Moto wa Katiba Mpya CHADEMA kutinga Ikulu; KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka

Mkuu hapo penye red ndo pamenifanya nichangie kwenye hii thread ambayo ni crap tupu.
Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team.
Mswalie mtume walahi ili iweje!! Rais mwenye udenda anachaguaga???!! epusha balaa bwana weweeee??!!
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CHADEMA.

Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
Kumbuka kuwa haya wanayopeleka yameshajadiliwa kwenye kamati kuu ambapo pia kuna akina mdee, lucy rejia na wengine so mawazo na matakwa yako yatakuwa involved, na kama kutakuwa na suala la jinsia linalohitaji mwanamke anaweza kuongezwa tu with time!!!!
 
hoja ina nguvu mana jenda ni siasa na nadhani cdm wangeitumia ingewaongezea credit sana,lakini nasikitika wana jamvi wana tabia ya kutukana watu wanaoleta thred ambazo wao haziwafurahishi.tubadilike wandugu.....kama hujapendezwa na jambo changia kwa ustaarabu.
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CHADEMA.

Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja...
Mkuu tujulishe wengine tuko mbali na Bandari ya salama, kwani yule bwana ni MNGESE.
 
Ni crap kwa mawazo yako duni na huko kwa Mbowe mtangulize kwanza mama yako na dada zako kama unadhani hii ni njia sahihi ya kurespond thread usiyoipenda.......
sasa nimekuelewa. Elewa kuwa kamati ya chadema haina muda wala mawazo ya kipuuuzi uliyoyaainisha kwenye bandiko lako la kwanza eti wanawake wawepo ili kumfurahisha Kikwete. Na kama ni kumfurahisha tu nashauri na hulazimiki kuchukua ushauri wangu, mpeleke mama yako kwenye kamati ili Kikwete akafurahi nae...
 
Wewe unayedhani ni sahihi kumpelekea Mbowe mama yako endelea tu siwezi kukukataza, thread yangu inahusu kamati kutokuwa na mwanamama, kama una akili changia maudhui ya thread yangu na usianzishe mapya.
Nimesha changia...nina akilie....
turudi kwenye hoja yako...mawazo yako ni ya msingi sana lakini uliharibu kwenye maneno haya
Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
maneno uliyoyatumia ni rahisi pia na wewe kujibiwa kama ulivyojibiwa huko juu..
 
sasa nimekuelewa. Elewa kuwa kamati ya chadema haina muda wala mawazo ya kipuuuzi uliyoyaainisha kwenye bandiko lako la kwanza eti wanawake wawepo ili kumfurahisha Kikwete. Na kama ni kumfurahisha tu nashauri na hulazimiki kuchukua ushauri wangu, mpeleke mama yako kwenye kamati ili Kikwete akafurahi nae...

Na ndio maana nikaomba unioneshe mfano kwa kuanza kumpeleka mama yako kwanza kisha ndio ulete majibu kama haya
 
.
hoja ina nguvu mana jenda ni siasa na nadhani cdm wangeitumia ingewaongezea credit sana,lakini nasikitika wana jamvi wana tabia ya kutukana watu wanaoleta thred ambazo wao haziwafurahishi.tubadilike wandugu.....kama hujapendezwa na jambo changia kwa ustaarabu.
Mbona amejibiwa kwa usataarabu yeye kasema hivi "Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja...." akajibiwa hivi "Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team" sasa ulitaka ustaarabu upi utakao endana na swala lake
 
MODS, mada ya kumuona Rais ni tofauti na mada ya tamko. ukizichanganya mada hizi flow ya mjadala inakinzana,mada ya kumwona Rais haioko kwenye tamko la chadema usiunganishe mada tofauti ya tamko na kumwona Rais kwenye mjadala mmoja. thread yangu iachwe ijitegemee ili tupate mtitiriko bora wa mada hizo mbili.

My take: Nawapongeza chadema kwa kutambua mapema kwamba kama wakisusa wenzao watakula. katiba itatengenezwa na wao chadema watabaki nyuma. hata hivyo sijui kama watamalizaje matakwa ya wafuasi na mashabiki wao wanaotaka maandamano nchi nzima.

Wamechukua uamuzi mpya na mzuri kwa wakati muafaka kwa sababu hata kama wangeamua kwenda kufanya maandamano Rais asingeweza kuwapa fursa ya kuwasikiliza. Wamegeuka nyuma na kuchagua kilicho bora kwa sasa.

Badala ya kutoa masharti ya namna ya kumuona Rais chadema wajiandae kwa hoja za kumshawishi Rais na Rais atakuwa na hoja zake. Kama chadema wataanza kwa kumpa masharti Rais kabla ya kuonana naye na Rais akitoa masharti kwa chadema kabla ya kuwapokea Ikulu wazo jema la chadema litakufa.

Pande mbili zenye masharti kamwe haziwezi kukaa kwenye meza ya mazungumzo. Chadema bebeni hoja kwenda kwa Rais msibebe masharti.

Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kuja na hoja nzito na nzuri kama hii. Tokea mikiki ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni dhahiri kuwa viongozi wakuu na kamati kuu ya CDM hawajapati fursa ya kupumzika ikizingatiwa matukio yakiyofuata mara tu baada ya uchaguzi.

Ni kutokana na stress hizi chama kimerudi nyuma kidogo katika priotisation yaani kipi kitangulie na kipi kifuate. Hivi kati ya viongozi wakuu na mwanasheria wa chama Mhe Tundu Kissu kukimbilia Arusha na hatimaye kukamatwa na kufunguliwa mashataka kisa eti Mhe Godbless Lema kakataa dhamana ya mahakama anataka kwenda magereza na kutangulia kutoa elimu kwa umma ya nini maana ya muswada wa sheria kusomwa kwa mara ya kwanza au mara ya pili bungeni kabla ya kufikishwa kwa muswada wa mchakato wa marekebisho ya katiba ni kipi kilihitajika kufanyika mwezi Oktoba/Novemba 2011.

Matokeo yake muswada wa mchakato wa marekebisho ya katiba ulipowasilishwa bungeni, CCM na Spika wakifahamu watanzania hawana elimu ya uraia na hata wasomi hawafahamu kanuni za bunge wakatumia mudhaiifu huo kuwasilisha muswada huo bungeni na Spika akatumika kuzima nguvu wa wabunge wa upinzani. Mabishano yalipoanza kati ya wabunge wa CDM na wale wa CCM kuhusu utaratibu wa kusomwa kwa muswada huu muhimu sana, mamilioni ya watanzania tukabaki tumepigwa butwaa tukishindwa kujua tuchukue hatua ipi kwa kuwa hatukuwa tukielewa chochote kinachobishaniwa.

Kihistoria madai ya katiba mpya sio ajenda na haijawahi kuwa ajenda ya CCM ni ajenda ya wapinzani kwa ujumla wao, binafsi sioni kukutana na JK kutusaidia nini kufikiwa kwa madai ya CDM na wapinzani ikizingatiwa kuwa kutekelezwa ka madai ya CDM ama wapinzani kuna maana moja nayo ni kuondoa katika katiba yetu mianya inayotumiwa na CCM kushinda chagzui au kuiba kura.

Kwa maoni yangu badala ya kukutana na JK, CDM ingepanga mikutano na CUF kwa maana kutafuta usuluhishi baina ya vyama hivi kwa lengo la kujenga nguvu za vyama vya upinzani kudao katiba mpya na haki za watanganyika na wazanzibari ambao wataingia katika muungano kwa ridhaa yao wenyewe badalaya hali ilivyo sasa.
 
