Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Nakubaliana na Ndahani. Huyu mama kapachikwa pale na mafisadi ili wadhibiti uendeshaji wa bunge. Hajui kanuni za bunge na not too long in the near future atajiumbua mwenyewe.

Huo ndiyo ukweli. Huyu mama hakutarajiwa kufanya tofauti na anavyofanya sasa. Ukweli ni kwamba anaifanya kazi yake bila ya kukiuka makubaliano. Hadidu za rejea alizopewa ni kuhakikisha kwamba mijadala yenye maslahi kwa taifa au mijadala yoyote yenye muelekeo wa kuwadhuru matajiri zake hailioni jua la siku. Ame-perfect art nzuri ya kudhibiti voice of reason zote na ndiyo maana hata uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za bunge ulikuwa ni kichekesho na mpango wa kudhibiti mawaziri wanaoonekan ni kikwazo cha MRADI WA URAIS wa MTU fulani. kwa ujumla Spika huyu ni kielelezo cha Bunge liloshindwa na kupwaya kuliko mabunge yoyote katika historia ya nchi hii. Lakini mimi naamini mara zote dhulma ina mwisho wake na hatimaye atatokea wa kuwafuta machozi watanzania hawa waliotiwa utumwani na HUU MHIMILI WA UOVU wa Spika huyu na makuhani wawili walioiweka nchi hii mateka.
 
Ndugu wana jamvi hivi kwa mtazamo wa undeshaji wa Bunge la sasa mbona naona kama Spika wetu huyu ana mfumo wa udictator??? Wenye information na utendaji wake wa huko nyuma atujuze.

mi nili comment hapa nikapigwa BAN ya miezi 3...ngoja nikae kimya nisije waudhi wakubwa
 
Kipimo cha kumjua mtu mwenye jazba au ambaye hajaridhika na hali fulani ni kuangalia kauli na mwenendo wake baada ya tukio au matukio husika...kwa wanaofuatilia vikao vya Bunge lililoahirishwa Dodoma,it is evident kwamba Spika wetu wa sasa ana jazba!! Hii ni kutokana na kwamba mara kadhaa amekua akidai yeye hana tatizo na mtu wala kinyongo wala hakasiriki!!! Na haya huyasema bila kuulizwa na mtu wala nini?? Saikolojia ya kawaida kabisa inatosha kuonyesha kwamba kila anapoongea haya huwa yupo katika msongo!! tunaomba mlio karibu mumshauri,atapata matatizo ya kiafya, kama bado hana!!!
 
Kipimo cha kumjua mtu mwenye jazba au ambaye hajaridhika na hali fulani ni kuangalia kauli na mwenendo wake baada ya tukio au matukio husika...kwa wanaofuatilia vikao vya Bunge lililoahirishwa Dodoma,it is evident kwamba Spika wetu wa sasa ana jazba!! Hii ni kutokana na kwamba mara kadhaa amekua akidai yeye hana tatizo na mtu wala kinyongo wala hakasiriki!!! Na haya huyasema bila kuulizwa na mtu wala nini?? Saikolojia ya kawaida kabisa inatosha kuonyesha kwamba kila anapoongea haya huwa yupo katika msongo!! tunaomba mlio karibu mumshauri,atapata matatizo ya kiafya, kama bado hana!!!

mkuu... kama ninakuona vile na nikisoma saikolojia yako .... umenifurahisha sana kuweza kuisoma saikolojia ya huyu mama ... tena haihitaji saikolojia kumsoma ... macho tu na hisia
 
hairekebishiki,ukitaka kujua sura yake na muonekano wake vinaashiria shari tu,nadhani hata moyoni ni hivyo hivyo tu
toka nimemjua kwenye siasa sijawahi kumpenda.nilishtuka alipochaguliwa spika.tutegemee mengi.
 
tulihitaji spika mwenye taaluma ya sheria ..aliyesheheneka na justice katika damu yake na sii mwana mama ambaye amekaa mkao wa kukariri kanuni na kuongoza bunge kwa kutumia busara rojorojo
 
Duh,nadhani ianzishwe namna ya kumrekebishe huyu mama,kuna siku atapigwa vichwa Bungeni...asipoangalia atakufa kwa presha,CHADEMA wachokozi sana!!!
 
Mkuu unaelewa unachokiandika au ndo umeamua kuongeza idadi ya posts kwako?

Naelewa nachoandika mkuu...CHADEMA wachokozi sana, kuna siku huyu mama yatamtoka matusi ya nguoni,nakwambia!!!
 
Lakini mie bado najiuliza kwanini walimwondoa Spika wa Bunge lililopita? Bado najiuliza mbona walimng'oa Samwel Sitta?
 
5170501743_1fe7e9bf8f_z.jpg
Kama kuna Mtanzania yeyote anafahamu malengo ya Makinda Bungeni au kama anajua kitu anachofikiria kichwani tunaomba atujulishe. Kinachoendelea Bungeni ni maigizo na ndoto tusiotaka kuiota. Huyu mwanamke naona hajui kazi ya "Tanzania Parliament" Tunacho kiona ni Bunge Kutaka kuwabuluza wananchi na kuwanyima haki yao. "This is not democracy" Bunge ni chombo pekee cha Kitaifa kutetea "Haki" na Kuchunguza shunguli zote za serikali. Kwanini Makinda anazuia uchunguzi wa Mabomu ya Gongo la Mboto? Hiyo Hiyo Serikali imeshindwa kuwalinda wananchi na hii ni mara ya pili sasa, kwanini tumwachie Kikwete, Mwinyi na Davis Mwamunyange. Tukirudi Dowans na EPA Makinda anamkumbatia Rostam.
Tusome hizi kazi ya Bunge kutoka website yao:
In view of that parliament can assumes the following roles:
-To pass laws for the good governance.
-To provide, by giving legislative sanction to taxation and acquisition
of means to carrying out the work of the government.
-To scrutinize government policy and administration, including
proposal for expenditure; and to debate major issues of the day.

Parliament of Tanzania

"Wananchi Twendeni Kuandamana Bungeni Square na Kumpa Makinda Ujumbe wa Wananchi"
 
Hajui akifanyacho sababu kawekwa na mafisadi huku akipewa maagizo yao kufanya watakavyo. yupo kwa ajili ya waliomuweka na si wananchi.... sera za Thithiemu ni maslai ya chama kwanza wananchi baadae endapo wakikumbuka na kilindana waziri mwinyi ataendelea kulindwa hata mabomu yalipuke kila siku
 
Aliwekwa na RA na wanamtandao wake sasa anachokifanya ni kukidhi matakwa yao,yaani hamna kusikiliza hoja kutoka CDM maana itaiuwa CCM hiyo ndiyo kazi aliyonayo

Mwisho wa siku wakamilishe kumweka EL kuwa mgombea urais,yaani wao tayari wanaangalia 2015 na kazi ni moja tu kuhakikisha kuwa EL atashinda na kweli anaonekana kushinda maana ukiangalia kamati za Bunge tayari yeye mwenyewe anawakabili wapinzania wake Sita na Membe na kuzuia issue ya Richmond/Dowans kijao wao tayari atawabana Makamba JR na pia kumbana Makufuli na Mwakiembe kupitia kwa kupitia Serukamba na hata IGP, DG-TIS kumpa briefing kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ni EL
Hivyo hii inaonyesha kuwa Bunge la kumi ni la aina yake tangia tupate uhuru

Yafaa kila mmoja akatafakari na kuchukua hatua nini kifuate baada ya hapo!
 
Back
Top Bottom