mhalisi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 1,181
- 320
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.
Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".
Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?
Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.
Kikwete humuwezi.
unamaanisha nini? au nae ataondolewa bungeni kama Lema kwa kupitia rufaa ya Hawa Nghubi?