.Mbona amejibiwa kwa usataarabu yeye kasema hivi "Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja...." akajibiwa hivi "Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team" sasa ulitaka ustaarabu upi utakao endana na swala lake

Kama unaona ni ushauri mzuri basi peleka mama yako ndugu, mbona unapingana hata na wachangiaji walioona ukosefu wa ustaarabu hapa? Hoja hapa ilikuwa ni kujumuishwa wanawake. Iwe kwa lengo lolote lile; mama yangu anatoka wapi tena? Sasa anza wewe kumpelekea Mbowe mama yako ndio uje na ushauri huu
 
Wewe si ndiyo unae taka kumfarahisha Kikwe te kwanini usifanye hivyo.....

Sijakataa lakini kwa nini usianze kumpelekea wewe mama yako. Kama mama yako kafa peleka hata mke wako? Kisha ukirudi ubaki katika maudhui ya thread na sio kutaka ku-abuse individuals hapa.
 
Baada ya magwanda kutambuwa kuwa sera yao ya kususasusa imewageukia juzi bungeni na hususan baada ya kuchambuliwa na Kikwete alipokutana na wazee, Watanzania wengi wamewaona viongozi waliowachaguwa kuwawakilisha bungeni kwa tiketi ya magwanda wamekosea na hawakuwatendea haki kwa kususasusa kwao na kutokuweza kupinga mswaada kwa kufata sheria na badala yake wakafata kuonekana kwenye Tv wakisusa. Hilo ni pigo kubwa sana kwa magwanda wakikubali wasikubali ilikuwa si busara kususasusa kama mitoto inayo deka, unamdekea nani?

Kwa kuwa wameshalikoroga turufu yao kwa sasa ni kumtambuwa Rais waliyesusa hata kusikiliza hotuba na kuomba kukutana nae ili japo kidogo warudishe hadhi kuwa waonekane wanafanya kazi.

La kumuona Rais, najiuliza na niliuliza humu wanakwenda kumuona kama Rais? au Mwenyekiti wa CCM ?

Wajipange vizuri, Kikwete ni kicha na alishawahi kusema "waende watarudi" na sasa imetimia.

Umewashuka haooooo.
Huyu gamba wa kike huwaga simwelewi au genius huyu. Kila akianza anaanza na ushabiki. Ukitaka umkasirishe huyu fox mtaje JK lakini sioni maake jamaa kwa mijimama hajambo!!
 
Mimi sioni ubaya wowote kwenye kamati hii. Kamati ni nzuri yenye wasomi wazuri wa sheria kama akina Prof. Safari kwahiyo tutegemee mambo yataenda vizuri.
 
Watu wamechaguliwa kwa uwezo wao na nia maalum. Kwanza Kikwete ili kukutana na hao wajumbe itabidi afikirie mara mbili mbili kwanza kwani hao ni watu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja both kisiasa na kisheria.

Hao maprofessors wawili ni watu waliobebea kitaaluma kwenye mambo ya siasa na sheria.
 
gender balance crap! Bado kidogo tutadai waliofaulu mbona hakuna mwanamama. Kwani waliochaguliwa si ni binadamu? What gender have to do with kamati?
 
Majina ambayo nayakumbuka ni: Dr Slaa, Mbowe, Tundu Lisu, Prof Safari, Prof. Baregu...
Cracwise, kuna point ya kuzungumzika kwenye hoja yako, ila ondoa hiyo dhana ya uwepo wa mwanamke
kwenye kamati kwa ajili ya kukidhi hobbie ya Mkuu wa Kaya sababu japo unamaanisha kuwapigia chapuo
wanawake ila umewadhalilisha kwa kiwango cha juu sana. naomba uwe muungwana tafadhali
 
Mkuki kwa nguruwe, hahahahaaaaa......


Wewe unayedhani ni sahihi kumpelekea Mbowe mama yako endelea tu siwezi kukukataza, thread yangu inahusu kamati kutokuwa na mwanamama, kama una akili changia maudhui ya thread yangu na usianzishe mapya.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom