Nimemchukia mno Baba Mdogo baada ya kujimilikisha nyumba na eneo la babu

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,770
4,260
Kwa ufupi ni kwamba, babu yangu katika pilikapilika za kutafuta alifanikiwa kumiliki eneo ambalo lipo jirani kabisa na barabara ya lami, baada ya kustaafu katika shughuli za kiserikali basi akaamua kuhamia kijijini ambapo alifanikiwa kununua shamba na akajenga..

kule mjini akajenga pia nyumba ya vyumba viwili baada ya ile mwanzo kuchakaa,japo hakufanikiwa kuifanyia finishing..utata ukaanzia pale ba mdogo alipokuja kumuomba babu amalizie hiyo nyumba na atakaa hapo hadi gharama alizotumia kwenye finishing ziishe ndipo ahamie kwake..bila hiyana babu akamkubalia ba mdogo na familia yake wakahamia hapo ila cha kushangaza akaanza kuongeza vyumba vingne bila makubaliano, na mwishowe amegoma kabisa kutoka hapo na anadai ni kwake,..

babu alipofariki mwaka Jana, ding mdogo amegoma kabisa eneo hilo analoishi kujumuishwa kwenye Mali za babu, kiukweli nimekuwa disappointed sana na Tabia ya unyang'anyi na dhuluma aliyoionyesha dingo mdogo..

pamoja na kuwa namiliki viwanja vyangu maeneo mbalimbali na pia nna mijengo yangu binafs nimeshindwa kumsamehe na namchukia yeye pamoja na kizaz chake kwa kitendo cha dhuluma alichofanya..

Ushauri: kama kuna MTU anataraji kuiga Tabia hii, basi jiandae na vita vikali vya kifamilia don't dare (usithubutu).
 
Warithi ni watoto tu.

Swali a kujiuliza: baba yako yupo hai?
Kama yupo hai kwa nini kakaa kimya?
Kama hayupo hai wewe sio sehemu ya warithi.

Na kama alikufa kabla ya babu yako, mtu harithiwi Mali zake mpaka awe amefariki na watoto wake au mtu aliye mchagua.

Lakini vipi ikiwa alimpa mwanae kwa sharti la kupaendeleza?

Hapo mtamalizana, kaa mbali na Mali za urithi.
 
Kuna dogo mwingine tu hapa kitaa, alikuwa anagombana na watoto wa marehemu kisa Mama yake aliolewa na marehemu baada ya Mke wa yule marehemu kufa na kuacha watoto wawili na huyu dogo anayegombana na watoto wa marehemu sio mtoto wa ndoa wa marehemu
Huyo dogo akili hana.
Ila ikiwa jasho a mamaye lilitumika kwenye utafutaji.ana haki.
 
Nami niliwahi kuwa na akili za kijinga kama hizi

babu alioa wake wawili na alikuwa na eneo zaidi ya hekari 50. Kabla hajafa kawakabidhi watoto wa bibi yangu mdogo. Bibi kizaa baba hakuambulia chochote.

Nikajidai kiherehere kumuuliza babu alinipa jibu moja ambalo lilibifanya nami nitafute vyangu

Alinijibu; kwanza shukuru eneo langu limewatunza hadi kuwafikisha umri huo wa kujitegemea . Nilipitia dhiki kubwa kuliko wenzangu waliouza maeneo yao wakaacha familia zao wakiangaika pa kulima na watoto wao kufa kwa utapia mlo.

Niliacha ili liwakuze mjitegemee kutafuta vyenu kama nilivyotafuta mimi. Je ningeamua kuuza hili eneo hata kabla hamjazaliwa leo hii ungekuja kuniuliza ujinga huo. Usinipangie nani wa kumpa kitu changu. Tafuta vyako usubirie wajukuu zako waje kukupangia wa kuwagawia.

