Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Kama ufisadi ni kuiba wake za watu basi hata kuiba waume za watu ni ufisadi, na huyu ASM naye ni fisadi kwani alikuwa na affair na muungwana na wakati huo tayari muungwana ana mke wa ndoa.Na mpaka sasa huyu mama ni msela ina maana anaendelea kufisadi waume wa wenzake.
 
Huyu Speaker Mpya hana jipya bali anaturudisha nyuma badala ya kusonga mbele kama taifa, kiswahili kinakuwa kila siku. Kumbe akiulizwa maana ya neno "kuchakachua" atatafsiri kizamani kuwa ni kuchanganya ulanzi uliolala kuchachusha ulanzi mpya ili iwe pombe! Huu ni upuuzi unaofaa kupuuzwa na tusitegemee wabunge wa upinzani kupata ushirikiano toka kwake. Ameanza vibaya na lazima ata,aliza vibaya na atakisambaratisha chama chake kabla ya 2015. Kwa staili hii ni sawa na kuwasafisha mafisadi toka kwenye matope yao.

Makamba alishasema CCM siyo fisadi ila baadhi ya wanachama wake ni mafisadi sas je ina maana wanachama wa CCM wanaiba wake za watu?

Kamusi ni kitu static....lugha inabadilika kila siku kwani neno CHANGUDOA limo katika hiyo kamusi?...leo tukimwita yeye Anna Makinda CHANGUDOA si ataenda mahakamani?...je tuje na hiyo hiyo kamusi mahakamni kujitetea?....ukweli ni kuwa maana halisi ya FISADI inaeleweka na yeye anaijua sasa atuambie tuwaite nini hao MAFISADI kama hawataki hili neno achague haraka sana kabla hatujachukia
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.


Kweli utapeli wa kisiasa umetuzidi waTZ!!! Sasa hapo atataka kutuambia nini???
 
Kama ufisadi ni kuiba wake za watu basi hata kuiba waume za watu ni ufisadi, na huyu ASM naye ni fisadi kwani alikuwa na affair na muungwana na wakati huo tayari muungwana ana mke wa ndoa.Na mpaka sasa huyu mama ni msela ina maana anaendelea kufisadi waume wa wenzake.

Ina maana huyu mnyalu ni NUNGA YEMBE?
 
Miaka 5 mtasikia taarabu zikilindima ndani ya Bunge. Maana huyu mwananke ana maneno ya kejeli (taarabu) hadi anamkejeli bosi wake (Mpiganaji 6).

Naona hajui alitendalo na kama bado anaingia kwenye siku zake basi itakuwa mara 2 kwa mwezi
 
Kamusi gani hiyo inayotoa maana ya neno fisadi kuwa ni wezi wa wake za watu (ingawa dhana nzima naikataa)? Na wezi wa waume za watu nao wanaitwaje sasa?

according to TUKI swahili-english dictionary


fisadi nm ma- [a-/wa-] 1 seducer, reprobate, lecher. 2 intrigue. kv quarrelling, dissolute, evil, lewd, profligate.
 
Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.

Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Hizi ni siasa za maki taka. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kweli kama atafanya kazi yake vizuri? La hasha! Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.

Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake! Sikuwa na imani na utendaji wa ccm tangu mwanzo, lakini hii imeniongezea kutokuwa na imani na Anna Makinda kama Speaker anayefaa.

SIDHANI KAMA ALIKOSEA, KWANI NDIO ILIVYO KWENYE KAMUSI, HILI HUKUSIKIA AU KULIONA
"Kuwa spika ni ratiba ya maisha yangu, ni kitu ambacho nilikuwa nakifikiria na mimi ni mtu wa kufuata taratibu. Kwanza sijui kama kuna mafisadi kwa kuwa fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu," alisema Makinda.

Kuhusu uendeshaji wake wa bunge alisema kuwa hatakubaliana na hoja za kukomoana bali atahitaji hoja zilizofanyiwa utafiti ili maamuzi yanapotolewa yaweze kuleta tija.

Alisema siasa si za kuzua maneno tu lazima hoja ziwe za kitafiti na ni lazima wabunge wawe na uwezo wa kuibua mambo ili kazi iwe nzito.

"Nasikitika kuwa bunge lililopita lilikuwa na hoja nzito moja tu ya Richmond, zilitakiwa ziwe zaidi ya kumi kama hizo ili bunge liwe na nguvu zaidi,"alisema Spika huyo ambaye katika bunge lililopita alikuwa Naibu Spika akimsaidia Sitta.

Makinda alisema katika bunge hili atatoa kipaumbele kwa huduma za wabunge na wafanyakazi wa bunge kuwa bora zaidi na kutoa elimu kwa wabunge iliwaweze kuzielewa kanuni vizuri
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.

1. Kwa hiyo mtu akitembea/akiiba mke wa mtu kwa tafasiri ya spika wetu ndiye fisadi - du!!! this is very kali, jamani hivi huyu ni spika au mama mshereheshaji wa kitchen party ya uswahilini. Kwa hiyo walituibia fedha zetu za EPA, Richmond, Maremeta nk ni wasafi kwa tafasiri ya spika ili mradi hawajaiba wake za watu.
2. Yaani unadhani kama katumwa na mafisadi akubali kuwa wamemtuma? - this defies logic and common sense
3. Kama hao mafisadi hawajui atasemaje hawajamtuma?

Jamani naomba awepo mtu wa kuwa anamkumbusha mara kwa mara kuwa kwa sasa yeye ndiye spika wa bunge na bunge ni moja kati ya mihili ya dola. Nadhani anajisahau (labda sababu ya ugeni) kuwa yeye ni spika wa bunge - chombo chenye heshima kubwa ktk jamii.
 
Huyo mama atachemsha sana msishangae, hivi alishawahi kuwa na mume? hajawahi iba mume wa mtu? tuna records zake
Mwambieni asimchafue slaa :hippie:
 
Huyu Anna Makinda mwenyewe hana mume, tujiulize kiu anakatia wapi kama si kwa waume za watu?? Namfaham mtoto wake mmoja wa kike tulikuwa naye hapa Ndzengelendete baadaye akaenda UK kusoma, alizaa na mume wa mtu. Kwa tafsiri yake inaonyesha naye ni fisadi. Kwanza ktk maadili ya kiafrika kumpa uspika mwanamke asiye na mume NHUNGAYEMBE ni kosa kubwa.

Ni kweli Mama Makinda HANA MME kwa hiyo yeye ni mwizi wa waume za watu!

Hivi jamani hakuna kipengele kinachombana Spika kuwa LAZIMA AWE MME ALIYEOA AU MKE ALIYEOLEWA? Maana kwenye upande wa mhimili wa Serikali yaani Urais lazima awe na MKE AMBAYE ANAKUWA FIRST LADY au sijui FIRST MAN kama itatokea tukawa na Rais mwanamke.
 
hii ilikuwa ni 7th july 2008

makinda ashangaa mafisadi kusafishwa

na godfrey god, iringa
tanzania daima~sauti ya watu

naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, anna makinda amewakoromea baadhi ya wabunge na watu wanaofanya kazi ya kuwasafisha mafisadi kuacha mara moja kwa madai kuwa hawawatendei haki watanzania wenzao.

Makinda ambaye pia ni mbunge wa njombe kusini, alitoa kauli hiyo nzito jana wakati akiwasalimia wapiga kura wake katika kata ya njombe mjini kwenye mkesha wa mwenge wa uhuru.

