Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,627
Wanabodi,
Kwa Maslahi ya Taifa ya Jumapili ya leo, 12 February, 2023
KONGOLE JAJI MKUU WA TANZANIA KUSISITIZA UMUHIMU WA USULUHISHI KUTATUA MIGOGORO, KUTAKUZA UCHUMI
Kwa Maslahi ya Taifa leo, inawachambulia sehemu ya hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamisi Juma kwenye Siku ya Sheria ya mwaka huu 2023 iliyofanyika katika uwanja wa Chinangali jijini Dodoma, na kwa vile mimi nawaandikia wananchi wa kawaida kabisa, baadhi ya vifungu vya sheria, nitaviacha na kuwaachia wanasheria, wananchi wa kawaida wanachotaka ni haki, kutendewa haki na haki kuonekana inatendeka.
Kauli mbiu ya siku ya sheria mwaka huu wa 2023 inasema “UMUHIMU WA UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA YA USULUHISHI KATIKA KUKUZA UCHUMI ENDELEVU: WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU”, Jaji Mkuu Prof. Juma amesema umuhimu wa usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ni kwa mujibu wa Inara ya 107 ya Katiba inayoitaka Mahakama katika kutoa uamuzi wa mashauri, inatakiwa kuzingatia kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro. Kanuni hii ya Katiba inazingatia faida kubwa za matumizi ya usuluhishi katika utatuzi wa migogoro zikijumuisha kupunguza gharama na muda wa kuendesha shauri na kuendeleza undugu miongoni mwa wadaawa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) imeweka Kanuni mbili muhimu ambazo bado hazizingatiwi kikamilifu na mhimili wa mahakama wakati wa kusikiliza mashauri Mahakamani na hivyo kusababisha uchelewaji mkubwa wa mashauri na kuongeza gharama za uendeshaji wa mashauri. Ibara ya 107A (2) (d) imetamka kanuni inayoitaka Mahakama, wakati inasikiliza mashauri ya madai au jinai, kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro. Ibara ya 107A (2) (e) imetamka kanuni nyingine muhimu sana kuwa, katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa mujibu wa sheria, Mahakama zitende haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.
Sio mara moja wala mbili tumeshuhudia wananchi wengi wakikosa haki zao mahakamani kwa kesi zao kutupwa kwasababu tuu ya makosa ya kiufundi, “legal technicalities”, na hili sio kosa na mhusika ni kosa la mawakili.
Mfano mzuri ni kesi ya mwanasiasa Zitto Kabwe alipovuliwa unachama wa Chadema aliwa ni Naibu Katibu Mkuu, (NKM), kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, mamlaka ya nidhamu ya NKM ni Baraza Kuu, Kamati Kuu ya Chadema, ilipata wapi mamlaka na uwezo wa kumfuta uanachama NKM wakati sio mamlaka yake ya nidhamu?!.
Zitto alikimbilia mahakamani na kesi yake ikatupwa kwa makosa ya kiufundi!, hivyo kupoteza haki yake, na baada ya kushindwa kesi, katiba ya Chadema imeweka kifungu kinachokwenda kinyume na katiba ya JMT, kuwa mwanachama wa Chadema haruhusiwi kufungua shauri mahakamani dhidi ya chama, na akifungua, akishindwa anakuwa amejifukuzisha uanachama!, hivyo Zitto baada ya kushindwa kesi, akafungasha kwa kuliaga Bunge na kujitoa Chadema huku Chasema wenyewe wakishangilia kumtimua!. Niliwapa Chadema angalizo Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" bahati mbaya sana Chadema hawaijui karma, hivyo hawajui the consequences za kudhulumu haki za wanachama wake!.
