Nini kimempata Nassari?

Makinda ni kiherehere tu Nassari alisema ratiba ni kuapishwa trh 11 saa 3 asubuhi na ataondoka Arusha trh 10 yaani leo na habari zilizopo yuko njiani. Haya mengine ni mbwembwe tu Spika hana ujanja wowote zaidi ya kumwapisha mbona Sumari hakuapishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na marupurupu alikuwa anapata kama kawaida.
 
Mimi sijangai kwa akili ya huyu dogo alisema tangu kwenye kampeni kuwa huko anakwenda kutafuta mchumba labda amempata na yuko nae honey moon. Sio jambo la kawaida hili. Aibu na fedheha kwa wapiga kura
Kwa akili yako unadhani Sioi atapewa ubunge badala yake.
 
Babu yake na ninahisi kwasababu viongozi wetu bwana mmmmmhhh.
Nafikiri haukufuatilia pindi alipotangazwa mshindi,ktk mahijiano yake na vyombo vya habari alisema 'tumeanza mungu na tutamaliza mungu' sasa babu ni yupi?
 
Wewe Bukanga matusi hayana tija kwani hizo ndizo hisia zangu hivyo ungepaswa kunipa hoja za kuniondoa kwenye hisia hizo kama si za kweli sasa tukianza kujibizana kwa maneno machafu ni kutatua tatizo au kulijenga
 
sioni sababu ya kwenda na msafara dodoma! Na hata kama kuna huo ulazima kwanini usiende hata jana? Wana jf tuliwekewa uzi humu ukionyesha ratiba ya shughuli za bunge na ilionyesha wazi shughuli ya kwanza ni kuapishwa wabunge wapya! Iweje muhusika mwenyewe asifahamu? Au kapuuzia? Sisi wote ni cdm lakini tujifunze kukubali kukosolewa tukikosea
 
Kupata ridhaa ya kuuwakilisha umma ndio issue ya msingi. Kuapishwa bungeni sio case sensitive sana, ataapishwa siku nyingine.
 
Mkekuu siyo wote walitajao jina la Mungu na wakaweza kuona ufalme wa Mbinguni
 
Wewe Bukanga matusi hayana tija kwani hizo ndizo hisia zangu hivyo ungepaswa kunipa hoja za kuniondoa kwenye hisia hizo kama si za kweli sasa tukianza kujibizana kwa maneno machafu ni kutatua tatizo au kulijenga

Nasena hivi punguza hisia mkuu!!
 
Marehemu Jeremiah Sumari mbunge aliyepita toka Arumeru Mashariki mpaka anafariki alikuwa bado hajaapishwa Bungeni, hivyo hili siyo jipya!
 
Tumeshuhudia kabla ya kuanza shughuli nyingine za bunge,spita alimhitaji joshua na mwenzake wakapate uthibitisho wa ubenge wao,yaani kiapo sasa hawakuwepo ni kitu cha kushangaza kidogo.ila hatujui kilichowasibu ni vyema km kuna mwana jf anafahamu atutaarifu.
 
sioni sababu ya kwenda na msafara dodoma! Na hata kama kuna huo ulazima kwanini usiende hata jana? Wana jf tuliwekewa uzi humu ukionyesha ratiba ya shughuli za bunge na ilionyesha wazi shughuli ya kwanza ni kuapishwa wabunge wapya! Iweje muhusika mwenyewe asifahamu? Au kapuuzia? Sisi wote ni cdm lakini tujifunze kukubali kukosolewa tukikosea

huu ni uzembe wa uongozi chadema..chadema vitu vingi tunafanya kama tupo kwenye kampeni kwa hali hii kunatofauti gani na wasira anaelala bungeni.?
 
Back
Top Bottom