Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

William;

Naomba nijibu maswali haya 3 tafadhali;

Mosi;wenye uchaguzi wa spika ndani ya CCM kwani Mzee Sitta alipigiwa kura?alipata kura ngapi?

Pili,kama jibu hakupigiwa kura iweje basi useme alishindwa kwenye kugombea kiti hicho?

Tatu,je Mze Sitta alishindwa au HAKUTEULIWA na kamati kuu ya CCM?

- Mkuu hata huko zilipigwa kura waulize waliohusika utaambiwa.

William.
 
"...lack of matrimonial life and conjugal rights may lead to serious brain distortions, resulting into persistent of stresses and frequent hallucinations..."
 
- Well it is only six months, you can't compare with those TWO HARD YEARS! ha! ha! ha! ah! ha! by the way is that why you are the way you are cause of those TWO YEARS? Ha! ha! ha!


William.
 
- Well it is only six months, you can't compare with those TWO HARD YEARS! ha! ha! ha! ah! ha! by the way is that why you are the way you are cause of those TWO YEARS? Ha! ha! ha!


William.


Mkuu bora ufiche jina uje na jina ambalo ni anonymous. Kiingereza gani hicho?
Ndo mana unaambiwa usichangia humu kwa ma great thinkers.
Unaidhalilisha familia ya Mzee Malechela. No wonder umesomeshwa kwa kodi yangu.
 
Ili tuendelee tunahitaji mambo manne; watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora. Maneno hayo tuliyaimba sana miaka ya themanini tuliokuwa shule ya msingi enzi hizo. CCM wanajua wazi kuwa kinachokosekana kwa nchi hii ni siasa safi na uongozi bora. CCM wanaendesha siasa chafu na uongozi mbovu. Hilo wanalijua.

Kwa wale wanaofatoa ushauri nasaha huwa wanajua kuwa watu wengi wanapokutwa na virusi vya ukimwi, reaction ya kwanza huwa ni KUKATAA (denial).

CCM wako hivyo hivyo. Toka mwaka 1995 anticorruption drive ndo ilikuwa agenda kubwa ya chaguzi zote. Wote tunakumbuka Mkapa alivyoingia madarakani na tume ya walioba na jinsi alivyoshindwa misserably kutekeleza yale yaliyokuwemo kwenye report ya tume ile. Strategy ya mkapa miaka mitano ya mwisho ya utawala wake (baada ya kifo cha mwalimu) ilikuwa ni kuukataa ufisadi (corruption). Tunajua baada ya kuukataa ufisadi nini kilichofuatia - yeye mwenyewe kujizamisha katika ufisadi.

Serikali ya kikwete iliingia kwa gia ile ile ya anti-corruption. Baada ya kushindwa anti-corruption drive kutokana na yeye mwenyewe kuhusishwa (makashfa yote makubwa yanaashiria kushiriki kwa Kikwete mwenyewe). Kikwete aliwahi kutoa kauli nyingi mno za kutia kinyaa. Kwa mfano aliwahi kusema kuwa wauza-unga anawafahamu ila anawapa muda kujirekebisha (Wakati Mhe. Amina Chifupa - RIP alipolibebea bango suala la unga). Wakati bandari ilipokuwa katika kilele cha utendaji mbovu na wizi wa mizigo, Kikwete alienda bandarini na kusema wezi wa mizigo serikali inawajua ile inajiandaa kuwachukulia hatua.

Wakati EPA ilipofika kilele chake Kikwete vile vile alisema wahusika wote wanawajua na wanarudisha pesa. Wote tunajua hazikurudi zote na wote tunajua waliopelekwa mahakamani ni wachache tu, wengi wapo mtaani na wanatesa na mipesa ile ile. Wakati wa kashfa ya richmond tunajua mwanzoni rais alivyoonekana kulivalia njuga, lakini baadaye akapoteza STEAM baada ya kuwa vinara wakubwa walikuwa ni members wa inner circle.

Kwenye kampeni zake za mwaka huu Kikwete hajazungumzia kabisa corruption, kwa maana Kikwete naye kaingia kule kule kwa mkapa yaani kwenye DENIAL. hiyo ndo strategy ya mpya ya Kikwete, kukataa kuwa corruption ipo na kuwa ni tatizo.

Hilo ndilo analoliakisi Mama Speaker Mpya. Denial kuwa corruption ipo na ni tatizo linalotakiwa kushughulikiwa. Corruption imeigharimu CCM majimbo mengi sana ya uchaguzi (Kina makamba wameshasema matatizo ya kura za maoni ndiyo yaliyosababisha CCM kushindwa majimbo waliyoshindwa). Lakini Strategy yao inarudi kuwa ile ile ya kukataa kuwa corruption ipo.

Neno Ufisadi lilichaguliwa kuwa neno linalofaa kuchukua maana ya neno CORRUPTION. Uchaguzi huo ulifanywa na waswahili wenzetu wa Kenya. Watanzania tumeona ni kweli Mbadala wa neno corruption si neno rushwa. Neno corruption ni pana zaidi ya neno rushwa linalozungumzia hongo tu au mlungula. Neno corruption ni pana zaidi na linabeba uzito zaidi.