Sasa hivi kuna kesi nyingine mahakamani dhidi Chadema kwa mazingira yale yale kama ya kesi ya Zitto. CC ya Chadema imekaa tena kama kawaida yake, as a kangaroo court na kumtimua Halima Mdee!, huyu ni Mwenyekiti wa Bawacha, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, CC ya Chadema inapomtimua Mwenyekiti wa Bawacha, imepata wapi mamlaka hayo ya kumfuta uanachama mtu kama Halima Mdee, wakati CC hiyo sio mamlaka yake ya nidhamu?.
Mamlaka rasmi ya nidhamu ya Halima Mdee ni Baraza Kuu, Chadema ilishindwa kuitisha kikao cha Baraza Kuu kwasababu fulani, (naijua), thanks God, kukajitokeza Msamaria mwema fulani, (namjua), akawezesha kikao cha Baraza Kuu kikaitishwa, hii sasa ndio mamlaka sahihi ya nidhamu ya Halima Mdee, kwanini kikao cha Baraza Kuu kilipoitishwa shauri la Halima Mdee halikusikilizwa?, na badala yake kikao cha Baraza Kuu kilikaa kama mamlaka ya rufaa kwa wabunge waliotimuliwa na CC ya Chadema, lakini kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha ni Baraza Kuu, na mamlaka yake ya rufaa ni Mkutano Mkuu. Chadema imekuwa ikitumia hizi loopholes za legal technicalities kuwahukumu wanachama wake kikangaroo court na kushangilia utimuaji huo bila kupima the consequences, amini nawaambia the karmic consequences za kuwatimua kama mbwa, watu waliokipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu ni devastating!. Mpaka sasa Chadema wanayo chance ya usuluhishi na hao wabunge wao 19 waliowatimua Kikangaroo.
Kufuatia Zitto kushindwa kesi yake kwa legal technicalities, nikatoa angalizo The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! sasa angalau mahakama imekubali kuwasikiliza, natumaini safari hii mahakama itatenda haki. Ila hata kama mahakamani watashindwa na Chadema kufanikiwa kuwatimua, the consequences will be devastating for Chadema kama nilivyo eleza hapa Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari limetunga sheria kufanikisha matumizi ya usuluhishi kwa kupitisha Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.1 ya mwaka 2020 [Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act No. 1 of 2020] iliyozifanyia marekebisho Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai (SURA YA 33) kwa kuongeza Kifungu kipya cha 64A, kinachotamka kuwa, wadaawa, sasa wana hiyari ya kutatua mgogoro wao nje ya Mahakama.
Endapo wadaawa watafikia makubaliano nje ya Mahakama, watayasajili katika ngazi husika ya Mahakama na makubaliano hayo yatakuwa na nguvu ya amri ya mwisho ya Mahakama katika mgogoro huo. Ni wajibu wa Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea; kila mara kuwakumbusha wadaawa uwepo wa hiyo nafasi ya kutatua migogoro nje ya Mahakama kwa nia hiyo hiyo ya kuwataka wenye migogoro kutumia usuluhishi badala ya kukimbilia Mahakamani, hii iboreshwe zaidi kwa kutungwa sheria kuwa kesi zote za madai, lazima kwanza zianzie usuhishi ukishindikana ndipo ziende mahakamani.
Jaji Mkuu Prof. Juma, ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuweka mazingira ya kisheria ya kusuluhisha migogoro nje ya Mahakama kwa kutoa orodha ya wasuluhishi. (d) Mihimili ya Bunge na Serikali Inatambua Usuluhishi ni Tiba ya Ucheleweshwaji wa Mashauri Mahakamani. Kauli mbiu hii, inatoa tahadhari kwa Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea ambao ndio wahusika wakubwa wa uendeshaji wa mashauri Mahakamani. Mihimili ya Bunge na Serikali, tayari imeelewa kuwa dawa ya ucheleweshwaji wa mashauri Mahakamani ni usuluhishi ambao tayari umewezeshwa kwa kutungiwa Sheria nyingi katika maeneo mbali mbali ambayo usuluhishi unawezekana.
