Niko njiapanda Sijielewi Jamani

haya ndio matatizo ya kuanza mambo ya mahusiano ukiwa tayari akili imekomaa. 1st love mara nyingi inapagawisha. kucharuka mapema kuna faida zake, hakuna kupagawishana, mtu akikuzingua, tosa kule songa mbele, hakuna kuwaza wala nini, kwani huyo leah ndio kabeba maisha yako? mwanake umekutana nae na meno ya 32 mdomoni leo anakufanya utake kufukuzwa kazi. hebu songa mbele. hata kama ameanza kukupigia, achana nae..!! hakukufikiria wakati wewe unamuhitaji, sasa leo wa nini. huyo hata ukimuoa atakuchezea akili, amka kijana.

SAL,
Asante kwa ushauri wako.Amenisababishia hasara nyingi sana za kihali na kimali lakini nashangaa bado ati nampenda.Basi inabidi nichukulie kama nimefiwa na mtu muhimu kwangu afu niachane nae.
 
kama bado hujaelewa, inabidi upewe sup.
Kuna wengine huwa hawaelewi hadi sup na carry over.
 
Nimemuona Kongosho kachangia, nasubiri nimuone Lizzy, smile, AshaDii na yule mwingine mwenye jina la kifaransa. Hao naamin watatupa opande wa pili wa shilingi(about ladies) then mie ntarudi ku-summaries!
 
Wana jamvi'

Napiga hodi Jukwaani'

Nina tatizo la kimapenzi la mda mrefu ambalo naamini humu JF ndo mahala naweza kupata ufumbuzi wa tatizo langu.

Inahusu maisha yangu ya kimapenzi, Miaka minne iliyopita (2009) niliingia kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa mapenzi,Nikakutana na Leah akiwa mwaka wa kwanza chuoni mimi nikiwa mwaka wa pili.Huyu binti nilimpenda sana naye alionesha kuwa ananipenda,tukakubaliana kwa pamoja kuwa wapenzi,tukaweka misingi ya kutofanya mapenzi hadi tukioana,tukafanya mambo mengi pamoja,tukawa pamoja mda mwingi,fedha kidogo niliyokuwa nayo nilijibana kwa ajili ya kumtimizia mahitaji yake madogo madogo.Tulitambulishana kwa ndugu zetu wa karibu,kweli tukawa wawili.Mimi binafsi nilimpenda sana kuliko mnavyoweza kudhani.

Nikiwa mwaka wa tatu na yeye akiwa mwaka wa pili nikaanza kuona mabadiliko kidogo,lakini siku namaliza mtihani wa mwisho chuoni na kumaliza degree ya kwanza akaniacha rasmi bila sababu ya msingi.Aliniathiri sana mambo yangu mengi wakati huo nilikua na scholarship ya masters UK nikashindwa kwenda kwa sababu nilimiss deadline kwa sababu nililazwa hospitali kwa muda wa mwezi mzima na ushee.

Nilikua na bahati kwani mara tu baada ya kumaliza shule nilipata na ajira wakati huo nikiwa nimelazwa.Nikaanza kazi lakini nikiwa bado siwezi kukaa bila kumfikiria Leah,efficiency yangu kazini ikawa sio nzuri.Bosi wangu akaniita akanisihi nimwambie nini kinanisibu,ilinibidi nimweleze.Kwa busara zake akaamua kunipa likizo ya mwezi mzima na leave allowance hapo nikiwa na miezi miwili tu kazini.

Nikarelax kidogo.Baada ya miezi mitano nikapata msichana mwingine,huyu ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza kufanya nae mapenzi.Lakini nikawa bado simpendi kutoka moyoni.Hakuna siku wala saa inapita bila kumuwaza Leah.Nikawa nashindwa kum care huyu msichana kwa sababu moyo wangu hauko kwake.Tukaamua kuvunja uhusiano.

Mwaka 2011 Februari nikawa na msichana mwingine ambae niko nae hadi sasa,huyu ananipenda kwelikweli hadi mimi hua naogopa.Lakini moyoni mwangu nalazimisha kumpenda.Ukweli nampenda Leah.Bado siwezi bila yeye.

Naomba mnisaidie;

1.Huyu wa sasa ananipenda sana lakini moyo wangu haupo kwake,nifanyeje?
2.Leah anaonesha kutonipenda kabisa kwa sababu hata nikimpigia simu hapokei,lakini nampenda kulikoni,nifanyeje?
3.Naogopa kuja kuwa mume msumbufu kwa familia pale nitakapooa nisiyempenda kwa dhati,nifanyeje?


....umeniudhi sana
, ulipozaliwa uliambiwa bila huyo leah hutaishi?
acha upuuzi wewe. unapoteza wakati wako bure kung'ang'ania
penzi lililokwisha nyauka!

...nakuapia, huyo leah akikurudia na kukuacha tena
utajiua wewe!
 
shukuru umempata wingine ambaye anakupenda sana.kumpata anayekupenda ni msaada mkubwa katika kumsahau huyo aliyekutosa.kuna watu wanatoswa na hawapati watu wakuapnda kwa dhati kama ww? can u imagine?
kinachokusumbua na kukuumiza ni kule kuachwa na mtu ambaye ulimpenda, kumthamini na kumsaidia,bado unamaumivu ya kudharauliwa,lkn si dhani kama bado unampenda kama mwanzo. na hata kama akirudi uwe nae tena unaweza ukaishia kulipiza kisasi kwa kumsaliti ili upunguze maumivu.
Mpotezee tu,
 