Watu wote wameshalipokea neno UFISADI, kama mbadala wa neno la kiingireza CORRUPTION. Speaker mpya anapotumia press conference yake ya kwanza kukataa tafsiri ya neno ufisadi inayokubalika na watanzania wote anajichanganya yeye mwenyewe. Ni kweli ana-akisi mpango mkakati wa CCM wa kukataa kuwa corruption ni tatizo. Waandishi wa kamusi hawajaingia tu mitamboni, lakini version mpya ya kamusi itakuwa na maana hii mpya ya ufisadi. Ni kujidanganya kwa CCM na watendaji wake kuwa kuendelea kuukataa UFISADI ndo suluhisho.

Ufisadi upo, tunauona kila siku, unatuumiza na unaendelea kulitafuna taifa. Hata kama CCM wananufaika na ufisadi huo na kuona kuwa kusema ufisadi haupo ndo njia sahihi, wajue kuwa mbinu hii haitawasaidia. Hata wizi wa kura ni sehemu ya UFISADI ULIOKUBUHU. CCM kama wanaamini wataendelea kutegemea ufisadi kuwepo madarakani waangalie SOMALIA.
 
Mkuu William huhitaji kujenga fikra kwa mtindo wa vipande vipande. Hapa hajadiliwi Anne Makinda wa 2010 tu, sisi wengine tunamfahamu tangu akianza ubunge 1975 (Sijui ulikuwa wapi?). Tabia mbaya za Makinda si suala la kusubiri, wanaomfahamu wanamfahamu, bahati mbaya wengine mnaanza kumwona Makinda kwenye uspika na ndiyo maana mnasema tumwache afanye kazi ndo tumhukumu. Hivi William hujui hata kuwa Makinda alikuwa naibu spika? Au unadhani mtu akishakuwa spika anakuwa mwingine tofauti na alivyokuwa naibu? Fungua macho mkuu.

Ni sawa na mtu anayesema tusubiri tuone utendaji wa Kikwete wakati tumeona utendaje wake for the last 5 years
 
Pasco, kweli una maana kuwa huyu mama pamoja na kujua maana ya neno Fisadi kikamusi, hajui maana ya neno hilo hilo katika muktadha wa siasa za TZ? Kama kweli hajui maana ya neno fisadi kama tulijuavyo wengi weti katika muktahda wa siasa za TZ, Basi nina shaka na uwezo wake wa kupembua issues. Anyway tumpe nafasi "Ulimi hauna mfupa"; lakini alipaswa kufikiri kwanza na kuchuja mambo kabla ya kusema. syo ku halalish amakosa kwa kwa kutumia dictionary.
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.

Pasco hapo umeniacha hoi.
Kwa hiyo Makinda angeulizwa maana ya kuchakachua angejibu ni staili ya muziki wa dansi? Give me a break, misamiati hukua na FISADI maana yake hata vidudu wa hii nchi wanajua.
 
Mkuu bora ufiche jina uje na jina ambalo ni anonymous. Kiingereza gani hicho?
Ndo mana unaambiwa usichangia humu kwa ma great thinkers.
Unaidhalilisha familia ya Mzee Malechela. No wonder umesomeshwa kwa kodi yangu.

- Naona ujumbe umekufikia tayari, kwamba miaka miwili sio sawa na miezi sita, hata wewe unaweza kuingia kwa jina lako maana naona unateseka sana, otherwise jaribu kubadili maneno maana kwa kawaida una maneno matatu tu, jina langu/familia, elimu, na umaarufu ndio maan inakua rahisi sana kukujua, pole sana!

- Otherwise tafsiri ya ufisadi kama Mama Makinda alivyoisema, ambayo haikubaliani na wengi humu na kugeuzwa kuwa ndio kipimo cha uwezo wake kiuongozi wa taifa ni very serious ishu!

William.
 
Kumbukeni huyu kawekwa na mafisadi ili aje kuwasafisha na ndio keshaanza kazi hivyo!!tushike vichwa na mioyo yetu wakati tunasubiri kifuatacho.
 
Pasco, kweli una maana kuwa huyu mama pamoja na kujua maana ya neno Fisadi kikamusi, hajui maana ya neno hilo hilo katika muktadha wa siasa za TZ? Kama kweli hajui maana ya neno fisadi kama tulijuavyo wengi weti katika muktahda wa siasa za TZ, Basi nina shaka na uwezo wake wa kupembua issues. Anyway tumpe nafasi "Ulimi hauna mfupa"; lakini alipaswa kufikiri kwanza na kuchuja mambo kabla ya kusema. syo ku halalish amakosa kwa kwa kutumia dictionary.

- Mhhhhh! maneno mazito sana mkuuu!


William.
 
