Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,505
- 113,620
Wanabodi
Kupitia kipindi changu kipya cha KMT, kinachorushwa hewani na Channel Ten, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku, namarudio Jumatano Saa 9:30 alasiri, Jumapili hii ni Katibu Mkuu wa Chadema, JJ. Mnyika, kuunguruma.
Katika kipindi hicho, JJ. Mnyika atathibitisha jinsi maridhiano na CCM yalivyo isaidia Chadema, ambapo mwanzo waligoma kuutambua uchaguzi na kuyatambua matokeo, lakini kupitia maridhiano sasa Chadema inautambua uchaguzi, inayatambua matokeo ya uchaguzi, na kumtambua Mbunge wake mmoja tuu, Aida Kenani.
Pia JJ Mnyika atajibu hoja mbalimbali za mwandishi Pasco Mayalla, zikiwemo hoja kuhusu wale wabunge wake 19, likiwemo jibu la swali ”Kwanini Chadema mpaka leo haijaripoti polisi kuhusu jinai ya kughushi ya wabunge hao 19?”.
Jiunge nami hiyo saa 3:00, kipindi hiki ni recorded, na kwa vile Channel Ten haina live streaming kwa vipindi vya kawaida, mimi nitakuleta live stream kupitia Channel yangu, kisha nitatuma link jf ili hata wasio na TV, waweze kufuatilia kupitia live stream na mitandao ya kijamii.
Kipindi kilichopita nilizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema.
Vipindi vijavyo, kwa Chadema, nitamtafuta Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,kwa ACT Wazalendo ,nitamtafuta Zitto na OMO, na kwa CCM Makonda atatosha.
Usikose!.
Paskali