Mnyika, Zitto na Regia: Tupeni mchanganuo wa hela zinazolipwa kwa Mbunge ili tujue

Shukran Regia! Nilipata nafasi jana ya kuongea na kijana mmoja wa Kiingereza na yeye alinieleza wazi wazi mapato ya mbunge wake bila kuguna. Sasa kilichopo hapa kwetu ni nini? Kuna haja ya kuiwajibisha serikali yetu. Hawana madaraka ya kukataa kutoa mishahara ya wabunge wetu. Hii ndiyo sababu wanakuwa na uwezo wa kuongea kama wanavyotaka. Kama jana haka kamama kalivyoongea, kalinikera sana mimi.
 
Msando Ablert!...unaheshimika mzee!

Majibu ndio haya, na obviously amejibu kama nilivyodokeza awali kwenye post yangu No 14 juu!
Japokuwa mheshimiwa ameweka wazi kwamba tuwe na subira, yatakuja wekwa hadharani tu siku moja kwa namna nyingineyo tofauti na hapa.
So currently we have to reserve our comments.

One thing, hapa niliponasikia mwili wote umeganda. In all honesty, I feel pain na nakosa majibu ya maswali yote ninayojiuliza. Sasa hii ni nini? Kuna sababu gani anachopata Mbunge kiwe siri? Hili halistahili kuvumiliwa. Lazima tulishikie bango. Kwa nini wanaficha? Unawezaje kumficha muajiri wako? Mbunge wangu lazima atuambie wananchi anapata nini kwa kazi tuliyomtuma. Hizo kanuni ni kwa ajili yao sio kwa ajili yetu sisi. Hazitufungi hata kidogo. Na nitazitafuta nione zinasemaje ili tujue nini kifanyike.
 
Msando.Heshima Mbele!How are you?

Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.

Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.

Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.

Aluta Continua.
Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.

Watanzania halafu bado mnaamini Hicho ni chama cha Watu Makini. Watanzania Tumeliwa!!!, hakuna cha Upinzani kwa ajili ya Masilahi ya Watanzania wala nini, Maslahi binafsi ndiyo wabunge hao wanaweka mbele, hawajali kabisa kwamba kwa kukubali inayoitwa eti "mkopo" hiyo bila kuhoji, na pia kujaribu Kuficha habari za kupatiwa pesa hizo ni dalili ya UjanjaUjanja usio na faida kwa Wananchi.

Ni lini hawa watu watajitofautisha na wale walioshindwa kutetea maslahi ya Umma?.
Wana Moral Authority gani ya kukemea Ufisadi lakini hawako Tayari kukemea pesa za bwerereree wanazopata bila kuzitolea jasho stahiki, na ambazo kila senti inayoingia mfukoni mwao ina thamani kubwa sana kwa raia masikini?

Hawa Watu wametuangusha sana, hii siyo kauli mbiu ya Uchaguzi waliyoombea kura katika majimbo yao, na wala si kauli mbiu waliyoombea kura za Uraisi kwa Mgombea wao.
 
safi sana mbunge,asante kwa mrejesho wa taarifa natumai umeeleweka vilivyo....
 
Mheshimiwa Regia,

Kwanza nikupongeze kwa kujitokeza na kutujibu yale tunayojiuliza. Nikushukuru pia kwa kuwa mkweli kwetu kwa sababu tumeweza kufahamu kwamba semina Elekezi nia yake ilikuwa kuwafunda jinsi ya kuungana na watawala na kuendeleza usiri katika mambo ambayo ni ya wananchi.

Hilo pia ni jambo la msingi kwetu kufahamu. Naamini kabisa kwamba siri hii haitakuwa ya muda mrefu nitajulikana. Sioni sababu ya viongozi kuambiwa wataje mali zao zote halafu wakati huo huo waambiwe wasiseme kiasi gani wanapata kutokana na nafasi zao za uongozi. Imefika wakati sasa tusimamie uongozi wa kuwajibika kwa wananchi.

Bunge lisjigeuze kuwa wananchi. Siku zote Bunge ni chombo cha uwakilishi na sio anayewakilishwa. In other terms, an agent does not become the principal when appointed to act as an agent. He or she remains an agent forever. He can not bestow on himself or hereself the 'being' of the principal. Sasa Bunge letu lazima litambue hilo, linabaki kuwa chombo cha uwakilishi sio lenyewe ndio linakuwa 'wananchi'.

Wabunge wa CDM wanaomlaumu Lema kwa kutoa siri ya mikopo tuwafahamu. Endapo tutawajua hakuna haja ya kuwaonea haya. Muda wa kubebana na kuoneana haya kisa ni mwenzangu hakuna. Hicho ndicho kilichotufikisha hapa na CCM!! Maslahi ya chama mbele. Hakuna. Maslahi ya nchi mbele halafu chama kitafuata baadae. Mtu akienda tofauti na yale tunayoyasimamia hakuna kumuonea aibu, ni kumdiscipline right away. Ni heri kuwa na Wabunge Wawili wenye uadilifu kuliko kuwa na Wabunge Mia mbili ambao sio waadilifu.

