GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kuhani msiba wa Hayati Ali Hassan Mwinyi huko Mikocheni Dar es Salaam ameonekana akiwa na huzuni kubwa sana na masikitiko makubwa akiwa anaongea na vyombo vya habari
Jakaya Kikwete amekiri kuwa yeye hakuwa lolote bali alikuwa katibu wa kawaida wa CCM wilaya ya Masasi huko Mtwara mara baada ya kutoka jeshini miaka hiyo ya 1980's
Kwa mujibu wa Jakaya Kikwete: Rais Mwinyi kwa maono yake ndiye aliyeamua kumtoa huko kijijini Masasi na kumpa ubunge wa viti maalum na baadae kumteua kuwa Naibu Waziri
Jakaya kikwete amesisitiza kwa yeye ni msiba mzito sana kwani amepoteza mtu muhimu kwenye maisha yake aliyamfikisha mpaka hapa alipo kwa sasa
Baada ya maneno hayo ya kukiri kutolewa kijijini Masasi na kuingizwa kwenye mfumo na hayati Rais Mwinyi, Jakaya Kikwete hakutaka kuulizwa maswali mengine toka kwa waandishi wa habari kutokana na majonzi aliyokuwa nayo