Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Jamaa dhaifu sana huyu ona ahadi zake - alitoa akiwa wapi......

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Mbona hujaandika ahadi za mhishimiwa mnyika alipoahidi ubungo kuhusu kero kadhaa ambazo mpaka sasa hajazitekeleza ! Ama nyani haoni kunnndule!
 
hehehe kwa wewe mchangiaji ukichangia kimnyika nyika na wewe unakula ban ya mwaka mmoja/au miezi mitatu. Spika/mods na bunge la JF naomba kutoa hoja
 
Huyo mtoto anajifunza kuwa mkweli kwa nafsi yake na kwa jamii! Kama kiongozi ni dhaifu na hata hao watoto wanaliona hilo wazi, haisaidii kimalezi kuendelea kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Hebu jaribu kufanya utafiti kidogo tu hapo mtaani kwako kwa kuwauliza watoto kama waliisikia kauli ya Mnyika na wana maoni gani - naamini watakushangaza sana mkuu!

Pamoja na yote Kindafu, imetuuma sana sisi tunaoamini kuwa Kiongozi yeyote huchaguliwa na Mungu, hivyo kumdhihaki na kumvunjia heshma ni sawa na kudhihaki/kuvunjia heshma wale wote anaowaongoza including wewe.
 
Nawaambia hivi, mnazidi kumpa kichwa, kijana aliyepata madaraka madogo tu ya kuwakilisha wananchi bungeni, akashindwa kuchangia hoja ya bajeti akaanza kututukana wengi sana, wabunge wote, na wana ccm wote na wananchi wote.

Huyu hatumuwachi, tutahakikisha anapewa adabu ili iwe fundisho kwa wengine.

Utampa adhabu gani? yule mchawi wenu wa Mwembechai kesha kufa. Mnyika yupo fresh na leo kaingia mjengoni kama kawa JK mwenyewe ni dhaifu tu, na pale alipo ni kwa kuiba na kuchakachua
 
Nadhani imefika wakati sasa Rais inabidi aoneshe udikteta kama wa Mkapa , enzi zile midono ya watu kama hawa ilifyata kama mikia ! Rais tunaomba uwashikishe adabu watu kama hawa ambao hawana nidhamu kabisa, hata iweje huwezi kuwa na kiburi na dharau kiasi hicho kwa kiongozi wako wa nchi! Rais tunaomba huyu aadabishwe ! na iwe fundisho kwa wengine !

umekwishaambiwa baba Riz1 ni DHAIFU, hayo unayomuomba ayafanye hawezi kuyafanya.
 
Pamoja na yote Kindafu, imetuuma sana sisi tunaoamini kuwa Kiongozi yeyote huchaguliwa na Mungu, hivyo kumdhihaki na kumvunjia heshma ni sawa na kudhihaki/kuvunjia heshma wale wote anaowaongoza including wewe.

Unafikiri hata povu likikutoka mpaka asubuhi neno DHAIFU ndio litafutika?
 
ZOmba sijaona kosa la Mnyika,unajua Watanganyika tumezoea kupewa sifa zisizo zetu na kufurahi kwelikweli lakini akija mtu akikwambia ukweli kuhusu udhaifu unachukia kwelikweli sasa ifike wakati tuwe tayari kupewa ukweli na kuuchukua na kufanyia kazi.Tusikamiane bila sababu kila mtanzania ana haki ya kuongea na kufanya anachotaka ilihali havunji sheria ya nchi.Hivyo Mnyika kama kijana wa leo ana haki ya kusema kile anachokiona kuwa kweli mradi havunji sheria.Kuambiwa dhaifu siyo kutukana ila muambiwa ajiangalie wapi yuko dhaifu achukue hatua stahiki.Kumwambia Myika utaona hapo ndipo mnapokosea.Tukubali katika kutokukubaliana. vijana wa miaka ya sitini siyo sawa na vijana wa miaka hii.Wanajua ukweli na wanaupigania,tuwaunge mkono kwa maslahi ya taifa letu,watoto na wajukuu zetu.Tuache lugha za kutishana.
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Ni DHAIFU tuu hata ufanye nini?
 
Mnyika ameharibia watoto wetu wanaofuatilia kwa makini Bunge kwa lengo la kujifunza jinsi wawakilishi wetu wanavyoongea na kuijadili bajeti.

Pamoja na kufurahia bunge, watoto pia wanajifunza jinsi watakavyoongea wakikua iwapo wataamua kuingia kwenye siasa.

Walichojifunza kwa huyu mpuuzi Mnyika ni jinsi ya kuwatukana baba zao hadharani.

Aibu sana, nimewapiga marufuku wanangu kuangalia kipindi cha Bunge ....until further notice.

hapo kwenye blue, na wewe ni dhaifu tu! huwezi kumzuia mtoto kuangalia Bunge kwa sababu za kipuuzi ulizoziweka hapa
 
Mnyika ameharibia watoto wetu wanaofuatilia kwa makini Bunge kwa lengo la kujifunza jinsi wawakilishi wetu wanavyoongea na kuijadili bajeti.

Pamoja na kufurahia bunge, watoto pia wanajifunza jinsi watakavyoongea wakikua iwapo wataamua kuingia kwenye siasa.

Walichojifunza kwa huyu mpuuzi Mnyika ni jinsi ya kuwatukana baba zao hadharani.

Aibu sana, nimewapiga marufuku wanangu kuangalia kipindi cha Bunge ....until further notice.

Kuwanyima watoto wasiangalie bunge ni Udhaifu mkubwa sana tena udikteta ambao unaofanywa na UAMSHO
 
magamba mmeshikwa pabaya safari hii wananchi wamewashtukia wamechoka kusubiria maaendeleo miaka 50 ya uhuru.
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.
Kaka mimi nakuona wote hawajakuelewa kama mimi, unachotaka tuseme hapa ni kwamba, Kikwete na Raisi aliyetangulia wote ni WADHAIFU, mjadala sasa unaweza kufungwa. Ila nakukumbushia pia Dr Hosea wa Takukuru alisema kuwa raisi anaogopa wala Rushwa, sasa naona huyu kijana kaamua tu call spade a spade SAFI SANA KIJANA MNYIKa
 
Mbona hujaandika ahadi za mhishimiwa mnyika alipoahidi ubungo kuhusu kero kadhaa ambazo mpaka sasa hajazitekeleza ! Ama nyani haoni kunnndule!

Wee Kima mimi sikai Ubungo ila ni Mtanzania....nadhani umenisoma wewe goi goi na dhaifu
 
Ukweli utabaki kuwa ni ukweli tu hata kama ni ngumu kumeza,taratibu mtazoea kuambiwa ukweli na sio hadithi za "anaangushwa na watendaji wake"
 
Back
Top Bottom