Suala la posho za wabunge tutalileta hapa wenyewe ili wananchi wajue ukweli wa jambo linalowahusu.
 
Watanzania halafu bado mnaamini Hicho ni chama cha Watu Makini. Watanzania Tumeliwa!!!, hakuna cha Upinzani kwa ajili ya Masilahi ya Watanzania wala nini, Maslahi binafsi ndiyo wabunge hao wanaweka mbele, hawajali kabisa kwamba kwa kukubali inayoitwa eti "mkopo" hiyo bila kuhoji, na pia kujaribu Kuficha habari za kupatiwa pesa hizo ni dalili ya UjanjaUjanja usio na faida kwa Wananchi.

Ni lini hawa watu watajitofautisha na wale walioshindwa kutetea maslahi ya Umma?.
Wana Moral Authority gani ya kukemea Ufisadi lakini hawako Tayari kukemea pesa za bwerereree wanazopata bila kuzitolea jasho stahiki, na ambazo kila senti inayoingia mfukoni mwao ina thamani kubwa sana kwa raia masikini?

Hawa Watu wametuangusha sana, hii siyo kauli mbiu ya Uchaguzi waliyoombea kura katika majimbo yao, na wala si kauli mbiu waliyoombea kura za Uraisi kwa Mgombea wao.

Huu ndio ushabiki wa kijinga ambao unaturudisha nyuma. Tunaongelea Chama au Wabunge? Tofautisha Chama makini na Wabunge Makini. Kwani Regia ni Mbunge wa Chama gani? Mimi ni Diwani wa Chama gani?

Kama mtu akikosea na ni mwanachama wetu tuna kila sababu ya kutokumuonea aibu, hicho ndicho chama makini. Chadema hakisimamii posho kubwa kwa wabunge. Kumbuka vita na maneno ya Dr. Slaa katika hili. Uliza msimamo wa Chama kuhusu hili.

Jitahidi siku zote katika maisha yako kuwa wa msaada kwa nchi yako na nafsi yako mwenyewe. Unapoamua kuandika kitu fikiria ni msaada gani unaoutoa kwa nchi yako na nafsi yako. Huo ndio uwe muongozo wako. Ushabiki usiwe muongozo wako. Hata kama nia ni kuirekebisha CDM sio kwa njia ya kulalama na kukatisha tamaa watanzania kwa maneno 'tumeliwa' nk. Jenga hoja yako vizuri na ujumbe wako utafika.
 
Nadhani inajulikana kuwa posho ni kubwa na wanalipwa mara mbili wakati mwingine na iliwai kuongelewa katika bunge lililopita. Lakini what next baada ya kujua? Tutademand zipunguzwe? Je tutajuaje kuwa baada ya kupunguzwa zitaenda kwenye yale tuliyoyategemea? Maana kama PM anasema sitaki mashangingi linaletwa kwako analisusa linapelekwa kwa mwingine je amesaidia hapo? Hivyo hivyo posho hizi tunauhakika kuwa baada ya kupunguzwa zitaenda tulikotegemea?

Mimi nadhani kuwe na njia bora ya kupunguza matumizi ikiwemo chai iliyotengewa 20 billions ili hata wabunge wakikatwa tujue inakwenda wapi. Au iwekwe hadharani for the time being kuwa kila mbunge akatwe kiasi fulani kitumike kwenye kitu fualni au iwekwe motion bungeni hata hoja binafsi ya kureview hayo malipo ili hela hizo ziende kwenye vitu vya maendeleo. Maana kila mbunge akitoa Milion 1 tuna M 300 kwa mwezi, kwa mwaka 3.6 Bilion, hii inajenga madarasa kibao au hata barabara ya zaidi ya km 3 kiwango cha lami.(APPROXIMATE FIGURES)

ITAFUTWE JINSI YA KUPUNGUZWA TUNAJUA POSHO NI KUBWA SANA.
 
Bunge lisjigeuze kuwa wananchi. Siku zote Bunge ni chombo cha uwakilishi na sio anayewakilishwa. In other terms, an agent does not become the principal when appointed to act as an agent. He or she remains an agent forever. He can not bestow on himself or hereself the 'being' of the principal. Sasa Bunge letu lazima litambue hilo, linabaki kuwa chombo cha uwakilishi sio lenyewe ndio linakuwa 'wananchi'

Mkuu, Msando,
Literally, bUNGE NI AGENT wa Principal Wananchi.
Lakini naamini unajua 100% kwamba kiuhalisia haitendeki hivyo.
Kubwa zaidi nilionalo mimi, ni kwamba Bunge kama mhimili wa serikali lina Bajeti yake inayopitia kwenye Ofisi ya Waziri mkuu- Sera, Uratibu Bunge.
Sasa basi, kama bajeti hii inapitishwa kwa mbwembwe zote, basi wa kulaumiwa si beneficiary wa maslahi...maana anapewa kilichopitishwa kiuhalali na muhimili wa Dola, ambapo vitu kama mikopo ya magari ni inclusive.

Sheria za utendaji wa Zimamoto zinasema "dont extinguish the flame, but the base of flame"!...sisi tunahoji wanachopewa wabunge, lakini for that case tulitakiwa kuikataa bajeti in principal, ambayo breakdowns zake zilionyesha wazi kuwa zinayo fedha ya mkopo wa usafiri kwa Mbunge!..huh!
Hata kuwachukia baadhi ya wabunge wa cdm(kwa hali ya sasa ya ratio ya upinzani vs tawala) ni futile!

Kuna njia/suluhu ya kufanya ambayo wote tunaijua...tuitumie hiyo siku za usoni!
Ni mtazamo tu!

Nadhani inajulikana kuwa posho ni kubwa na wanalipwa mara mbili wakati mwingine na iliwai kuongelewa katika bunge lililopita. Lakini what next baada ya kujua? Tutademand zipunguzwe? Je tutajuaje kuwa baada ya kupunguzwa zitaenda kwenye yale tuliyoyategemea? Maana kama PM anasema sitaki mashangingi linaletwa kwako analisusa linapelekwa kwa mwingine je amesaidia hapo? Hivyo hivyo posho hizi tunauhakika kuwa baada ya kupunguzwa zitaenda tulikotegemea?

Mimi nadhani kuwe na njia bora ya kupunguza matumizi ikiwemo chai iliyotengewa 20 billions ili hata wabunge wakikatwa tujue inakwenda wapi. Au iwekwe hadharani for the time being kuwa kila mbunge akatwe kiasi fulani kitumike kwenye kitu fualni au iwekwe motion bungeni hata hoja binafsi ya kureview hayo malipo ili hela hizo ziende kwenye vitu vya maendeleo. Maana kila mbunge akitoa Milion 1 tuna M 300 kwa mwezi, kwa mwaka 3.6 Bilion, hii inajenga madarasa kibao au hata barabara ya zaidi ya km 3 kiwango cha lami.(APPROXIMATE FIGURES)

ITAFUTWE JINSI YA KUPUNGUZWA TUNAJUA POSHO NI KUBWA SANA.

Mugerezi, tambua pia kila Mbunge anatakiwa alipe kiasi fulani kwa chama chake (huu ni utaratibu wa vyama sio sheria) ili kujenga chama. Ninavyofahamu (mimi sio mtaalamu wa kodi) malipo kwa Mbunge hayakatwi kodi, hivyo fedha hizo zinazoeenda kwa vyama vya siasa zinakuwa accounted for vipi haieleweki. Hili ni jambo la kuchunguzwa pia.

Haya yote yanagusa maslahi ya wnegi na sio vitu ambavyo vitampatia mtu wafuasi wengi. Ila penye ukweli tuweke wazi.
 
Mkuu, Msando,
Literally, bUNGE NI AGENT wa Principal Wananchi.
Lakini naamini unajua 100% kwamba kiuhalisia haitendeki hivyo.
Kubwa zaidi nilionalo mimi, ni kwamba Bunge kama mhimili wa serikali lina Bajeti yake inayopitia kwenye Ofisi ya Waziri mkuu- Sera, Uratibu Bunge.
Sasa basi, kama bajeti hii inapitishwa kwa mbwembwe zote, basi wa kulaumiwa si beneficiary wa maslahi...maana anapewa kilichopitishwa kiuhalali na muhimili wa Dola, ambapo vitu kama mikopo ya magari ni inclusive.

Sheria za utendaji wa Zimamoto zinasema "dont extinguish the flame, but the base of flame"!...sisi tunahoji wanachopewa wabunge, lakini for that case tulitakiwa kuikataa bajeti in principal, ambayo breakdowns zake zilionyesha wazi kuwa zinayo fedha ya mkopo wa usafiri kwa Mbunge!..huh!
Hata kuwachukia baadhi ya wabunge wa cdm(kwa hali ya sasa ya ratio ya upinzani vs tawala) ni futile!

Kuna njia/suluhu ya kufanya ambayo wote tunaijua...tuitumie hiyo siku za usoni!
Ni mtazamo tu!

PakaJimmy, nimekusoma. Njia hiyo tunafanyaje ili iwe na mafanikio? Tujadili kando! Kupanga ni kuchagua, na kuchagua ni kupanga. Kidogo kidogo tutafika.
 
Msando.Heshima Mbele!How are you?

Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.

Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.

Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.

Aluta Continua.
Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.

I see f u can't beat them join them
 
Mkuu, Chadema ni vema!
Nimesoma majibu yako kwa swali la diwani Msando na nimeelewa vizuri kile ambacho unataka kutuaminisha huku ukiacha ukweli halisi moyoni mwako.

Pamoja na kufungwa na "kanuni za usiri za bunge" binafsi najiridhisha kuwa kama kweli una nia ya kuweka mapato ya mbunge hadharani basi majukwaa yapo mengi, tena mengi sana, nasisitiza ni mengi mno. Unaweza hata ukatumia njia ya Anonymus na umma wote ukaelewa bila ya kuhatarisha kibarua chako kwa Anna.
Haya shime fanya hivyo kama uko siriaz.
 
Mnyika na Zitto mbona kimya? Tunasubiri majibu yenu. Au dada Regia amejibu kwa niaba yenu? Sidhani. Tunaomba majibu.
 
Mkuu, Chadema ni vema!
Nimesoma majibu yako kwa swali la diwani Msando na nimeelewa vizuri kile ambacho unataka kutuaminisha huku ukiacha ukweli halisi moyoni mwako.

Pamoja na kufungwa na "kanuni za usiri za bunge" binafsi najiridhisha kuwa kama kweli una nia ya kuweka mapato ya mbunge hadharani basi majukwaa yapo mengi, tena mengi sana, nasisitiza ni mengi mno. Unaweza hata ukatumia njia ya Anonymus na umma wote ukaelewa bila ya kuhatarisha kibarua chako kwa Anna.
Haya shime fanya hivyo kama uko siriaz.
Anitumie hata mimi kwa pM, nitaweka hadharani...Sasa hivi nchi hii ni kujilipua tu bana!
Huenda hata watoto na wajukuu zetu wataona faida!
 
Regia Mtema unaelekea kuwa mbunge bora,siamini kama Zitto na Mnyika na yale ma id yao mengine wameshindwa kutuambia ukweli

ha ha ha ha ha ha ha LOL! wamekusikia mkuu natamani wawe na maID mengine watupe kitu live bila chenga
 
Labda ni mimi sijui wakuu...

Hivi Mbunge anafanya kazi gani nzito kumzidi Mkuu wa shule ya seko?...kwa kuangalia Mkuu wa seko ana wajibu mzito sana kulinganisha na Mbunge!...mbaya zaidi ni kwamba wengine ndio wanapata nafasi nzuri ya kusinzia mule ndani ya mjengo!

Au title ya "kuwakilisha jimbo" inaonekana nzito sana..mbona hata hivyo hatuwaoni majimboni?...au niile kugonga yale madawati kukubaliana na hoja?...ni kazi gani ya ziada wanafanya inayostahili kulipwa hela nyingi hivi na fringe benefits za kuudhi?

Ningepata POWERS leo hii Mbunge anapata mwisho wa mwezi mshahara sawa na wa AfisaElimu(W)...basi!

Naomba nisaidiwe hizo kazi, maana nahisi kupungukiwa ufahamu!
 
Msando.Heshima Mbele!How are you?

Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.

Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.

Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.

Aluta Continua.
Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.
That's my girl!!!

safi sana Regia kwa kukubali kuna hypocrisy ya hali ya juu kwa hao tunaowaita wawakilishi wa wananchi na pia mfumo wetu bado ni wa demokrasia kamili

nasema hivi kwasababu unashangaa unakatazwa ku-share info za kipato lakini unatakiwa kuorodhesha mali ulizonazo kama kiongozi, how can one rationalize income na outcome??

anyway nimependa jibu lako
 
shukrani sana Mh. Regia,tumekusoma vyema bila chenga. lakini sababu kubwa ya wabunge kufundwa wasitoe siri za kipato ni tofauti kubwa iliopo kati ya kipato chao na kipato cha mtumishi wa kawaida(mwenye bachelor).mshahara wa mbunge mmoja kwa mwezi (weka kando maposho) unaweza kuwalipa watumishi wenye shahada (TGS D1) wa kutosha tu (sijui idadi kamili). kwa mantiki hiyo lazima bunge litumie njia ya ziada kuficha hiyo siri kwa sababu wanajua wananchi wakijua waziwazi lazima watapata moto.inauma sana maana pesa wanayolipwa ni kodi ya mtanzania halafu wanamficha mtanzania asijue ni kiasi gani cha pesa yake inatumika kumlipa mbunge.kweli mtanzania anafanywa punda,mbeba mizigo kwa manufaa ya mwenye punda ambae pia humpanda punda.kibaya zaidi na mtanzania amekubali kua punda
 
Basi kwa kuwa Zitto ni mzoefu atawasaidia wenzake katika kutuletea huo mchanganuo wa posho na kadhalika nyingine
 
Back
Top Bottom