Niliondoka bila kuaga. Nikapambana kivyangu sasa nina hekari 100 nazomiliki nasubiria wajukuu waje waniketee kihelehele kunipangia nani wa kumugawia
 
Nami niliwahi kuwa na akili za kijinga kama hizi

babu alioa wake wawili na alikuwa na eneo zaidi ya hekari 50. Kabla hajafa kawakabidhi watoto wa bibi yangu mdogo. Bibi kizaa baba hakuambulia chochote.
Nikajidai kiherehere kumuuliza babu alinipa jibu moja ambalo lilibifanya nami nitafute vyangu

Alinijibu; kwanza shukuru eneo langu limewatunza hadi kuwafikisha umri huo wa kujitegemea . Nilipitia dhiki kubwa kuliko wenzangu waliouza maeneo yao wakaacha familia zao wakiangaika pa kulima na watoto wao kufa kwa utapia mlo. Niliacha ili liwakuze mjitegemee kutafuta vyenu kama nilivyotafuta mimi. Je ningeamua kuuza hili eneo hata kabla hamjazaliwa leo hii ungekuja kuniuliza ujinga huo. Usinipangie nani wa kumpa kitu changu. Tafuta vyako usubirie wajukuu zako waje kukupangia wa kuwagawia. Niliondoka bila kuaga. Nikapambana kivyangu sasa nina hekari 100 nazomiliki nasubiria wajukuu waje waniketee kihelehele kunipangia nani wa kumugawia
Sasa hizo hasira
 
Urithi limekua janga kubwa sana hapa nchini vijana wengi wa siku hizi wanawaza urithi tu pasipo kutafuta wao wenyewe.
Kuna familia moja nilikuta wanagombana hadi kupelekana mahakamani kisa mjomba kauza sehemu ya ardhi kwa mfanya biashara wa hizi petrol station.
Mjomba mtu alichukua kama ml 70 ? Kitendo hicho kikawafanya wajomba( watoto wa marehemu dada yake) waje wadai urithi wa mama yao aliefariki.
Mahakamani mjomba wao akawakana mimi hawa siwajui naomba mahakama iwaulize wanatoka ukoo upi na majina yao wanaitwa wakina nani?
Mwisho wa siku mjomba akashinda kesi.
 
Nami niliwahi kuwa na akili za kijinga kama hizi

babu alioa wake wawili na alikuwa na eneo zaidi ya hekari 50. Kabla hajafa kawakabidhi watoto wa bibi yangu mdogo. Bibi kizaa baba hakuambulia chochote.
Nikajidai kiherehere kumuuliza babu alinipa jibu moja ambalo lilibifanya nami nitafute vyangu

Alinijibu; kwanza shukuru eneo langu limewatunza hadi kuwafikisha umri huo wa kujitegemea . Nilipitia dhiki kubwa kuliko wenzangu waliouza maeneo yao wakaacha familia zao wakiangaika pa kulima na watoto wao kufa kwa utapia mlo. Niliacha ili liwakuze mjitegemee kutafuta vyenu kama nilivyotafuta mimi. Je ningeamua kuuza hili eneo hata kabla hamjazaliwa leo hii ungekuja kuniuliza ujinga huo. Usinipangie nani wa kumpa kitu changu. Tafuta vyako usubirie wajukuu zako waje kukupangia wa kuwagawia. Niliondoka bila kuaga. Nikapambana kivyangu sasa nina hekari 100 nazomiliki nasubiria wajukuu waje waniketee kihelehele kunipangia nani wa kumugawia
Wahindi....waarabu....ndio wanatuzidi kwenye mambo haya...
 
alifanikiwa kumiliki eneo ambalo lipo jirani kabisa na barabara ya lami,
Wapi huko ?
1711402330016.png
 
Mimi nilikataa habari za urithi wa mali kitambo.

Nitarithi something symbolic kama Biblia ya familia na michoro ya Kiinjinia ya Mzee wangu.

Vingine hivyo mambo ya mali watagawana wadogo zangu.

One.
 
Kuna dogo mwingine tu hapa kitaa, alikuwa anagombana na watoto wa marehemu kisa Mama yake aliolewa na marehemu baada ya Mke wa yule marehemu kufa na kuacha watoto wawili na huyu dogo anayegombana na watoto wa marehemu sio mtoto wa ndoa wa marehemu
"sio mtoto wa ndoa wa marehemu", ukizaa mtoto wa ndoa na mtoto asiye wa ndoa tofauti yao kwako ni nini? Mmoja ni mwanao kidogo na mwingine mwanao sana? Naomba ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom