Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Tunawakati mgumu sana kuona hata chombo kinachotunga sheria kinapindisha sheria kwa maslahi ya wachache...hii ni hatari sana. Pia ni ukweli usiopingika kwamba huyu spika yupo kwa maslahi ya chama chake. Sidhani hata kama anakumbuka kiapo chake cha kuongoza bunge.
 
Yeye anatimiza matakwa ya waliomuweka, ambao ni EL na RA. Kwa kuanzia kamuweka EL katika kamati nyeti then kamtupia mtoto wa Kibaraka Makamba kubalance issues za umeme ili waendelee kula nchi. Huyu Makinda ni Kinda kweli na hatari sana kwa maendeleo ya nchi hii
 
Huyu mama si tulishasema katumwa! Huyu yupo kusikiliza RA na EL wanasema nini. Historia itamhukumu tu. Leo Mubarak ni historia itakuwa Anna.
 
Ndugu wana jamvi hivi kwa mtazamo wa undeshaji wa Bunge la sasa mbona naona kama Spika wetu huyu ana mfumo wa udictator??? Wenye information na utendaji wake wa huko nyuma atujuze.
 
MAMA SPIKA ANNA MAKINDA, BUNGENI KUHESHIMIWE TU 'NGUVU YA HOJA'
KWA WASHIRIKI WOTE; UMRI, VYEO NA USOMI TUKASUBIRIANE MITAANI

Bungeni ndiko pekee mahala ambapo hata nyau tu huthubutu kumtazama moja kwa moja mfalme usoni huku mchezo ukichezwa kwa maneno mdomoni, akili kichwani na maspika wakiwa ni refasrii na washika bendera.

Nasema bungeni ndiko mahala ambapo mchezaji wa kulipwa au kepteni kwenye timu asipokaa vizuri hulambwa chenga mara kibao na wachezaji chipukizi; wengine ambao hata majina bado hawa. Ndio!! Bunge ndio uwanja wa siasa penye mazungumzo ya kistaarabu tu (vijembe, kejeli, na mizengwe mahala pake sokoni) huku kukiw ni kwamba kinachotafutwa kwa kiasi kikubwa ni kushawishiana mwelekeo wa mambo, kuridhishana UKWELI ULIPO, na kutatwa matatizo ya jamii iliowatumeni mahala pale.

Hivyo, hali iliojitokeza kati ya viongozi wetu Waziri Mkuu na Mbunge wa Sumbawanga na mwenzake Mbunge wa Arusha, Gdbless Lema, majuzi bungeni Dodoma, lina mengi mazuri ya kutufundisha kadri bunge letu linavyoendelea kuseheni viongozi vijana na wasomi, kuliko kuishia tu kwenye kutuhumiana UTOVU WA LABDA NIDHAMU na hata wengine kuonekana kule kwamba kila kitiririkacho toka vinywani mwao siku zote kibakia na kuendelea kuwa ni UKWELI NA UKWELI MTUPU!!!

Tusisahau pia kwamba siku zote watu tumezingirwa na minada ya kila aina katika maisha tunayoishi. Wakati mnada wa wafanyabiashara wa mitumba ni Mchikichini kwa Makamba Dar, mnada wa nyama ni Vigunguti, Simu za Wizi pale makutano ya barabara za Independence na Makungnya, ya wambeya vijiweni, na mnada wa silaha haramu toka Rwanda ni pale Kijitonyama Breakpoint, kwao wao wanasiasa mnada wao wa kuuza na au kutetea mawazo chini ya misingi inayoeleweka ni bungeni.

Mpaka hapo kwaza nitangulize po ngezi zangu kwa wabunge wa CHADEMA kwa namna ya pekee wanavyochangia kuweka VIWANGO VYA KIMATAIFA KATIKA UENDESHWAJI WA BUNGE LA VYAMA VINGI ambyo kwa bahati mbaya hayakuzoeleka katika nchi yetu ambayo imekwepo chini ya mfumo wa chama kimoja. Pia, kwa namna ya pekee nimpongeze Mhe Godbless Lema kwa utetezi w nguvu anaouleta bungeni dhidi ya madai ya Waziri Mkuu. Wadadisi wa mambo wanahofia kwamba endapo kutabainika kwamba Mhe Pinda alitoa majibu rahisi kwa maswali magumu basi ofisi ya spika itamchukulia hatua gani?? Jamani wabunge wa CHADEMA mko deepu saaana!! Duu, kwa mtaji wa utetezi huo sasa hapa ni patamu mnoooooooo!! Na sasa tunasubiri kweli kweli mwenendo mzima baada ya hapa tuone inavyokwenda.

