Hivi ujio wa Babu wa Loliondo ulipangwa na kundi fulani au babu na kundi lake walipanga kula 500/=na kutupima ujinga wetu?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Kwanza nitoe pole kwa kifo cha mchungaji mzee wetu mwaisapila "Babu wa loliondo."

Nije kwenye ajenda husika. Babu wa loliondo aliutangazia umma kuwa kaoteshwa na mungu dawa ya kutibu magonjwa sugu kama vile UKIMWI, pressure, kisukari n.K nilitarajia kusikia serikali imemtaka apeleke dawa zake zikafanyiwe utafiti kwanza kama kweli zinatibu ili apewe kibali cha kutibu.

Badala yake Wananchi walimiminika loliondo kwa misafara mirefu ya magari makubwa kwa madogo malori kwa mabasi licha ya ubovu wa barabara uliosababisha magari kukwama na wagonjwa kufariki kabla hata ya kunywa kikombe cha babu.

Kikombe kilichopatikana na kugawiwa na babu mwenyewe tu na hakuna aliyeruhusiwa kugawa kikombe baada ya kulipa sh.500/= tu

Kilichonishangaza ni serikali bila kujiridhisha kuwa dawa ya babu kama inatibu ilianza kukarabati barabara. Kingine kilichonishangaza ni ujio wa viongozi wa Serikali kushiriki unywaji wa kikombe cha babu huku wakijua tiba ya babu haijafanyiwa utafiti na serikali.

Swali ya kujiuliza
Kwanini serikali iliiamini tiba ya babu wa loliondo bila kuifanyia utafiti na ikawaacha wananchi kuitumia?

1. Je endapo ingetokea tiba ya babu ikaua wananchi mamia kwa maelfu lingekuwa kosa la babu wa loliondo wananchi waliokunywa au serikali kutokuifanyia utafiti?
2. Je ujio wa babu wa loliondo ulitengenezwa na kundi fulani la wahuni kwa kushirikiana na babu wa loliondo mzee mchungaji mwaisapila ili kujipatia fedha na kutupima ujinga watanzania?
 

Attachments

  • cadhho.jpg
    cadhho.jpg
    34.2 KB · Views: 3
  • JamiiForums198023176.jpg
    JamiiForums198023176.jpg
    9.4 KB · Views: 8
  • JamiiForums625727970.jpg
    JamiiForums625727970.jpg
    9.3 KB · Views: 9
Moja kati ya somo zuri linalohusu saikolojia!.. huyu mzee alijua kucheza na bongo za watu bhana!.
Mkuu hii itakuwa Kuna mkono wa mtu mnono ulihusika hapo media zikanunulika kwa vipande kadhaa vya shekeli!.
Au kama sivyo basi mzee kipaji chake ni chahali ya juu... Tukio la loliondo lilikuwa ni tukio lakutupima tumekuwa kiasi gani nafikiri matokeo mnayo...😂
 
Watu walipuuza hata matamko ya wakuu wa dini zao! Maana imani huanzia unapoanzia kuamini, kikubwa Pendaneni sana!
 
Back
Top Bottom