Mheshimiwa Regia,
Nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri. Sikutaka kuingia kwa kina baada ya maelezo yako ya mwanzo kwa sababu kuu moja, bado Zitto na Mnyika hwajajibu chochote ili tujue mawazo au maoni yao. Nimekuwa mgumu kuamini haraka haraka kwamba na wao wanaweza kuwa na mawazo au msimamo kama wako.
Kwa nini nimesubiri? Zitto ninayemjua mimi amekuwa mzoefu wa kufukuzwa na kuwajibishwa kila alipopita. Zitto alifukuzwa O'level akafukuzwa A'level na akafukuzwa Chuo Kikuu. Zitto alifukizwa/simamishwa Bungeni. Kufukuzwa kote huko ilikuwa ni kwa sababu alikuwa anasema ukweli na kupinga waziwazi yale aliyoyaamini. Bado nasubiri nione katika hili inakuwaje. Inawezekana sasa hivi approach yake ni tofauti lakini bado nitasubiri nilishuhudie hilo au alitolee maelezo. Ukimya wake kwa wengine unaweza ukaonekana kama ni woga au amebadilika. Sitakuwa mwepesi kuamini hivyo mpaka mwenyewe aseme au ukimya wake umaanishe hivyo.
Kuhus Mnyika na yeye natarajia atasema neno. Endapo hatasema ataelezea kwa nin hajasema neno katika hili. Namfahamu na wengi humu ndani wamemuona ni mtu wa aina gani. Suala la Kanuni kumbana sidhani kama linamsumbua sana. Angekuwa anajali kanuni na sheria asingenipokea mimi na Zitto tulipofukuzwa chuo mwaka 2003 na kutuhifadhi chumbani kwake almost wiki tatu. Angefuata kanuni na By Laws za Chuo. Pia asingeniafirisha usiku kutoka Morogoro mpaka Dar kukimbilia Mgomo mwaka 2004 huku akiwa kiongozi wa TYVA na YUNA kwani alivunja kanuni nyingi tu. Mbona hakuogopa kipindi hicho? Kwa nini aogope sasa hivi?
Tukirudi kwako wakati nasubiri bila kuchoka kuwasikia Zitto na Mnyika, je taarifa uliyoitoa kwa wananchi wako wa kilombero ilikuwa ni kwenye hadhara au uliwapa mmoja mmoja? Uliwatangazia wakati wa mchana kwenye mwanga au usiku? Najaribu kuangalia tofauti ya eneo la kutolea taarifa hiyo i.e kwenye jukwaa la siasa kwa maandishi na kwenye mkutano wa hadhara kwa maneno.
Kwenye JF hakuna ushahidi wowote ambao unaweza kupokelewa mahakamani au kwenye kamati ya maadili kuonyesha na kuthibitisha kwamba ni wewe umesema utakachosema. Ni nani atathibitisha ni wewe? Je kama nimechukua picha yako, nikaingia nayo humu ndani pamoja na jina lako nani atajua?? nani atapinga?? Mods watathibitisha vipi ni wewe?? Lakini bado siamini kwamba kipato cha Mbunge ni siri. Nikipata muda nitasoma kanuni za Bunge.
Ila ukisimama hadharani kila mtu anakuona, mashahidi watajitokeza, usalama wa taifa watakuona, waandishi watakupiga picha uthibitisho utakuwepo kwamba ni wewe umesema mbunge analipwa kiasi gani. Hapo unatakiwa uwe muoga zaidi.
Lakini, kwa sababu ninajua tutaonana au tutazungumza nje ya hapa naamini nitapata ufafanuzi zaidi. nitakuomba kama una nakala ya Kanuni za Bunge recent unitumie kwa email ili nizipitie na nitakuwa mshauri wako kuhusu masuala yote ya kanuni. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hazikufungi bila sababu.
Kwa sasa ninasubiri bila kuchoka kumsikia Zitto na Mnyika. Ukiwapata wafikishie salamu kwamba tunawasubiri humu.
Kila la kheri Mheshimiwa.
