Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Wewe neno UDHAIFU linakukera nini kwani? Mtu anayepata PASS darasani utesema ni STRONG au WEAK? Hivi unaijua SWOT analysis? Ushawahi kuwa katika interview ya kazi na ukaulizwa weakness zako ni zipi? WEAKNESS ndio UDHAIFU kama hujui! Na ni neno la kawaida sana........Hata Museveni ni dhaifu kwa kudhani familia yake tu ndio ina uwezo wa kutawala. Kila binadamu (akiwemo Mnyika) ANA UDHAIFU WAKE.......sasa labda Kikwete ni jini na si binadamu basi atakuwa hana udhaifu!

Hatokuelewa unaonge na Huyu ZOMBA ambaye shule imempitia pembeni. We angalia hata kauli zake. Usipoteze muda.
 
SISIEM mshazoea kupigiwa makofi kwenye kila kitu ndio maana mnapenda kusifiwa hata kama ni wadhaifu..KIMSINGI KIKWETE NI MDHAIFU TENA SANA TUU
 
Mnyika ameharibia watoto wetu wanaofuatilia kwa makini Bunge kwa lengo la kujifunza jinsi wawakilishi wetu wanavyoongea na kuijadili bajeti.

Pamoja na kufurahia bunge, watoto pia wanajifunza jinsi watakavyoongea wakikua iwapo wataamua kuingia kwenye siasa.

Walichojifunza kwa huyu mpuuzi Mnyika ni jinsi ya kuwatukana baba zao hadharani.

Aibu sana, nimewapiga marufuku wanangu kuangalia kipindi cha Bunge ....until further notice.

sasa watoto wako kupitia mnyika wamejua jk ni dhaifu kwani wewe hukuweza kumwambia kwa hiyo acha wenye ujasiri wakufundisha wanao yanayo endelea nchini wawambie.

Usipowafundisha wanao, jirani zako watawafundisha.
 
Nadhani imefika wakati sasa Rais inabidi aoneshe udikteta kama wa Mkapa , enzi zile midono ya watu kama hawa ilifyata kama mikia ! Rais tunaomba uwashikishe adabu watu kama hawa ambao hawana nidhamu kabisa, hata iweje huwezi kuwa na kiburi na dharau kiasi hicho kwa kiongozi wako wa nchi! Rais tunaomba huyu aadabishwe ! na iwe fundisho kwa wengine !

Enzi hizo zimeshapita, huwezi kuzirudisha, nyoka lazima aitwe nyoka si vinginevyo
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Alichokosea Mnyika ni kusema mfalme yu uchi hadharani wakati watu wazima wanaona mfalme kavaa vazi lisiloonekana,lakini in reality huo ndio ukweli,km ccm mmeshindwa kumuambia acheni wenye uwezo wa kufanya hivyo wafanye.bravo kijana cuz umefungua uwanja mpya wa kuelezana ukweli pale inapobidi.
 
du ukija kwa uzinzi nyinyimu hapo si mmeoza mbona dhaifu aliwahi kumfungulia demu aliyezaa nae dodoma grosary, mwigulu oh mzee wa miongozo
 
Watu Kama wewe ni wakupeleka Cameroon mkavunishwe Chai na Migambo wakiwasimamia kwa nyuma.

Soma hapa basi
MNYIKA ANGEKUWA DHAIFU ZAIDI KAMA ANGEFUTA KAULI YAKE BUNGENI.

1. Kama udhaifu ni kuto kujua kwa nini wananchi wako ni maskini
wakati wako nchi tajiri. Mnyika yuko sahihi.

2. Kama huwezi kumuwajibisha au kuona madudu ya katibu mkuu au katibu
kiongozi mpaka bunge lishikilie bango na kushinikiza wang'oke ndio
uzinduke kufanya maamuzi basi mnyika yuko sahihi.

3. Kama kweli watu wamelibia taifa kupitia dili za magumashi halafu
una watangazia warejeshe fedha ili wasichukuliwe hatua na wakati
huohuo vibaka wanauwawa au kuchomwa moto kwa kuiba kuku na simu basi
ni dhahiri kuna udhaifu wa kiungozi. Mnyika yuko sahihi.

4. Kama ndege inaingia kwenye anga ya nchi yako na kubeba wanyama
kupeleka Arabuni bila hatua zozote kuchukuliwa ni dhahiri kuna udhaifu
wa kimfumo ulio kubuhu serikalini. Mnyika yuko sahihi.

5. Kama rais anafunga safari kwenda kuomba misaada na wakati huohuo
misaada anayopewa hailingani thamani na raslimali zinazo vunwa kwenye
nchi yake basi Mnyika yuko sahihi.

6. Kama rais anadiriki kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya
trilion 9 huku akijua kuwa hazitekelezeki ni hadaa kwa wananchi, chama
na serikali. Mnyika yuko sahihi.

7. Kama taasisi ya Ikulu na mfumo wake wa utawala umehusika kuingilia
maamuzi ya mhimili wa haki kwa kutoa hukumu ya upendeleo ili kumkomoa
au kumnyang'anya mbunge wadhifa kama jinsi ilivyo lalamikiwa. Mnyika
yuko sahihi.

8. Kama serikali inatenga 70% kwa matumizi kwenye bajeti yake na 30%
kwenye maendeleo. Ni dhahiri kuwa ni aina ya serikali dhaifu yenye
viongozi wavivu wa kufikiri.

Kama hivyo ndivyo, nasimama na kijana mwenzangu kwa ukakamavu na
kupaza sauti yenye mwale mkali. Namuunga mkono Mnyika.
 
Awaue kama kina Kombe?au wafungwe kama wale wanamuziki? Ulimwengu huu ni mwingine, usimponze amfuate Taylor bure wakati wewe utakuwa unakula maisha kwa mafanikio yatakayo letwa na Chadema baada ya 2015

Babu yenu Nyerere alokuwa akiua waziwazi kina marehemu Hanga mbona hakuwahi kuuliwa? na matokeo yake amekuja kuuliwa na ambao aliwaamini sana tunavosikia kutoka kwa kina vicent nyerere! kwani adabu ni kuua tu ! kwalipi kubwa mpaka auliwe mnyika? afungwe tu kumshikisha adabu kwa kumdhalilisha kiongozi wa nchi!
 
Na mimi pia nasema RAISI KIKWETE NI DHAIFU TENA SANA!!! haya nasubiri hiyo vita.. kawatishie mafisadi wenzio wewe..
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Rais ni binadamu kama wengine, so anaweza kuwa strong au dhaifu. Na kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa, ana uwezo wa kukosolewa vilevile.

Kikwete kakosolewa hajatukanwa.
 
I am very sorry kwa watu wanaoumia kwa kikwete kuitwa legelege mi nafikiri pia nchi hii imemshinda hajui chakufanya na sasa ana iongoza kwa maelekezo toka kwa wapuuzi fulani fulani. kwa sababu kama huwezi kutoa maamuzi kwenye matatizo nyeti na makubwa ndani ya nchi yako, badala yake unaenda kutalii nje, kama hata mpango wa miaka mitano aliouandaa yeye mwenyewe na mawaziri wake na ukapata sifa kedekede bunge likaupitisha. leo mwaka mmoja tu baaadae anashindwa kusimamia budget i reflect mpango ambao hata kuna baadhi wanadiriki kuuita mpango wa kikwete. mwingine kasema eti mnyika aheshimu watu wazima, hata kama ni watu nusu , wazee, wa baba, wa mama na wengine unao wafahamu wewe kama niwapuuzi,legelege, au dhaifu ni msema kwelitu ndie atakae simama na kusema bana wewe ni mpuuzi legelege au dhaifu. Big up mnyika endeleza mapambano ya ukombozi mpaka kieleweke
 
Masikini we, kwa bahati mbaya nasikitika kuwa uwezo wako wa kufikiri ni dhaifu kama naibu spika, kusema Rais Kikwete ni dhaifu sio kutangaza vita, naibu spika alitakiwa kumpa nafasi Mh. Mnyika afafanue kwanza ni ndhaifu kwa lipi? pili mwaka 2010 hatukuchagua malaika kuiongoza Tanzania bali tulimchagua binadamu aitwae Jakaya Mrisho Kikwete kutuongoza hivyo binadamu wote tu dhaifu akiwemo Rais Kikwete hivyo, sio sahihi kutuaminisha watanzania kuwa Rais Kikwete hawezi kuwa dhaifu.
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Zomba naomba nitofautiane na wewe kwenye hili!!! JK toka ameingia zilikuwako dalili lukuki tu za kudhihirisha udhaifu wake! Yapo, meeingi tu, katika hayo naomba niongelee moja tu! JK ameshindwa kuongoza taasisi ya UwT. Hii ni taasisi nyeti kwake kama rais, ndiyo inayomuoongeza kwenye mambo meeenigi sana katika utendaji wake.

Kwa mfumo wetu mbaya, wengi tu wamejitahidi kutumia vibaya taasisi hii kujinufaisha. Sasa JK ameshindwa kuwa taasisi iliyo imara na moja kumsaidia, UwT imegawanyika na ndo maana mambo ya serikali yake, ikiwamo madudu, tunayapata live mitaani!! Kwa hiyo angeweza kutumia taasisi hii kuendesha vita binafsi na Mnyika, nasikitika kukwambia hawezi maana haiko "coherent" iko kama muunganiko wa maji na mafuta!!

Mnyika kamlima JK bungeni si kwa vita binafsi, ila ka-ainisha weakness zake! Weakness si tusi!! So Mnyika was and still is right!! Nyie endeleeni tu kucheza ngoma za CDM, najua mtashtuka mmekuwa chama cha upinzani, ndo akili zitarudi!!
 
Babu yenu Nyerere alokuwa akiua waziwazi kina marehemu Hanga mbona hakuwahi kuuliwa? na matokeo yake amekuja kuuliwa na ambao aliwaamini sana tunavosikia kutoka kwa kina vicent nyerere! kwani adabu ni kuua tu ! kwalipi kubwa mpaka auliwe mnyika? afungwe tu kumshikisha adabu kwa kumdhalilisha kiongozi wa nchi!
hee, hivi kusema rais ni dhaifu ni kudhalilisha?so ukisema ukweli unaouma, umedhalilisha...kama unataka kujua kikwete ni dhaifu angalia hata baraza lake la mawaziri, alilibadilisha lakini kwa malalamiko ya ooh, kuna watendaji ilibidi wawajibike nk, huo ni udhaifu na kukosa maamuzi...
 
Watu Kama wewe ni wakupeleka Cameroon mkavunishwe Chai na Migambo wakiwasimamia kwa nyuma.

Soma hapa basi
MNYIKA ANGEKUWA DHAIFU ZAIDI KAMA ANGEFUTA KAULI YAKE BUNGENI.

1. Kama udhaifu ni kuto kujua kwa nini wananchi wako ni maskini
wakati wako nchi tajiri. Mnyika yuko sahihi.

2. Kama huwezi kumuwajibisha au kuona madudu ya katibu mkuu au katibu
kiongozi mpaka bunge lishikilie bango na kushinikiza wang'oke ndio
uzinduke kufanya maamuzi basi mnyika yuko sahihi.

3. Kama kweli watu wamelibia taifa kupitia dili za magumashi halafu
una watangazia warejeshe fedha ili wasichukuliwe hatua na wakati
huohuo vibaka wanauwawa au kuchomwa moto kwa kuiba kuku na simu basi
ni dhahiri kuna udhaifu wa kiungozi. Mnyika yuko sahihi.

4. Kama ndege inaingia kwenye anga ya nchi yako na kubeba wanyama
kupeleka Arabuni bila hatua zozote kuchukuliwa ni dhahiri kuna udhaifu
wa kimfumo ulio kubuhu serikalini. Mnyika yuko sahihi.