yalishawakuta wengi nami pia nna experience na jambo kama lako lakini nilifunguka bro' nikafuta fikra hizo nikaanzisha mawazo mapya kwenye kichwa changu, nakutengeneza hisia kuwa ni mtu hatari na ni adui mbaya kwangu kwani athamini chcote kile mlichofanya au kutafakari mkiwa pamoja.
nikajenga mawazo mapya kwani ilikuwa the same unampata akupendaye lakini unang'ang'na na uyo ni mateso makubwa njia yangu ilikuwa ni kusali sana kumwomba mungu akusaidie kumtoa moyoni mwako na kufunga karoom kaliko ndani ya moyo wako kalikojaa yeye na kukufungulia chumba kipya ndani ya moyo na ubongo wako ili uingize vipya wallahh! tena utashangaa nakujiona ulikuwa mbumbumbu wakati huo. funguka sasa achana na kuwaza ya zamani jenga uhusiano mpya mpende akupendae na mkubali kuwa ni zaidi ya yule kwa kila jambo haswa kwa upendo wake fikiri jinsi anavyojituma kukupenda je naye akikuacha utafanyaje? achana nae uyo leah ni mtu hatari kwako kwakuwa ameweza kutwist mind yako atakavyo hilo ni pepo ama la ni jinamizi. pole sana
 
Kaka siku nyingine ukome na hiyo staili yako ya mpaka muowane ndo mfanye.Ndo hasa kinachokuuma hapa wala sio mapenzi ya kihivyo.Cha kufanya wewe mpotezee tu endelea uliyekuwa nae sasa hivi.Au kama unaweza endelea ku mwinda ukimpata una mtupia nyavu halafu unatulia kwa huyu wa sasa.

kweli binadamu tupo tofauti sana, mimi mtu ambaye haatujaoneshana makalio yetu, akiniacha, namsahau ndani ya week moja
 
Loh me mwaya sina cha kukuambia zaid ya pole weeee.
kama leah hana hata dalili yan hakupendii kbs ya nn kujiumiza ivyo jaman.
mpende akupendae asiyekupenda achana nae, acha mapenzi ya movie na tamthilia kijan grow up and move on!! kwa maneno mengine maisha lazima yaendelee alaah.
 
Mimi ushauri wangu kidogo ni weird

Freeland....najua kuna kitu kinakusumbua kwamba kwanza ulimpenda sana, pili ulikubali kuvumilia hadi muoane, tatu ulimgharimikia sana, nne akakuacha bila sababu (bila shaka alishoboka)

Hapa hatuna nafasi ya kusikia upande wa pili wa shilingi., ila kama unayosema ni kweli na kweli tupu, ten unastahili remedies.

Bila kujali wala kuathiri mahusiano yako ya sasa.....akikupigia simu huyo Leah hebu onana naye, msikilize anasema nini, kisha mmombe mkamalizie pale mlipoishia. Ninaamini kabisa mkimalizie pale hutakuwa unajisikia maumivu kiviile. Hadithi hapa ni kwamba umelipia 'mzigo' kisha haujawa delivered. baas

Changamka fasta kisha huyooo unarudi zako...tena ndo utaona kuwa huyo Leah kumbe hana cha ajabu saaana na huyu wa sasa kama ulivosema anamfunika.

jamani ni mawazo yangu hayo.
 
Dah!! wewe mwanaume wewe!!!!!
Yani nimeishiwa cha kukwambia km hujamuelewa Mr Rock na wengine mambo waliyokuambia,
Nakushauri hivi,
Ili uweze kumsahahu huo lea wako kwanza achana na huyo dada wa watu aliyejitoa kukupenda kwa moyo wake wote,
Then nenda kalie lie kwa huyo lea mrudiane,
Alfu utakapokuta usichokitarajia kwa lea na ukaonja manyanyaso ya kimapnz kutoka kwa mwanamke,
Siku nyingine ukibahatika kumpata binti akakupenda km ulienae sasa utakuwa na adabu ya kuheshimu na kujali hisia za wenzio na kuachana na huo upupu unaouwaza sasa.(in short unachokifanya kwa ulienae sasa kimenidhi sana)
 
Mpotezee mkuu, yeye kishaonyesha kutokuwa na mapenzi kwako, hivyo basi kwendelea kumnga'nga'nia ni kama kuchomwa na mwiba na uache kuutoa ili uwe unajikumbushia njia uliyopita ukachomwa na huo mwiba, kimbia na achana nae, she was not meant to be yours.
 
What if leah amesha move on? Utaendelea kumsubiri? Bado haujauruhusu moyo wako kupenda tena thats why utabaki kuwa stuck in the old memories of leah. Fikiria vizuri umepata bahati ya kupata msichana anayekupenda kwa dhati, tulia nae muanze maisha ya furaha na amani pamoja.
 
kweliii unamoyo wa chumaa kamandaa...to let it go doesn't mean your weak,but show how strong ur to let it goes,kwanini ungangania m2 asie kupendaaa,moyo wako ulipo sio penzi lilipo,hata ukiwaa na huyo leah juaa atakutesaa maana anajua unampendaaa,na huwezi kumuachaa hata akizini njeee>penda unapopendwaa jifunzeee kumsahau
 
Huyo uliyenaye ndiye wako wa kweli. Lea si wako na ungekuwa kuwa naye huenda angekuharibia maisha. Hakupendi na hatakama atasema anakupenda atakuwa anakudanganya. Anayekupenda hawezi kukupiga kibuti hivyo. Mheshimu huyo uliyekuwa naye na mungu atawabariki. Yupo msichana mmoja alinifanyia hivyo, toka nimuache nimebarikiwa sana kimaisha. Hivi sasa ananitamani niendelee naye huku akiwa na mumewe. Nimekataa, nimeweka msimamo siwezi kurudisha matapishi. Hayo hayajakukuta peke yako jihadhari tafadhari utaharibikiwa maisha usipokuwa na msimamo katika maisha yako ya ndoa/mapenzi.

By Midavudavu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom