Ubunge kama vilivyo vyeo vyote vya kisiasa nchi hii ni uwekezaji unaolipa sana. Hawawezi kusema wanalipwaje. Tunagharamia sana SIASA kwa kisingizio cha demokrasia. Ndio maana mimi nasema tupunguze ukubwa wa Bunge letu. Ni kubwa mno. Zanzibar ina Wabunge wawili kila jimbo ingawa mwingine anajiita mwakilishi. Hapa kwetu kuna Halmashauri/ Manispaa/ Miji ina wabunge zaidi ya wawili kwa vigezo vya kijinga kabisa vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kuna VITI MAALUM vya akina Regia zaidi ya 150. Chaguzi zenyewe na hatimaye Bunge lenyewe ndio hilo!