5. Kama rais anafunga safari kwenda kuomba misaada na wakati huohuo
misaada anayopewa hailingani thamani na raslimali zinazo vunwa kwenye
nchi yake basi Mnyika yuko sahihi.

6. Kama rais anadiriki kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya
trilion 9 huku akijua kuwa hazitekelezeki ni hadaa kwa wananchi, chama
na serikali. Mnyika yuko sahihi.

7. Kama taasisi ya Ikulu na mfumo wake wa utawala umehusika kuingilia
maamuzi ya mhimili wa haki kwa kutoa hukumu ya upendeleo ili kumkomoa
au kumnyang'anya mbunge wadhifa kama jinsi ilivyo lalamikiwa. Mnyika
yuko sahihi.

8. Kama serikali inatenga 70% kwa matumizi kwenye bajeti yake na 30%
kwenye maendeleo. Ni dhahiri kuwa ni aina ya serikali dhaifu yenye
viongozi wavivu wa kufikiri.

Kama hivyo ndivyo, nasimama na kijana mwenzangu kwa ukakamavu na
kupaza sauti yenye mwale mkali. Namuunga mkono Mnyika.

Mkuu nakuunga mkono kwenye hoja zote, na hapo namba 5 ungeongeza ukweli pia kwamba Rais anafunga safari kwenda kutembeza kibakuli ila ukizingatia ukubwa wa msafara anaondamana nao gharama + posho wanazokatiana zinazidi kile anachopata huko!! Hongera Mnyika kwa ujasiri wa kumvika paka kengele!
 
Nasema hivi, nyinyi hamuelewi msemo wa Kiswahili unaosema "asiyefundwa na ***** hufundwa na ulimengu", huyu kijana hajafudwa kwao, na sasa ulimwengu utamfunda. Kacheza na moto ambao haujuwi joto lake.

Kajiingiza kichwa kichwa pabaya sana, kavuka mipaka ya demokrasia, kashindwa kuleta hoja kaleta dharau na hilo hatuliwachi likapita ili iwe fundisho kwa wengine.

Wewe Zomba kwa woga na udhaifu wako hata kikwete akikutaka utamkubalia haraka sana kwa udhaifu ulionao!
 
Hivi kama raisi JK ni dhaifu mlitaka Mnyika asemeje?hivi kama mtu kaiba utatumia lugha gani,je utasema aa kachukua tu,wakati kaiba?jamani kumwambia mtu mkubwa kwa umri au kicheo kama au mtawala au Tajiri kuwa hili haliko sawa tusidanganyane sio dhambi wala sio utovu wa nidhamu.karne ya leo hatutaweza kufika kama huwezi kumwambia mtu makosa yake au mapungufu yake.ni kweli JK ni dhaifu sana.
ANGALIZO wewe ZOMBA usijidanganye kwa kuleta vitisho kumtisha Mnyika,hata kama ni umoja wa wanawake Tanzania zamani ikiwa usalama wa Taifa,USIMTISHE MTU KWA KARNE HII.hapo utaamsha mengi yaliyolala,na usidhani watu hawako nyuma ya Mnyika,tena msije kudanganyana kabisa.
na kwa taarifa yako mnachotakiwa kufanya ni kumshauri JK atende contrary to udahifu wake hapo tutabadilisha lugha,lakini leo hii bado nasema JK ni dhaifu sana
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Mnyika hana sababu yoyote ile ya kushindana na dhaifu Kikwete na alichokisema ni ukweli mtupu na kuna ushahidi chungu nzima kuanzia 2005 hadi hii leo unaothibitisha kauli ya Mnyika. Hata Wabunge wa Magamba waliona Rais wao ni dhaifu ndio maana wakamshikiza awafukuze kazi mawaziri wake. Siyo siri Msanii Kikwete ni dhaifu.
 
Back
Top Bottom