Kweli sasa bunge letu si kama enzi zao Marehemu Amran Mayagila,Komanya, Joseph Rwegasira au Fredrick Msuya ambako mbunge kazi yake ilikua ni kuingia pale mjengoni na kuanza kuchapa usingizi waka mjadala ukiendelea huku akitajwa tu jina na spika wa wakati huo, Marehemu Chifu Adam Safi kumuuliza maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, mara utasikia mtu mzima kaibuka ndotoni na udenda ukichuruzika, na kusilibia tu jibu lolote lile kama vile 'MHESHIMIWA SPIKA NAUNGA MKONO HOJA ASILIMIA KWA MIA KAMA ILIVYOSEMWA NA MVUNGUMZAJI ALIYETANGULIA'.

Sasa hivi kweli karibu kila mbuge, hasa wale wa upinzani ni watu ambao ni wadadisi wakubwa na wa kudadavua kweli kila nukta n kituo azungumzapo mtu bungeni na hada huku majukwaani mitaani. Ni watu ambao ni wafuatiliaji wakubwa wa mambo, WENYE NIDHAMU KUBWA KWA 'NGUVU YA HOJA' ILA WATOVU WAKUBWA WA NIDHAMU KWA 'HOJA ZA NGUVU'; hata kama hoja za aina hiyo zinashilishwa mbunge mwenye umri mkubwa kuliko Mrehemu mpendwawetu Mzee Abdalla Fundikira, mwenye usomi zaidi ya Maprofesa Sarungi, Mwakyusa au Mwandosya, au mwenye cheo kikubwa cnini kama Mhe Rostam Aziz - kinachoheshimiwa ni nguvu ya hoja tu!!

Je mnaonaje bungeni tukazingatia zaidi heshima, adabu na unyenyeke mkubwa kwa NGUVU ZA HOJA PEKE YAKE (kwa maslahi ya wale waliotutuma bungeni kuwatetea) kama wajumbe rasmi bungeni, halafu baadaye sana tu kukaanza kuzingatia heshima, adabu na unyenyekevu mkubwa kwa umri wa mtu, elimu yake au cheo pindi tukishatoka nje ya bunge??

Hili ni muhimu sana na lazima liwe hivyo mheshimiwa spika kwa sabu ilikuondoa hatari ya waheshimiwa wabunge kubaguana kiumri, kiusomi, na au ki-vyeo kule mjengoni, ni bora tutambue ya kwamba wangiapo ndani ya bunge la ni kazi moja tu - UWAKILISHI WA WATU WAKE WITHOUT FEAR OF FAVOUR - hivyo dira yake kuu ya kutolea heshima, adabu na unyenyekevu ni NGUVU YA HOJA TUU, ili ubunge wake kama li-taasisi linalotegemewa na wengi sana nje ya bunge liweze kufanya kazi bila vikwazo vingi. Hapo ndipo taasisi za Uwaziri Mkuu na Ubunge wa Jimbo la Arusha au nyingine yoyote itaweza kufanya kazi kwa umurua wake stahiki.

Lakini pindi Ndugu Godbless Lema au Mr Sugu, Halima Mdee au David Kafulila anapokutana Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda aka 'Mtoto wa Mkulima' mwenzangu na mimi hapa basi hapo yale yoote heshima, adabu na unyenyekevu ZIWE MBEEELE KAMA TAI kama ilivyo ada katika jamii yetu ya ki-Tanzania, wazee kutambulika kwa kuwa wametuzaa, kisomo huingatiwa kwakuwa hutuwezesha vizuri zaidi kumudu mazingira yetu tunamoishi na vyeo vithaminiwe hasa wenye dhamana hizo wanapovitumia vizuri zaidi na kwa haki kwetu sote.

