Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

hapo......usiku wa kiza.....ngoja tuone......hapa yatokee ya tunisia misri ndo kitaeleweka...!! naona tunaenda enda tuu..:A S 20:
 
Tatizo wabongo tunajua sana longolongo.Tupunguze kuongea tuanzishe mwendo.Maji ya moto hayaunguzi moto
 
Hivi mimi mwenzenu nimempenda sana Yule mama anayeitwa Makinda au Kinda, Huwa sichoki kumuangalia maana nikipata mama kama yule hakuna wakunichezea maana ni mkali kuliko Mbwa, sijui Rostam ameshamnunua amlinde. Nipeni namba ya Makinda au ninawezaje kuwasiliana nae kama kuna mtu anawezakunisadia nitashukuru sana:coffee:
 
hivi hayawezi tokea mapinduzi ndani ya bunge akarudi Sitta kwenye uspika?
Me huyu mama simpendi hata kidogo
 
Inaamana hata CCM kama hawako kwenye 18 za EL na RA inakula kwao au? Tusubiri siku RA au EL wakiwa wanachangia, ili tuone her response and attitude...................

Wewe inaonekana haupo Tanzania, ni nani aliyekudanganya kwamba Rostam Aziz ana muda huo wa kuchangia mada? kwa taarifa yako bunge lililopita yeye ndio mbunge aliyeweka rekodi ya kutochangia chochote mpaka bunge linavunjwa. wewe unamjua Rostam au unamsikia tu? nawasikitikia sana watu wa Igunga. visenti mbuzi anavyowahonga na bado wanamrudisha bungeni wakati yeye bungeni huwa hana mpango napo zaidi ya kuutumia ubunge kujilinda kwenye biashara zake. kweli watu wa Igunga inabidi waanze mkakati kuanzia leo hii kuelekea 2015 ili kumng'oa huyu Muiran.
 
Ndo anachomaanisha,yeye kwake mradi mtu kajibiwa,ubora au usahihi wa majibu yeye haumhusu,anachotaka ni mtu ajibu chochote,in short anakera na sioni busara yake kwenye hilo!

Dai Slek Shia,

Nimefuatilia michango yako kwenye jukwaa hili nashawishika kukupongeza.
You are informed na reasoning yako inaangalia hoja. Keep up the good work!

Ni bahati mbaya sana Mh Spika anawaangusha kina mama wa Tanzania pengine ni kwa sababu alishinda not based on merit.
Sitarajii jema kutoka kwa mama Makinda na ikitokea akatenda lenye masilahi wa watanzania nitahesabu kwamba kalitenda kwa makosa tu!
 
mi nadhani mama bado anachukua uzoefu, lakini kama sihivyo amewekwa na mafisadi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huyu mama namfahamu tangu nakuwa hana mtoto wala mwenza.ukitaka uhakika nenda kijitonyama national haosing karibu na mabatini ndiko anakoo ishi.yuko na watoto wa ndugu zake tu.:twitch::twitch::twitch::twitch::twitch:
 
Makinda alaumiwa kwa kuchakachua kanuni


na Nuru Yanga


amka2.gif

JOPO la uangalizi wa shughuli za Bunge kutoka Kituo cha Sheria na Haki za binaadamu (LHRC) limesema wamesikitishwa na kitendo cha Bunge la Kumi linaloendelea jijini Dodoma kuchakachua baadhi ya kanuni na kubadilisha maana na tathmini ya sura nzima ya kanuni hizo.

Hayo yalisemwa juzi na mmoja wa waangalizi wa shughuli hizo, Deus Kibamba, wakati wa sherehe za uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya utendaji wa Bunge la Tisa zilizofanyika katika kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili mara baada ya sherehe hizo, Kibamba alisema Bunge la Kumi limeanza kuchakachua kanuni zilizobadilishwa mwaka 2007 ambapo wabunge kutoka chama cha upinzani wakitimia asilimia 12 wanaweza kuunda kambi ya upinzani lakini Bunge limebadilisha kanuni hiyo hadi kubadili sura nzima ya kanuni hiyo.