Kipengele namba sita;Hutambui kuwa ukiwa kwenye public office you are accountable to the public?Sijui ni kivipi unafananisha ufahamu wa mume ama mke kuhusiana na mishahara yao vs wananchi kujua ni kiasi gani wanawalipa nyie kama viongozi wao?Ama ubunge ni private sector?
Tanzania naisikitikia sana,juzi tu waziri mkuu ameenda kanisani kuhutubia kuwa ufisadi upo hadi kanisani as if kanisa lina uhusiano wowote ule na serikali,ama ufisadi wa serikalini ndiyo ufisadi wa kanisani!Yani huyo ni waziri mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu wa serikali...!Badala ya kuja na data za kuwa wamefanya nini kuumaliza ufisadi ie hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa dhidi ya ufisadi na mafisadi wa Taifa,yeye anaenda kulia kulia kanisani...Mkuu nimetoa mfano mdogo tu kwamba kama kwenye ngazi ndogo ya familia tunashindwa kuwa wa wazi kwenye masuala ya fedha tena kwa familia yako sembuse kwa wananchi?Wenzetu nchi zilizoendelea wana uwzi mkubwa katika ngazi zote?charity begins at home.Ukinisoam vizuri utanielewa binafsi napinga usiri huu ndio maana wananchi wa Kilombero wanafahamu na hata mdada anayenisaidia kazi nyumbani anafahamu kama Mbunge ninalipwaje na hata kabla sijawa Mbunge alifahamu pia.Mimi sijasema hatulipwi pesa nyingi,nenda kasome comment yangu ya kwanza.N kweli Wabunge wanalipwa vizuri na ndio maana kila mtu anataka kuwa Mbunge hata kwa njia zilizo haramu.Ubunge tanzania ni kitega uchumi.Kuna fursa nyingi sana kwenye Ubunge,hivi hamshangai mtu miaka nenda rudi Mbunge na wala hawataki kaucha mpaka mfumo uwateme?
Ndugu zangu wanaJF. Salaam.
Nimesoma kila mchango kwenye sredi hii kwakuwa sredi hii inanihusu moja kwa moja.Ninaelewa hoja zenu na nina washukuru wote kabisa mlionielewa na msionielewa.Kuna mambo kadhaa naomba niyaweke sawa.
1.Kuna watu hapa baada ya kusoma post niliyorusha mmelaumu kwa kusema ninakwepa kusema ukweli.Kundi hili nadhani halikunielewa nilichosema,nimesema wazi kabisa nje ya jukwaa hili naweza kusema na nikampa fursa mrusha sredi anitafute kwa njia nyingine.Alberto ana access namimi kwa kiasi kikubwa tu angeweza kunipata na ningempa mchanganuo wote including access ya kiwango cha juu cha mkopo kwa Mbunge kwenye benk.
2. Kuna wengine wamesema nitumie au ningetumia ID ya siri na kuna wengine wamesema eti kutokuwa na ID nyingine ni danaganya toto lakini ukweli ni kwamba sina ID nyingine kwasababu zifuatazo ninaamini kabisa nikiwa na ID nyingine na nikawa na post sredi mbalimbali hapa ndani ya wiki mbili tu nitakuwa nimeshajulikana.Nilipokuwa natumia jina la siri enzi hizo kama Gender Sensitive kuna watu wengi tu walikuwa wameshafahamu GS ni nani.The problem niko muwazi sana na siwezi kujificha wala kupretend hivyo nitajisumbua tu kuwa na ID za siri,sioni sababu.Baada ya kuwa Mbunge kuna baadhi ya watu walinishauri niwe na hayo maID ya siri lakini nikaona nitakuwa mtumwa tu,kwnini nijifiche?namdanganya nani?naogopa nini?
3.Kuna watu hapa wanasema kuwa naogopa kuwajibishwa na Kamati ya Maadili inakuwaje naogopa kusemwa tu?ndugu zangu mnachukulia kuwa hili suala ni dogo sana,sio dogo kama mnavyodhani.Ninachokataa hapa nikuvunja kanuni kwenye forum kama hii.Nimesema wazi kuwa nje ya hapa sitaficha.