UFISADI NI WIZI WA WAKE ZA WATU.....
TULAMBUE KISWAHILI
MWANANKE- MZALISHAJI TWAWEZA KUSEMA NI RASLIMALI, KWA KUWA NDIO INAKUZA UCHUMI(mali)
ZA WATU - INAMAANISHA WAMILIKI, WENYE MAMLAKA NA KITU(WATANZANIA)
KUIBA MKE - UNAWEZA UKAZINI NAE HALAFU IKAISHA NAU UKAMUOA KABISA
KWA HIVYO MFIKISHIENI MAZA MAKINDA- UFISADI - NI MWIZI WA RASLIMALI ZA WATU AU MALI ZA WATU KWA KUZITUMIA VISIVYO AU KUZICHUKUA KAMA ZAO KABISA

MFANO: LOWASA ALIVYOTUMIA MALI ZETU - WA DEAL LA RICHMOND(alizini na Mke wa mtu)
au mkapa alivyo chukua Kiwira- alioa mke wa watu
KIKWETE alivyoiba kura zetu- aliiba mke wa watu--- haki ya watanzania kujichagulia kiongozi wanaomtaka.....


asipoelewa mwambieni ani PM:A S angry:
 
@ kiwi umeongea ukweli kabisa...haitaji kupewa nafasi haonekane utendaji wake...alishapewa, alishakluwa kiongozi wa juu miaka nenda rudi... Hana jipya zaidi ya kuendeleza ufisadi bungeni....nimefurahishwa sana na majibu ya jokakuu kwa william,

nafikiri wiliam aishi tanzania au kama anaishi basi ameziba masikio na macho yake kutambua mambo muhimu,

anyway... Sio tusubiri.. Bali tuendelee kuumia mpaka hapo muda utakaposema.. Wazungu wanasema time will tell.. Ndio ataelewa vema maana ya fisadi na jinsi gani hauangamize ufisadi......

Kifupi mama anachemka sana, mara nyingi sio mara moja...fatilia kazi zake nyuma utaelewa
















mungu ilinde tanzania
 
Pasco,

..Mama Makinda ameulizwa kuhusu mafisadi kulingana na tafsiri ya neno hilo ktk siasa za leo za Tanzania.

..hivi ina maana akiulizwa kuhusu "vigogo" atasema ni vipande vya miti?

..hilo lilikuwa swali la mtego na kutokana na majibu yake amekwepa mtego mmoja na kutumbukia kwenye mtego mwingine.

..huyu ndiye anayedai kwamba amekuwa mbunge "maisha yake yote" halafu anashindwa kujibu maswali mapesi kama aliyoulizwa.

..so far naona kitakachomharibia Mama Makinda ni hii tabia ya kujibu maswali kwa jazba.

NB:

..Mama Makinda hakuwa kwenye timu ya kampeni ya uraisi ya Edward Lowassa mwaka 1995??


- Kwani mkuu Dr. Slaa hakuwahi kuwa member wa CCM? Si alitoka baada ya CCM kufanya makosa ya kumpitisha mtu mwingine zaidi yake, au? Halafu Richmond haikuwepo 1995!


William.
 
Sahihisho;

Kwa chaguzi za hivi karibuni Mama Makinda amekuwa anapita bila kupingwa;Mkoa wa Iringa ndiyo CCM inaongoza kwa kupita bila kupingwa na nyuma ya pazia kuna 'harufu' ya kale kamchezo;wanatumia hila kuogopa kupambana na Upinzani jukwaani na aliyoyafanya Mzee Kapwani wa CHADEMA kule kwenye jimbo la Isimani kwa Lukuvi kwa kutorudisha fomu ndiyo anachokifanya kila uchaguzi ukikaribia Dr Ngunangwa kwenye jimbo la Mama Makinda;sio tu yeye huwa harudishi fomu bali akarubuniwa na akaamua kabisa kurudi CCM huku akihaidiwa kulipwa marupurupu yake yote aliyopunjwa alipokuwa Mbunge mwaka 1995-2000!

Kweli siasa za TZ ni ngumu mno!

Jumlisha na kale ka mchezo ka jimbo la Ludewa ka kuchukuliwa kwa form ya ubunge kupitia CHADEMA na mtu asiye julikana. Na hatimaye kutorudishwa mpaka baada ya muda uliopangwa kupita. Hii ndio Iringa msiyoijua!!!
 
Lini na wapi alisema hivyo?

Ah! huyu mama kaja kwa moto wa kifisadi na hadi sasa kwa kumsikia mwenyewe ameshasema maneno ya kutia kichefu chefu kibao hana hata aibu. Yaani anakuja kichwa kichwa sana.

Kwa kifupi hayo kashatamka pamoja na mengineyo yanayoashiria kuwalinda mafisadi
 
Utu wake umenunuliwa na pesa za mafisadi.
Mwache aibu zimkumbe
Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.

Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Hizi ni siasa za maki taka. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kweli kama atafanya kazi yake vizuri? La hasha! Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.

Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake! Sikuwa na imani na utendaji wa ccm tangu mwanzo, lakini hii imeniongezea kutokuwa na imani na Anna Makinda kama Speaker anayefaa.
 
Back
Top Bottom