“Tumesikitishwa sana na kitendo cha Bunge la Kumi cha kubadilisha kanuni ambayo ilirekebishwa na Spika aliyepita wa Bunge la Tisa ambapo kanuni hiyo ilisema wabunge wa upinzani wakitimia asilimia 12 wanaweza kuunda kambi ya upinzani lakini tumeshuhudia CHADEMA ikichakachuliwa na kurekebishwa kwa kanuni hiyo,” alisema Kibamba.

Pia alisema kanuni na sheria za Bunge zinasema kambi ya upinzani inaweza kuchagua wenyeviti wa kamati tatu muhimu wanazopewa lakini cha ajabu chama tawala kimewachagulia kambi ya upinzani wenyeviti wa kamati hizo.

Akitoa mfano wa wenyeviti waliochaguliwa na chama tawala ni Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo ambaye alishawahi kufukuzwa kazi na kambi ya upinzani katika Bunge lililopita jambo ambalo alisema halijawatendea haki kambi ya upinzani ya kumjadili na kufanya maamuzi ya kumrejesha au laa.

Pia alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha vyama vingine vya upinzani kufurahia chama tawala kuchakachua kanuni na kuweza kuzibadilisha kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Aidha alisema kitendo cha kumchagua Mbunge wa Monduli, Edwad Lowassa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ambayo Mbunge wa Urambo mashariki Samwel Sitta ni mmoja wa wajumbe inaashiria kuwa Bunge la Kumi ni la kulipana visasi na kukomoana.

Wakati huohuo, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuongoza Bunge kwa kufuata kanuni na taratibu za Bunge na si kuongozwa kwa itikadi ya chama chake.

Hayo aliyasema jana Katibu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Ally Chitanda wakati wa kutoa tamko la mustakabali wa wabunge wa chama hicho kwa juhudi wanazozionyesha bungeni katika kutofautiana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani.

Alisema kuanzia Bunge lilipoanza wabunge wa CHADEMA wameonyesha msimamo kwa kuonyesha kile wanachokihitaji kwa maslahi ya Watanzania kwa kutokubaliana na hoja za wabunge wengine.

Chitanda alisema kuwa mwenendo wa Bunge unaonyesha Spika Makinda anashindwa kuliongoza kutokana na kukifuata chama chake katika kutaka kupunguza makali ya wabunge wa CHADEMA. “Tunataka Spika kufanya kazi zake kwa utashi na misingi inayopaswa kuendesha Bunge kama mhimili unaojitegemea, hii italeta heshima kwa chombo hicho na kuachana na itikadi au shinikizo kutoka upande fulani kwa maslahi binafsi,” alisema Chitanda
 
Huyu mama atakujajuta kwa anayoyafanya
Huenda hatajuta kama anayoyafanya hayaingiliani na malengo yake. Ni vizuri kutambua malengo yake wakati anagombea nafasi ile; je alitaka kuacha legacy ya namna gani? Kama aligombea kwa ajili ya mshiko basi huenda asijute kabisa, bali akazidi kufurahia kuwa mshiko wake unapanda chati kila anapoboronga kwenye upande wa legacy yake.
 
toka mwanzo ilijulikana huyu mama atakuwa kikwazo sana

Lakini kama Watanzania tukiamua kutomruhusu na upumbavu anaoutaka kuufanya dhidi ya Bunge hili basi itabidi aogope. Anaweza kushindana na nguvu ya umma kweli kama tukiamua kulalamika kwamba haturidhishwi na utendaji wake kama Spika?
 
.... wote tunajua wakina chenge, RA, EL na Makamba ndio waliomuweka pale, na wakampa mwongozo na tafsiri ya ufisadi kuwa ni kuchukua mke wa mtu tu, DOWANS, Richmond, Kagoda, Meremeta, Deepgreen asiguse.
.....kinachoshangaza mke wa ccm kamlengeshea CHADEMA, sasa mama-Kinda huu si ufisadi kwa tafsiri yako mwenyewe kweli? maana ule ushenga unatia mashaka juu ya dhamira yako kwa taifa hili.
 
Back
Top Bottom