4.Kuna kitu nimejifunza hapa, kuna watu wanashangaa mimi kuogopa kuwajibishwa na kamati ya maadili lakini wengi wao wako na majina ya siri,kwanini mnajificha,manogopa nini?si angalau mimi niko na jina langu halisi na ninafahamu fika kwamba kila ninapopost kitu sio wote watakao kipokea positively,ninafahamu fika nitakumbana na changamoto mbalimbali but altleast siziogopi na ninaziface.Jamani tafakarini kwa kina.
5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje.
6. Napenda kufahamu hivi humu ni wangapi wake au waume zao au watoto wao au wazazi wenu wanafahamu mishahara yao?
7. Kuna watu humu wametoa mfano niliposimamia msimamo wangu kuhusu tofauti ya PHD na First Degrees,Bungeni ninalindwa na Kanuni za Bunge,ninaweza kukubali au kukataa mwongozo wa Spika kama nilichokisema ndicho ninachokiamini na ndivyo ilivyokuwa.Hapa siwezi kuikwepa Kanuni ya kutotoa siri za Bunge.
Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira
Kipengele namba sita;Hutambui kuwa ukiwa kwenye public office you are accountable to the public?Sijui ni kivipi unafananisha ufahamu wa mume ama mke kuhusiana na mishahara yao vs wananchi kujua ni kiasi gani wanawalipa nyie kama viongozi wao?Ama ubunge ni private sector?
Mkuu nimetoa mfano mdogo tu kwamba kama kwenye ngazi ndogo ya familia tunashindwa kuwa wa wazi kwenye masuala ya fedha tena kwa familia yako sembuse kwa wananchi?Wenzetu nchi zilizoendelea wana uwzi mkubwa katika ngazi zote?charity begins at home.Ukinisoam vizuri utanielewa binafsi napinga usiri huu ndio maana wananchi wa Kilombero wanafahamu na hata mdada anayenisaidia kazi nyumbani anafahamu kama Mbunge ninalipwaje na hata kabla sijawa Mbunge alifahamu pia.Mimi sijasema hatulipwi pesa nyingi,nenda kasome comment yangu ya kwanza.N kweli Wabunge wanalipwa vizuri na ndio maana kila mtu anataka kuwa Mbunge hata kwa njia zilizo haramu.Ubunge tanzania ni kitega uchumi.Kuna fursa nyingi sana kwenye Ubunge,hivi hamshangai mtu miaka nenda rudi Mbunge na wala hawataki kaucha mpaka mfumo uwateme?
Tanzania naisikitikia sana,juzi tu waziri mkuu ameenda kanisani kuhutubia kuwa ufisadi upo hadi kanisani as if kanisa lina uhusiano wowote ule na serikali,ama ufisadi wa serikalini ndiyo ufisadi wa kanisani!Yani huyo ni waziri mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu wa serikali...!Badala ya kuja na data za kuwa wamefanya nini kuumaliza ufisadi ie hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa dhidi ya ufisadi na mafisadi wa Taifa,yeye anaenda kulia kulia kanisani...
Tuna tatizo kubwa sana watanzania....Ukitizama kiundani,Pinda ni kama anasema kila mtu ni fisadi kwa kutolea mfano kuwa ufisadi humo hadi kanisani nk,ni kama kuwaambia hao viongozi wa dini "mnapiga kelele za nini kuhusu ufisadi na wakati kuna ufisadi kanisani?"na inaonyesha wao kina Pinda hawaoni kama ufisadi upo ama kama ni tatizo pale inapokuaja kwenye maendeleo ya Taifa letu....
Pia hiyo haijustify kutokuwachukulia hatua mafisadi wa mali za umma...Same applies to this issue,ofisi mnazoshikilia ni public ones,mko accountable to the public,kwa hiyo kutoa kisingizio eti kwasababu familia hazielezani mishahara ie btn mke na mume ama mzazi na mwanawe,basi then ni sawa kwa wananchi kutoelezwa mishahara ya viongozi wao,hapo sikubaliani.