Mwisho, heshima, adabu na unyenyekevu zote kwa pamoja ni tamu sana ilioje kwa wanaozipata kila leo na hasa pale ambapo zote hupatikana kwa hiari zaidi!!!
 
Sidhani kama ni dikteta...nina shaka sana na confidence yake katika kuliendesha bunge. Inawezekana amevaa kiatu kikubwa kuliko mguu wake. Unajua tena kama unafanya kazi usio na elimu wala ujuzi nayo...dawa pekee ya kuwezesha mambo kwenda ni kukunja uso ili watu wajue unatisha ingawa ukweli wa mambo ni kuwa unaogopa watu wakisogea karibu na kuanza kudodosa mambo ya kikazi watagundua weakness yako!
 
Hali ilivyo serikali na chama cha Mapinduzi wameamua kukaba hata penati.
Wengi tulijiuliza vigezo vya kumweka Makinda Samamba pale bungeni badala ya gwiji la sheria kama Samweli sitta, Kumbe lengo walimweka beki wa ccm na serikali yake ili aweze kukaba hata penati.
 
mambo bado ninataka bunge letu liwe kama la kenya face by face na itakuwa ivo endapo cmd watakuwa tayari kwa ajr ya masirai ya umma mana ccm vilaza wote wapumb............. shame on them chichiemu
 
Nakubaliana na Ndahani. Huyu mama kapachikwa pale na mafisadi ili wadhibiti uendeshaji wa bunge. Hajui kanuni za bunge na not too long in the near future atajiumbua mwenyewe.
 
Ni yote ktk yote;
Udictator- kudhani ataendesha bunge kama kamati au idara ya chama cha mafisadi.
Umbumbumbu - Kutokujua kanunu na taratibu za bunge.
Ulimbukeni - kudhani kwamba mtangulizi wake hakufanya kazi nzuri kwa yeye tu ndo ataliweza bunge.
Ushamba - kufanya kazi ili awafurahihse waliomweka hapo.
Na kadhalika - kutetea na kulinda mafisadi.
 
Sidhani kama ni dikteta...nina shaka sana na confidence yake katika kuliendesha bunge. Inawezekana amevaa kiatu kikubwa kuliko mguu wake. Unajua tena kama unafanya kazi usio na elimu wala ujuzi nayo...dawa pekee ya kuwezesha mambo kwenda ni kukunja uso ili watu wajue unatisha ingawa ukweli wa mambo ni kuwa unaogopa watu wakisogea karibu na kuanza kudodosa mambo ya kikazi watagundua weakness yako!
Uko sahihi. Huyu mama huenda hata hajui umuhimu wa nafasi ile katika jamii, na huenda alisukumizwa kuwepo pale kwa kupenda madaraka yale bila kujua wajibu wake; alitakiwa awe amejifunza kuwa "Great power comes with responsibilities"
 
Sidhani kama ni dikteta...nina shaka sana na confidence yake katika kuliendesha bunge. Inawezekana amevaa kiatu kikubwa kuliko mguu wake. Unajua tena kama unafanya kazi usio na elimu wala ujuzi nayo...dawa pekee ya kuwezesha mambo kwenda ni kukunja uso ili watu wajue unatisha ingawa ukweli wa mambo ni kuwa unaogopa watu wakisogea karibu na kuanza kudodosa mambo ya kikazi watagundua weakness yako!

Aliwekwa pale on purpose, and she serves that purpose.
 
Sidhani kama ni dikteta...nina shaka sana na confidence yake katika kuliendesha bunge. Inawezekana amevaa kiatu kikubwa kuliko mguu wake. Unajua tena kama unafanya kazi usio na elimu wala ujuzi nayo...dawa pekee ya kuwezesha mambo kwenda ni kukunja uso ili watu wajue unatisha ingawa ukweli wa mambo ni kuwa unaogopa watu wakisogea karibu na kuanza kudodosa mambo ya kikazi watagundua weakness yako!

