Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

unamaanisha nini? au nae ataondolewa bungeni kama Lema kwa kupitia rufaa ya Hawa Nghubi?
 
CDM and its supporters are more loyal to the church than to the country!

vitabu vya dini vinasema kumcha bwana ni chanzo cha maarifa..cdm wanaheshimu dini ndio maana wanatetea watz..Kiongozi bora ametoka kwa bwana lkn sidhani km kikwete amechaguliwa na bwana ..
 
vitabu vya dini vinasema kumcha bwana ni chanzo cha maarifa..cdm wanaheshimu dini ndio maana wanatetea watz..Kiongozi bora ametoka kwa bwana lkn sidhani km kikwete amechaguliwa na bwana ..

Kikwete amechaguliwa na NEC.
 
Udhaifu wa kikwete utakoma tu pale atakapokamilisha ile list ya ahadi zake za 2010, unless otherwise ataendelea kuwa the known 'weak presdaaa'

Jamaa dhaifu sana huyu ona ahadi zake - alitoa akiwa wapi......

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Na wewe magamba yamekumaliza akili ninavyokufahamu sikutarajia kama ungechangia hoja ya kifala kama vile,kwa akili yako wewe unafikiri ccm pamoja na serikali yake watakosolewa na nani?badilika ndugu yangu acha mambo ya zamani.
 
Mkuu kuwa mkweli japo kwa nafsi yako tu jamani! Kati ya kauli ya Mnyika na mipasho+kejeli za kina Nchemba kipi ni matusi na kinakwaza watoto waliokuwa wanafuatilia???

Unachoita mipasho na kejeli havikuwa matusi. Lakini mtoto anapomsikia Mbunge kama Mnyika (kwa umri wake wengi wanatamani wajifunze kutoka kwake), akimdhihaki Rais wa nchi aliyechaguliwa na majority, anamdhalilisha live na kwa makusudi ndani ya Bunge, huyo mtoto anajifunza nini kama si kupotoka kimaadili?
 
Nawaambia hivi, mnazidi kumpa kichwa, kijana aliyepata madaraka madogo tu ya kuwakilisha wananchi bungeni, akashindwa kuchangia hoja ya bajeti akaanza kututukana wengi sana, wabunge wote, na wana ccm wote na wananchi wote.

Huyu hatumuwachi, tutahakikisha anapewa adabu ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Kikwete ni dhaifu...Na wana CCM wote ni wazembe tu halafu zomba unasema Kikwete ni raisi wa Jamhuri ye muungano wa Tz, wakati Zanzibar hawataki? Ungesikiliza baraza la Wawakilishi ungeelewa hali halisi yaani mpaka wawakilishi wa CCM wanaubeza muungano na kuusifia huo Uamsho... Mpakaa nchi inafikia hapa ilipo Kikwete ni dhaifu na hajui hafanyalo

Time will tell! Ukiacha lugha ya maudhi, Je, kuna UTENGE gani katika hoja ya Mnyika?
 
Babu yenu Nyerere alokuwa akiua waziwazi kina marehemu Hanga mbona hakuwahi kuuliwa? na matokeo yake amekuja kuuliwa na ambao aliwaamini sana tunavosikia kutoka kwa kina vicent nyerere! kwani adabu ni kuua tu ! kwalipi kubwa mpaka auliwe mnyika? afungwe tu kumshikisha adabu kwa kumdhalilisha kiongozi wa nchi!
Mama Hanga yupo. Mtafute akueleze vizuri namna mumewe alivyouawa. Ni wakati muafaka sasa kuhoji mambo yote mawili, yaani, MAPINDUZI na MUUNGANO, kuona kama yote ni HALALI.

Msikazanie Muungano tu. Muungano ni mtoto halali wa Mapinduzi ambayo yameleta akina Hanga na wengine kuuawa. Ukishavunja Muungano, Mapinduzi Daima hayatabaki salama.

Mambo mengi yatajulikana likiwemo hili la kuuawa kwa Hanga.
 
Mnyika hana sababu yoyote ile ya kushindana na dhaifu Kikwete na alichokisema ni ukweli mtupu na kuna ushahidi chungu nzima kuanzia 2005 hadi hii leo unaothibitisha kauli ya Mnyika. Hata Wabunge wa Magamba waliona Rais wao ni dhaifu ndio maana wakamshikiza awafukuze kazi mawaziri wake. Siyo siri Msanii Kikwete ni dhaifu.
Mkuu, tuwaache wapambe wapige kelele lakini wataumbuka siku mmoja.

Kwa mwenendo wa JK, hasa nikikumbuka wakati ule wa mjadala wa katiba na jinsi alivyowaumbua CCM kwa kusema kuwa hoja za upinzani zina mashiko kwa vile ni za msingi na mabadiliko makubwa yakafanywa licha ya povu lililowatoka Bungeni la kashfa na kejeli.

Suala la udhaifu wake mie naona hivi karibuni yeye mwenyewe atakuja kiri kwa kinywa chake kuwa " ndugu wananchi mambo mengi yamekuwa hayaendi sawasawa kwa vile nina udhaifu katika kuchukulia hatua makada wa chama changu kwa kuogopa kuleta makundi"

Baada ya kauli hiyo hawa wanaotoa povu hapa watasema nini? kuwa Rais kajitukana? Nakuhakikishia kauli hiyo lazima siku moja ataitoa.

Weka kumbukumbu ya nilichokisema leo.
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Mimi nasikitika sana kwamba hivi watu kwa nini mnabadilisha mada kiasi hiki?
Hivi kweli kusema JK ni dhaidu Mnyika amemtukana? Jamani kumbukeni mnyika si mtoto alichaguliwa na wananchi wa Ubungo ili awatetee. Yupo Bungeni kwa maswala nyeti ya taifa na angekuwa mtoto asingepewa majukumu na watu wa Ubungo kuwawakilisha Bungeni kwa maslahi yao.
Ninachoshangaa hivi amemtukana wapi JK? . kusema dhaifu ni tusi?

Yeye anajadili hoja za utendaji wa kazi na kwamba Budget inaandaliwa na Rais na kisha inawekwa saini ya wino mwekundu na JK na baadaye WAziri muhusika anapewa tu kwenda kuisoma . Sasa kusema hii budget inaonyesha udhaifu wa JK ndio anambiwa yeye ni mtoto amemvunjia heshima?
Angekuwa mtoto asingeruhusiwa kwenda pale Bungeni yeye anajadili kama Mbunge habari ya mtoto au mtu mzima JK inakujaje jamani?
Mimi napenda heshima kwa mtoto kumheshimu mkubwa lakini pale mkubwa anapokwenda kinyume aelezwe ukweli
Sasa anaambiwa kashindwa kujadili budget kisha anamtukana JK, jamani naomba tuache maneno ya KIZUSHI
Mimi si mwanachama wa CCM wala CDM na ninasema Mnyika hajamtukana JK.........
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Silly thinking, silly season............... Hivi kuna maendeleo Tanzania??? Labda unazungumzia kwenye familia chache za wana CCM wa Tanzania............ ambao walitokea kwenye familia za wakulima na wafugaji lakini leo hawawezi kuishi kwenye nyumba isiyo na swimming pool!!

Otherwise, to ordinary citizens, Tanzania is all about Poverty, hunger and diseases!!
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Ndugu Zomba; Watanzania tupo kama 45M, wanaoweza kupiga kura ni kama 22M unaweza kunieleza Rais Kikwete alichaguliwa na Watanzania wangapi na ni asilimia ngapi ya watanzania wote?, na hao waliobaki je wangempigia kura ya ndiyo au Hapana kama kukiwa na uchaguzi huru na wahaki na uliondaliwa mazingira mazuri ya kila aliyejiandikisha kupiga kura anapiga, (walau 85% ya waliojiandikisha kupiga kura waweze kupiga kura)

fikiria na tafakari ni wangapi wanaweza kuwa wamefurahishwa na kauli ya Mh Mnyika pia.
 