Ametoa kauli hiyo kipindi ambacho bunge limegawanyika makundi mawili, moja likiwatetea mafisadi, lingine likiwapinga huku likiishinikiza serikali kuchukua hatua.
sasa hivi kanyweshwa maji ya ufisadi hata hajui ufisadi ninini? Huyu mama ni hatari kuliko hata mafisadi kwani mpango wake mkubwa ni kuhakikisha anasimia maslahi ya hawa mafisadi na kuwasafisha baadhi yao ili waweze kushika nchi kipindi kijacho. Amewekwa pale na mafisadi papa na nilazima atimize matakwa yao kwa kukandamiza sauti yaumma na kuficha uovu wa hao mafisadi.. Eh mungu nusuru hili bunge katika mikono ya huyu mama
 
Siamini kuwa huyu Anna Semamba Makinda aliyechaguliwa na Wabunge wa CCM kwa kishindo baada ya kuteuliwa na CCM(CHAMA CHA MAFISADI) ameanza kuchemsha hata kabla ya Bunge kuanza rasmi.

Anne Makinda ameanza kuropoka na kuongea hovyo kana kwamba bado ni Mbunge wa kawaida. Inasikitisha sana. Kuna kauli mbili zenye utata ambazo tayari ameshazitoa katika siku hizi mbili. Hebu tizijadili:

  1. Kwamba FISADI ni yule anayeiba WAKE ZA WATU. Siamini masikio yangu kama kweli huyu mama ameongea kwa dhamiri toka moyoni au ilikuwa ni joke! Kama ni joke basi HATATUFAA kwenye nafasi hii ya Spika kwasababu huwezi kuanza kuleta utani kwenye maswala ambayo ni very sensitive kama hili la UFISADI. Hii tayari inaanza kutupa picha na uhalisia wa Spika tuliyenaye. Kama ameshaanza kupindisha maana halisi ya UFISADI ndipo tuanze kujua kuwa huyu mama kweli amewekwa na MAFISADI na tayari ameshaanza kazi ya kuwasafisha mafisadi.
  2. Kwamba katika kuzungumzia UHUSIANO wake na Spika Samwel Sitta kuwa ni kaka yake na anamheshimu na kama kuna mazuri au mabaya yaliyofanyika kwenye uongozi wa Spika Sitta na yeye anahusika. Sawa. Kauli iliyonipa utata mimi ni hiii ya kusema kuwa anamuheshimu Spika Sitta na kama Jina la Sitta lingelikuwemo kwenye orodha ya walioomba kugombea Uspika yeye angetoa jina lake!!!Uongo mkubwa. Kila mtu anajua kuwa Sita alishatangaza mapema kuwa ataendelea kuwania kiti chake cha Usipika na mdiyo maana hata mzee wa Vijisenti Chenge alianza kumrushia makombora Sitta kuwa hafai. Katika majina 13 yaliyopelekwa CC jina la Sitta lilikuwemo,Je mbona hatukumsikia Anne akijitoa kumwachia kaka yake Sitta anayemweheshimu. Na kama Chenge alitupa lawama kwa Spika Sitta kuwa aliliongoza Bunge vibaya basi nayeye Makinda ANAHUSIKA MAANA ALIKUWA NAIBU WAKE kwa hiyo na yeye angewajibika kwa kutoa jina lake lakini haikuwa hivo. Kwa hiyo huyu mama ni mwongo,mzushi na kigeugeu na hii inathibitisha tu kuwa ni kweli akatae au akubali ukweli ni kwamba yeye ametumwa na hao MAFISADI kuwa angombee hiyo nafasi ili kumtibulia na hatima yake kumnng'oa Spika Sita ili MAFISADI wapate nafasi ya kufanya mipango yao ya UFISADI na kuandaa Rais wao atakayekuja 2015.
Kwa hiyo BELIEVE ME,ANNA MAKINDA HATAKUWA SPIKA MZURI WA HILI BUNGE LA 10. YEYE ATAKUWA NI MWANAMKE WA KWANZA KUWA SPIKA NA SPIKA ALIYE MBOVU KABISA KULIKO MASIPIKA WOTE WALIOWAHI KUONGOZA BUNGE LA TANZANIA TOKEA WAKOLONI MPAKA SASA.