Lack of confidence breeds dictatorship! Hana confidence ndiyo maana anatumia ukali. Makinda ni dictator
 
Anahisi wapinzani wanataka kumchezea, hisia tope hizo. Na yeye anataka kwenda na kiwango cha aliyepita dooo itakua ngumu sana
ajui amewekwa na mafisadi na mwisho anataka kuwanyamazisha wapinzani mapema mmmmh sijui kama atafanikiwa.
 
Hata jimboni kwake mwendo ni huo tu, maamuzi yake kusema kweli ni amri moja na yeyote atakayebisha atakiona cha moto. Sio kwamba kuchaguliwa mara kwa mara na watu jimboni kwake anapendwa sana bali anaogopwa sana. Kuna tetesi pia kwamba amesheheni "utaalam wa kiafrika" na wanamjua vizuri sana. Tutegemee kuangukaanguka hovyo watu bungeni safari hii, maana wengi sana walioingia pale wapeuliza kwa wataalam kibali cha kuingia pale. Tatizo litaongezeka zaidi kwa sababu watunza misalaba safari hii nao idadi sio haba ingawa visima virefu navyo vimo.
 
Yaani swali lako km wewe unajijua ni mwanaume na umeishi kianaume siku zote kivitendo n.k. siku tu unaamua kutuuliza hivi mm ni mwanaume? Huyo mama ni kati ya yote aliyosema Umkhontoswize zaidi yake kuongezea ni kwamba she's INSANE.
 
wahenga katika kunena walipata kusema kwamba 'Lisemwalo lipo', tuvute subira tukingoja kuthibitisha!
 
Wanajamii,

Kuna mtu ana CV yake atuwekee? Kama hakuna basi walau tujue kiwango chake cha elimu.

Kazi ya uspika wa kipindi hiki utakuwa mgumu sana. Kama amepania kudhibiti na kuilinda serikali atakuwa anafanya makosa sana. Wabunge kazi yao ni kuibana serikali ili ihudumie wananchi ambao wanawakilishwa na wabunge. Hili bunge ni la la vyama vingi, wabunge wa upinzani wanatetea taifa zima, wanawakilisha zaidi ya majimbo yao. Wabunge wengi (si wote) wa CCM walishinda kwa pesa zao na usaidizi wa tume ya uchaguzi na sio kwa utashi wa wananchi ndiyo maana hata hawajali mambo yanayotuumiza watanzania. Wao wanajali tu kusimamia kitu kinaitwa maslahi ya chama chao. Hawana habari kuwa chama si chao tena ila ni cha Kamati Kuu peke yake.

Hivyo hata katika majimbo yetu yanayoongozwa na wabunge wa CCM tunawaona wapinzani kama watetezi wa kweli wa haki zetu. Hivyo Mheshimiwa Spika Anna Makinda aache kuwaonea wabunge wa upinzani. Watu walioouawa Arusha waliuawa mbali na kituo cha polisi. Dr Slaa alifuatwa na kupigwa mabomu kwenye mkutano halali, mbali na kituo cha polisi. Kuandamana au kugoma ni haki ya msingi ya raia kulezea kutokokuridhika kwake na uongozi au taasisi. Ni njia ya haki kujieleza kupinga uonevu au unyanyasaji. Lakini polisi waliwafuata viongozi wa CHADEMA na kuwapiga na kuwakamata.

Pinda nilikuwa namuheshimu sana lakini hivi karibuni amekuwa akisema sentensi zenye utata. Amekosa independence (uhuru) ya waziri mkuu inawezekana kuwa mtoto wa mkulima hakuna maana ile watu wanavyomfikiria. Ni mtu tu anayetaka umaarufu poa (cheap popularity) na wale si mtetezi wa wanyonge. Sokoine mtoto wa mfugaji alijitahidi kusimamia wanyonge, labda sijui mzee Peter naye angekuwa mtoto wa mfugaji??

Ninakerwa sana na utiifu wa kitapeli. Katika wakuu wetu wa serikali hawa wa sasa hivi wachache sana wanaoitumikia nchi kwa moyo wa dhati. Wengi wako pale kuji-position (kujiweka sawa) ama wapate gawio lao la mwisho au watasimama na kundi gani 2015.

INAUDHI STIFF!!
 
Back
Top Bottom