Mkuu, tuwaache wapambe wapige kelele lakini wataumbuka siku mmoja.
Kwa mwenendo wa JK,hasa nikikumbuka wakati ule wa mjadala wa katiba na jinsi alivyowaumbua CCM kwa kusema kuwa hoja za upinzani zina mashiko kwa vile ni za msingi na mabadiliko makubwa yakafanywa licha ya povu lililowatoka Bungeni la kashfa na kejeli.
Suala la udhaifu wake mie naona hivi karibuni yeye mwenyewe atakuja kiri kwa kinywa chake kuwa " ndugu wananchi mambo mengi yamekuwa hayaendi sawasawa kwa vile nina udhaifu katika kuchukulia hatua makada wa chama changu kwa kuogopa kuleta makundi"
Baada ya kauli hiyo hawa wanaotoa povu hapa watasema nini? kuwa Rais kajitukana? Nakuhakikishia kauli hiyo lazima siku moja ataitoa. Weka kumbukumbu ya nilichokisema leo.

Mfanyabiashara anayetaka kuzalisha biashara mpya tena ambayo anaamini haiwezi kushindana na iliyopo,lazima ataipaka matope sana ile ya awali, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa awali ni awali tu, Jk ni mwisho wa maneno.
 
Nawaambia hivi, mnazidi kumpa kichwa, kijana aliyepata madaraka madogo tu ya kuwakilisha wananchi bungeni, akashindwa kuchangia hoja ya bajeti akaanza kututukana wengi sana, wabunge wote, na wana ccm wote na wananchi wote.

Huyu hatumuwachi, tutahakikisha anapewa adabu ili iwe fundisho kwa wengine.
Adhabu ya kumvizia njiani na kumpiga mawe? maana hakuna nyingine. Hujui hata sheria za nchi hii? kauli yeyote ndani ya bunge inalindwa na sheria za bunge na ndio maana kapewa adhabu ya kutoka nje jana full stop.

Na kwa taarifa yako Mnyika ni jembe la uhakika, maana ingekuwa ni mbunge wa CCM ukimtoa nje yeye ni kwenda Chako ni chako kufakamia mipombe na mademu au wake za makada wa chama ajirushe, Mnyika ni muda wa kujisomea na kufanya research mbalimbali atakazo kuja kuwalima nazo.

Poleni sana yeye hatoki kile chama cha kipuuzi anatoka chama cha watafuta maendeleo ya nchi.
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Ujinga kweli ni mzigo mzito kuliko kontena. Angekuwa kweli hamuwezi usingekuta wewe upo bize hapa kumtetea. Naamini simba aliyelala hawezi kupoteza usingizi wake kwa kuwa panya anaunguruma. Hii ni dalili hata wewe unaujua udhaifu unaozungumziwa na ndio maana umejivika kibwebwe kucheza ngoma ya utetezi.

Ni ulegelege ndio unasababisha waliomzunguka na kumtambua ulegelege wake waanze kutafuna mpk hela za safari zake za kwenda kujikomba kwa wagawa suti.

Mnyika sio saizi yako, ameshindwa Hawa Nghumbi itakuwa wewe na suruali yako njiwa na makubazi?!

Siku zote unavyopinga muungano nilidhani uko na Mtikila, kumbe upo mulemule? Kumbe kinachokuunganisha na Kikwete ni UDINI na sio itikadi za kisiasa kwa kuwa mwenzio anataka MUUNGANO
 
unasema tu ni "dhaifu" lakini unashndwa kuonesha maendeleo yaliofanywa na rais yeyote wa kabla yake ambayo kikwete hajafanya zaidi.

Mnaposhindwa hoja mnaanza viroja, si humu jf tu, hata bungeni.

mheshimiwa zomba, pole mkuu, mie navyojua mbunge anapokwenda kinyume na taratibu za kikao hupewa alternative mbili 1.kufuta kauli yake au 2.kuthibitisha alichokisema. Wampe mnyika nafasi ya kuthibitisha udhaifu alionao kikwete.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom