Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,140
- 13,215
Joshua Nasari hayupo bungeni leo kuapishwa....
Hapana mkuu, ataapishwa kesho kutwa.
Kulikuwa na kutoelewana baina ya viongozi wa Chadema waliopo hapa Dodoma na Uongozi wa bunge. Chadema waliomba wabunge Hao waapishwe kesho, lakini kanuni zinasema wabunge wapya wataapishwa siku ya kikao cha kwanza na shughuli hiyo itakuwa ya kwanza. Lakini katibu wa bunge hakuwaeleza hivyo Chadema na ndio maana hata matangazo yaliyotolewa awali yalionyesha kuwa hawataapishwa Leo. Lakini kikao Kilipoanza asubuhi ikaonekana kwenye order paper kuwa uapishwaji unapaswa kuwepo. Lakini Chadema na bunge wameelewana na sasa Nassari na mwenzake wataapishwa Alhamis. Kesho Nassari atafanyiwa orientation.
Msafara wake, ukiongozwa na Mbowe na magari zaidi ya kumi ndio umeingia Dodoma kwa mbwembwe kama nusu saa iliyopita