa kaenda kunywa anaumwa nini mbona hajawahi kuniambia? Na kwa nini kanidanganya anasindikiza mgonjwa kumbe ni yeye mwenyewe? Halafu safari ilikuwa ya ghafla mimi kanijulisha kwa sms keshapanda gari!

Wakuu naona haijakaa njema kabisa nafichwa kitu flani.
 
watu bana....nendeni mkapime....sasa hujawa na uhusiano nae wa kitandani hofu ya nini? si ushukuru na uwe makini sasa? pengine hakuwa amepanga kwenda akaamua dakika za mwisho kwenda,akaona hutamwelewa ndo akadanganya.....take it easy na zaidi kuwa makini na maisha yako.
 
labda kaenda kutia kinga mwilini.......kukushauri ni bora mkapime kabla ya kuingia uhusiano wa kitandani
 
mkuu sasa Babu wa Loliondo kakuharibia ni hapo? Kama amekunywa hiyo dawa huoni kama Babu atakuwa amekusaidia sana? Don't dont jump to conclusions. Who know labda alikuwa na tatizo la uzazi?
 
Usiwe na wasiwasi, kama alikuwa na ugonjwa ndio vizuri kashatibiwa.
Nahisi alienda kwa mkumbo wa wenzie ila alikwambia ana mgonjwa ili kuipa uzito safari.
 
kaka shukuru Mungu hukuingia nae kwenye uhusiano, mkiwa tayari inabidi upime, kisha msubiri miezi mitatu kisha mpime tena mara ya pili, hapo ndo ndoa yaweza kutangazwa kwa usalama.
 
Ha hahahahha...

Umeanza kumlaumu babu wa watu bure mkuu.Ni kwa muda ganiumemjua huyo Gf wako?kapime na pia muende pamoja tu.
 
Wanaume mnapenda kucontrol wanawake sana sasa hata hajafikia ngazi ya uchumba unataka kumpangia maisha . Mwache atumie uhuru wake mpk utakapoamua kumuoa
 
mkuu sasa Babu wa Loliondo kakuharibia ni hapo? Kama amekunywa hiyo dawa huoni kama Babu atakuwa amekusaidia sana? Don't dont jump to conclusions. Who know labda alikuwa na tatizo la uzazi?

Nashukuru kunitia moyo. Hii ya kunidanganya ndiyo imenisumbua sana. Lakini nina uzoefu wangu mwingine fulani ambao likitokea tukio la kunirudishia kumbukumbu zile huwa najiona mwenye balaa sana.
 
MAONI YANGU:

Kwa sababu CCM na Serikali yake hawawezi kufanya kazi hadi wasukumwe na Chadema, basi naomba Chadema na hasa Wizara KIVULI husika na mambo ya Afya, Usafiri, Maji, Mawasiliano nk wafanye kikao na kuingilia kati hili swala.

Kama alivyopenedekeza mmoja wetu hapa, iwepo ofisi ya Booking mjini au mji mdogo sehemu fulani na watu wawe wanakwenda huko kwa makubaliano mapema. Iwepo booking na watu wajue watafika lini huko. Hawa wa bahati mbaya, waachwe wale tu ni mahututi na wenyeji wa eneo hilo ambao hawataweza tena kwenda hadi Arusha kufanya Booking.

Vinginevyo basi, hao watu wa kusimamia Booking, wawepo hapohapo kwa Babu na Computer zao/Simu zao. Unaweka booking na kujua kabisa siku fulani ndiyo uende.

Hivi vitengo vya kushughulikia MAJANGA kwa Tanzania vipo kweli au ni POROJO tu?

Chadema naomba tena, mkilivalia njuga hili swala, CCM watakurupuka kama kawaida ya na kujifanya ni lao. Ila mwisho wa siku, watu watafaidika na kupunguziwa matatizo yanayokwepeka. Utafikiri sijui tunaishi dunia gani?

Naomba watu wa Chadema wajulishwe kuhusu hii kitu na kwenye mawazo mengine basi na tuboreshe na utaratibu mzima wapelekewe Chadema na hapo watakapoutangaza, basi FIMBO itamchapa Kalumekenge na Kalumekenge (CCM) atakwenda shuleni..........
 
Wasiwasi wako ni nini? Kama ana ukimwi si umesema hamjachakachuana!! Ili kukata mzizi wa fitina nashauri mkacheki afya zenu.
 
Back
Top Bottom