Mhimili wa Mahakama na wadau wake, wataonekana kuwa wameshindwa mtihani wa viapo vyao na wajibu wao kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi wasipotekeleza wajibu wao wa kufanikisha Usuluhishi. Wananchi wanayo haki kuwashtaki mhimili wa Mahakama kwa mhimili wa Bunge, wakiona haki inachelewa kwa kujiuliza kwa nini Mhimili wa Mahakama hautumii Sheria zilizotungwa na Bunge, kuwasaidia wananchi kutatua migogoro kwa njia ya Usuluhishi?.
Mhimili wa serikali usipotenda haki unaweza kushitakiwa kwenye mhimili wa Mahakama na mahakama iakiamuru serikali kutenda haki, lakini ikitokea mhimili wa Bunge kutotenda haki kama Bunge letu kututungia sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba, na mahakama ikauthibitisha ubatili huo, kwanza ilipaswa Mahakama kuzibatilisha sheria batili hizo pale pale zilipothibisha ubatili wa kwenda kinyume cha katiba kwasababu anayebatilisha sheria batili zilizokwenda kinyume cha katiba, zinabatilishwa na katiba na sio Mahakama, kazi ya Mahakama ni kutangaza tuu ubatili huu, na ubatili ni ubatili wa void ab initio.
Bunge litunge sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, mahakama ikathibitisha sheria hiyo ni batili, kwanini Mahakama Kuu haikubatilisha sheria hiyo pale pale na badala yake kuiamuru serikali kuibadili na Mahakama ya Rufaa ikaurudisha ubatili huo kwa Bunge lile lile lililotunga ubatili huo ndio liuondoe hii imekaaje?.
Baada ya Bunge kutunga sheria batili ilitakiwa
1. Sheria batili ikiishatangazwa ni batili, ubatili huanzia hapo hapo na kubatilika pale pale!.
2. Bunge lilipaswa kuadhibiwa kwa kutunga sheria batili
3. Bunge kuamriwa kutunga sheria halali.
Lakini mfumo wetu wa utawala wa mihimili mitatu, hauna utaratibu wowote wa kuliadhibu Bunge letu linapokosea!.
Na mhimili wa Mahakama ni vivyo hivyo, mhimili wa Mahakama unapo wakosea wananchi kwa kutowatendea haki, ilibidi wananchi wawe na uwezo wa kuishitaki Mahakama kwa mhimili wa Bunge na Bunge kuwa na uwezo wa kuiadhibu mahakama pale ambapo mahakamani haijatenda haki kwa Watanzania, na mfano mzuri ni ile kesi ya Mtikila ya mgombea binafsi.
Mahakama Kuu imetamka wazi shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa kugombea uongozi ni shurti batili linakwenda kinyume cha katiba na kuamuru mgombea binafsi rukhsa na kuiamuru serikali kuandaa utaratibu. Mahakama ya Rufaa ukawakosea sana Watanzania kwa kulirejesha suala hili Bungeni, hakuna utaratibu wowote rasmi wa kuishitaki mahakama pale mahahama isipotenda haki, zaidi ya kuwatuma wabunge wetu kulalama tuu Bungeni la Bunge haliwezi kuufanya chochote mhimili wa Mahakama!.
Upo ushahidi kuwa Mihimili ya Bunge na Serikali ina ufahamu mkubwa kuhusu manufaa ya usuluhishi. Mhimili wa Mahakama na Wadau wake tukiwemo sisi mawakili, tutajiweka katika mazingira hatari mbele ya macho ya wananchi, endapo hatuzitumii Sheria zinazotoa nafasi za usuhishi na Sheria zinazotuzuia kutumia kanuni za kiufundi kuchelewesha haki.
Tukutane wiki ijayo kwa muendelezo wa makala hii kuhusu umuhimu wa usuluhishi na jinsi Rais Samia anavyotumia usuluhishi kuliponya taifa letu kisiasa hivyo kujikuta tunajiponya kiuchumi na kijamii.
Wasalaam
Paskali