ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Msando.Heshima Mbele!How are you?
Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.
Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.
Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.
Aluta Continua.
Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.
Regia,
Kwanza hongera kwa kujitokeza hapa. Umekuwa tofauti na wale wabunge wanaotumia blackberry na kuingia JF kila nusu saa lakini wameikacha thread hii muhimu.
Jibu lako linaonyesha ujasiri kwa sababu ni wazi kuwa na wewe utaingia kwenye kundi la kulaumiwa kama Mh. Lema. Anyway, hiyo ndio kazi ya kutumikia wananchi.
Katika jibu ulilitoa umedhihirisha kuwa hata wewe binafsi hauko tayari kufanya bidii ya kuhakikisha Mh. Diwani Msando anapata jibu la swali lake.
Sababu uliyotoa ya semina elekezi haina uzito, kwa sababu nchi inaendeshwa kwa sheria na sio kwa semina elekezi. Kama kuna sheria inayokukataza kufanya hivyo sote tutaiheshimu lakini sio wewe, wabunge wenzako na spika ku-connive katika kuhujumu wananchi.
Kumbuka Regia, uliposema uelewa wa watu wenye PhD Tanzania ni sawa na ule wa bachelor, spika alikupa "semina elekezi" kuwa ubadilishe msema wako; nilipenda sana jibu lako kwa spika - ulimwambia "mwa muono wangu mimi hivyo ndivyo ilivyo interms of thinking capacity". Kama uliweza kuikataa "semina elekezi" hadharani, ulishindwa vipi kuikataa semina elekezi za siri za Ubungo plaza?
Sababu nyingine uliyotoa kuwa huna ID nyingine nayo ni "danganya toto".ID za JF hazinunuliwi. Iwapo unaamini kuwa mh. Diwani anastahili kupata jibu la swali hili, unaweza kufungua ID nyingine au unaweza kumtumia PM.
Nakuomba umtumie Mh. Diwani PM ili yeye abebe barden ya kutujulisha wana JF wengine bila kusema kuwa wewe ndiye uliyemwambia, ili wabunge wanzako wasikulaumu, kwa sababu apparentlly lawama zao ni muhimu kuliko kulaumiwa na wananchi!
Kwa mara nyingine asante sana, tuendelee kuwatumikia watanzania.