Wakti mwingine inabidi watu turudi kwenye vitabu vitakatifu kabla hatujachukua maamuzi. Kweli watu wanazungumzia GENDER ISSUES,GENDER EQUALITY,etc. Usawa na upuuzi mwingine kama huo. Lakini hebu tuwe wa kweli wa kusema;call a spade a spade and not a big spoon. Biblia inasema SIMPI RUHUSA YA MWANAMKE KUMTAWALA MWANAMME.Yes,I like this. Utasema oh,mfumo dume,oh unyanyasaji wa kijinsia etc,etc.Lakini ukweli utasimama. Mwanamke hapashwi kuongoza wanaume,NEVER! Hiyo ni Biblia,Huyo ni Mungu. Anayepingana na hilo ataona matokeo yake. CCM kimetufikisha hapo kwa kisingizio cha kijinga kabisa! Kwamba ati tangu tupate uhuru nchi yetu haijawahi kuweka mwanamke kwenye mojawapo ya mihimili 3 ya nchi! Ebo,yaani all thise years mlikuwa wapi,mmekuja kuzinduka kwenye kiti cha Usipika 2010 kuwa ndiyo awe mwanamke. Basi na Waziri Mkuu 2010 awe mwanamke na Rais wa 2015 wekeni mwanamke halafu mtaona muziki wa kinamama kuendesha nchi!! Hivi kwanini mnafikiri Mungu amekataza wanawake wasiwatawale wanaume? Kwanini wanawake hawaruhusiwi kuwa Wachungaji au Mapadre?Je, kuna mwanamke anaweza kumuweka mwanamme mimba?? Show me one. Watu wanatafsri vibaya kuhusu hii lugha ya usawa. Ni katika maeneo fulani fulani tu siyo kuwa mwanamke anaweza kufanya kila jambo. Kuna mambo wanawake hawayawezi na hawatakaa wayaweze hata siku moja!Maumbile yao proves what they are. Biblia ina sema kuwa KAENI NA WANAWAKE KWA AKILI MAANA NI VIUMBE DHAIFU.That is the Bible. Kiumbe dhaifu unakipa kuongoza mhimili wa nchi kama Bunge,what do you expect?Sitaki kuingia sana into details kuhusu hayo lakini is a big discussion forum.

Mbona JK hakuanzaia kwake kwa kujitoa kwenye kugombea Urais akawaachia mwanamke ili awe Rais wa kwanza mwanamke? Kwanini Mwanamke aanzie kwenye Bunge kama siyo ilikuwa janja ya kumwengua Sitta.
Matokeo yake hayako mbali sana mtaanza kuyaona muda si mrefu.

CCM msifikiri Watanzania tunadanganyika kwa upuuzi wenu huu mnaowafanyia. Anne Semamba Makinda tuna uhakika AMEWEKWA KWA AJILI YA MASLAHI YA MAFISADI n akuna gazeti leo limeandika kuwa MAFISADI WAMEKUNYWA POMBE KUSHANGILIA KUONG'OLEWA KWA SPIKA SITTA.

Iko siku CCM mtakuja kulipia uhuni mnatufanyia Watanzania.

Wasaalamu.
 
mhh naogopa ku comment maana huyu mama analindwa kweli kwlei hapa JF..Muulize Kigogo kafanywa nini kwa kum comment huyu mama...yangu macho
 
MBONA ANAJUA ANALOLIFANYA HUYU AMETUMWA NA MAFISDI PAPA NDIO MAANA LEO ANASEMA HIVI KESHO HIVI KUTOKANA NA INAVYO MPENDEZA YEYE NA HAO WALIOMTUMA!



A bird doesn't sing because it has an answer, it sings because it has a song.
 
Back
Top Bottom