Kama kweli viongozi especially nyie wa upinzani mna uchungu kiukweli na Taifa hili,basi unafahamu hatua mnazoweza kuchukua ili kuwaondolea wananchi huu mzigo!Kumbuka wananchi ndiyo wamewaajiri,yani mwananchi ndiyo mwajiri wako na wewe kina Zitto na wengineo ni waajiriwa wa wananchi!Kama ilivyo kwa waziri mkuu ambaye alitakiwa aelewe kuwa kuna hatua za kuwachuklia mafisadi na si kusema eti ufisadi humo hadi makanisani,sasa dini na serikali wapi na wapi?Na hata kama upo kanisani kwani ina maana viongozi wa dini si wananchi wenye haki ya kuuliza kuhusu ufisadi wa serikali?Ni sawa na kuwambia mwananchi kuwa hata humo uraiani kuna ufisadi ama wizi na kwahivyo wanaosimamia mali za serikali nao wanaweza kuiba!hata humo kwenye institutions kama dini,kuna hatua za kuwachukulia mafisadi....Hata kwenye private institutions nk!
Na kwa upande wenu CDM,mnatakiwa muonyeshe utofauti kati yenu na ccm,mnapogombana just because kuna mwenye kuonyesha mapenzi ya kweli kwa wananchi(ie waliochukia hatua ya mbunge wa Arusha kuhusu 90 mil),then mnatufanya tujiulize maswali mengi sana.
Ofisi ya umma si mchezo ndugu zanguni,kama ni kweli mna nia ya kuwakomboa watanzania,ni lazima kwanza muanze kwa kubadili system na si kupiga kelele halafu mkishaingia ndani mnaona baadhi ya mambo kama haya ni sawa kwa vigezo vya "Semina elekezi"
Ama mishahara mnayolipwa na wananchi mnaona ni issue binafsi?
Kweli linapofika suala la maslahi maji na mafuta vimechangamana .
, hiyo sheria ya kumhukumu mtu kutaja mshahara wake iko kwenye katiba ipi hapa MSANDO nisaidie
ila mimi nimejaribu kumchimba mbunge mmoja ameniambia kwa mwezi wanapata 12 . ikijumuisha mshahara wake , mshahara wa driver , mshahara wa msaidizi , mafuta lita 420 @ 2,500 , matengenezo ya gari na nyumba .
na kila kikao wanachohudhuria wanalipwa posho ya 150,000 kwa siku .
Regia wanawake sisi ni waungwana na wakweli na kwa sasa tunazidi kukimbilia sifa nyingine ya kujiamini ukifanya matendo yanayofanana na wanafiki haipendezi .
Dr Slaa mara zote alikuwa akitangaza mshara wake tokea wabunge walipokuwa wakilipwa 2.1 mpaka ilipofika 6 m na hatukuwahi kusikia akihukumiwa kwa kuwa hakuwa akisema wabunge wanalipwa bali alikuwa akisema mimi Slaa ninalipwa
Dada yangu mpenzi ni mapema mno kuacha kusimamia maslahi ya wananchi na kusimamia maslahi ya wabunge
Nimelazimika kujiuliza, je ni vipi sheria au kanuni inaweza kutungwa kukuzuia kusema unalipwa au unapokea nini kama Mbunge? Kanuni hii inasemaje? Mpaka sasa bado sijaipata hiyo kanuni inayosema 'ni marufuku kwa Mbunge kumwambia mtu yeyote kiasi cha mshahara anachokipokea' au 'ni marufuku kwa Mbunge kutaja hadharani kiasi cha fedha anachopokea kwa nafasi yake ya ubunge'. Bado sijakiona kipengele au kifungu hicho.
Mh. Mbunge yeyote aliyemo humu jamvini au mtendaji wa bunge yeyote naomba anipatie kanuni, kifungu au kipengele hicho. Vinginevyo bado nasubiri kama Waheshimiwa zitto na mnyika watachangia hii hoja. Au kama kuna Mbunge mwingine anayeweza kutujuza afanye hivyo.