Binti niliyebahatika kuzaa na kuishi nae nimejikuta simpendi tena

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
329
1,059
Habari.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32. Kuna mdada nilianza nae mahusiano mwaka 2019 na nilikuwa serious nae katika mahusiano hayo muda huo mimi nilikuwa nimetoka kumaliza chuo. Nadhani unaelewa mtu akitoka chuo anavyokuwa na matarajio lukuki.

Baada ya muda mambo yangu nilivyoona hayaendi nilivyotarajia ikabidi nifanye uamuzi wa kuachana na huyu dada na kuendelea na Maisha ya upambanaji sababu kubwa iliyofanya mimi nisitishe mahusiano ni pindi Binti yupo kwenye pick ya kunipenda na akiwa na future ma mimi na akihitaji kuolewa nami ila mimi sikuwa na mpango huo baada ya mambo yangu kuwa Ovyo.

Ilapita miaka mingi kidogo mwaka 2023 nilibahatika kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona picha zake anavutia niliomba turudishe uhusiano upya kwa mara ya pili alisita kidogo ila kwa kuwa bado ananipenda akanikubalia.

Tulianza mahusiano upya yenye furaha na future ya kuja kuona baadae hapa mimi nikiwa nimeshapata kazi na yeye akifanya biashara.

Kufupisha stori binti alikuja kupata ujauzito katika kipindi sijajiandaa ,nikamwambia alee tu.
Mungu amesaidia akajifungua mtoto wa kiume.

Ila kwa sasa upendo umeshuka sio kama zamani.

Nimejikuta namchukia.
Simpendi tena.
Sina hamu nae ya penzi.

Natamani hata nivunje nae mahusiano nibaki kulea mtoto.

Naombeni ushauri kwa mlippitia hii hali.
 
Unafeli. Binti kama amekupenda kwa dhati na umejihakikishia pasi na shaka wewe ndiye mwanaume wa ndoto zake, fanya nae maisha.

Ishu ya hisia ni mtambuka. Kuna wakati hisia hushuka lakini utu unabaki pale pale.

Yawezekana pia hisia nae zimeshuka kwa vile umeshamfubaisha na amekosa matunzo.

Trust me, ukimuacha aende halafu akija kujipata na kupendeza si ajabu utaomba kupasha kiporo na kurudisha mahusiano upya. Mwisho wa siku uje kumpa majeraha ya hisia mpenzi/mume wake wa wakati huo aje kuwaponda single mothers humu ndani.
 
Hiyo ni kawaida Sana mkuu kutokana na kubadilika Kwa mfumo wa upewaji pussy wakati wa ujauzito Ndio maana mahusiano Mengi yanaishia kwenye ujauzito na singo Maza wanazidi mjini, Mwanamke akiwa na ujauzito ni Baraka ila pia ni balaa Bora mvuta bangi so mvumilie utakuja kumuelewa.

Na nikurekebishe Wanaume hatupendi tunatamani so akishazaa akirudi kuwa pisi utaanza tena kulia Lia.
 
Back
Top Bottom