Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
zomba, umenikumbusha hadithi ya Biblia pale shetani (in the form of a serpent) alipokuja kwa Eva/Hawa na kumuuliza, "Eti Mungu amewakataza kulila tunda la mti huu!??"

Kumbuka tu mtu anapotumia hilo neno, huwa anamaanisha kuwa anaujua ukweli wa alichokisema na anajuakiko sahihi, so it just remains to be a rhetorical question.
Thank you for acknowledging that.
Mchana mwema...
 
Last edited by a moderator:
[h=2]"Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete"!! Mleta mada hivi ni vita binafsi na Kikwete? au ni vita kwaniaba ya watanzania wote wapenda maendeleo??????!!!!! :frusty:[/h]
 
Unasema tu ni "dhaifu" lakini
unashndwa kuonesha maendeleo yaliofanywa na Rais yeyote wa kabla yake
ambayo Kikwete hajafanya zaidi.

Mnaposhindwa hoja mnaanza viroja, si humu JF tu, hata bungeni.

Mfumko wa bei,madawa hospitalini hamna,mishahara ya watumishi ni kiduchu. Ni viwanda vingapi vya serikali vimejengwa?
 
Unachoita mipasho na kejeli havikuwa matusi. Lakini mtoto anapomsikia Mbunge kama Mnyika (kwa umri wake wengi wanatamani wajifunze kutoka kwake), akimdhihaki Rais wa nchi aliyechaguliwa na majority, anamdhalilisha live na kwa makusudi ndani ya Bunge, huyo mtoto anajifunza nini kama si kupotoka kimaadili?

Huyo mtoto anajifunza kuwa mkweli kwa nafsi yake na kwa jamii! Kama kiongozi ni dhaifu na hata hao watoto wanaliona hilo wazi, haisaidii kimalezi kuendelea kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Hebu jaribu kufanya utafiti kidogo tu hapo mtaani kwako kwa kuwauliza watoto kama waliisikia kauli ya Mnyika na wana maoni gani - naamini watakushangaza sana mkuu!
 
Acha kutishia nyau wewe, huna lolote na hamtanfanya lolote.Tatizo hamtaki kuambiwa ukweli nyie magamba.
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Kwenda zako husitishe watu wakati wewe mwenyewe ni dhaifu kwa ulichoandika hapo juu!
 
"Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, kwa uzembe wa Bunge, na kwa sababu ya upuuzi wa CCM."
Tuma kwa watu 10 kama unamsapoti Mh. Mnyika bungeni.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mkuu hii imenyooka kweli kweli. Miaka 50, 100 ijayo itakuwepo kwenye Dictionary of quotations. Wakati huo wajukuu zangu watakuwa wanastaajabu tuliwezaje kuchagua hawa wanaotuongoza kwa hiyo hata na sisi tutaitwa wapuuzi pia
 
Nadhani imefika wakati sasa Rais inabidi aoneshe udikteta kama wa Mkapa , enzi zile midono ya watu kama hawa ilifyata kama mikia ! Rais tunaomba uwashikishe adabu watu kama hawa ambao hawana nidhamu kabisa, hata iweje huwezi kuwa na kiburi na dharau kiasi hicho kwa kiongozi wako wa nchi! Rais tunaomba huyu aadabishwe ! na iwe fundisho kwa wengine !

Acha ujinga wewe! Akiwa kama Mkapa unafikiri anaweza kupatikana mwanaume wa kutangaza hadharani kuwa atasusia SENSA?
 
Mimi inawezekana simuwezi kwa kuwa sipo pale mjengoni wala Serikalini, lakini nasema Mnyika Kikwete hamuwezi. Amuone vile vile anacheka cheka, lakini "mtoto akichezea wembe muache". Sisi tunalitazama hili sakata litaishia wapi.

Hatutomwachia kabisa "mpaka kieleweke", kitoto kidogo kile hakiwezi kuja kututukana tukakiacha kicheke cheke hovyo. Lazima ajuwe maana ya Serikali ni nini, maana ya Rais ni nini, maana ya Bunge ni nini na maana ya kutukana ni nini.

Naanza kampeni rasmi, ya kuhamasisha kushikishwa adabu. Na hapa nimeanza tu, kukumbusha kuwa Mnyika Kikwete hamuwezi.


Wana macho hawaoni.. wana masikio hawasikii...umaskini ni ugonjwa mbaya sana kuliko hata UKIMWI.. maana ukimwi hudhoofisha mwili na sasa kuna ARV, lakini umaskini hudumaza AKILI na hakuna tiba ya akili, na akili ikidumaa hata uwezo wa kufikiri hudumaa na hii ndio silaha kubwa ya CCM na imetumika kwa watu kama Zomba samahani sijui jina lako lina "M" maana nilifikiri lingefaa zaidi kama ungeondoa hiyo "M" kati ya"o" na "B"! maana watu wa aina yako hilo jina ndilo linawafaa!
 

Mnyika alikosea.


Mbunge anayeanza kwa kueleza matatizo ya jimbo lake, ufinyu wa bajeti iliyoelekezwa huko na jinsi serikali ilivyolisahau jimbo hilo kimaendeleo halafu mbunge huyo huyo anamaliza kwa kusema "...Mh. Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono bajeti hii kwa 100%....bajeti hii itapita.....na ndugu zetu msiojua ustaarabu jifunzeni kwetu" (hapa misukule mingine iliyobaki inapiga makofi na kushangilia) kamwe mbunge wa namna hii hawezi kuwa MPUUZI kamwe, huyu ni MPUMBAVU kabisa.

Ni vile Mnyika hajui kutofautisha wapuuzi na wapumbavu mpaka amefikia kuwadhalilisha wapuuzi kwa kuwafananisha na wabunge wa namna ya Lusinde

Halafu hili neno 'mpuuzi' watu wanalitafsiri kwa maana mbaya while neno hili linam-refer mtu anayepuuza mambo ama jambo,
Je CCM haijapuuza maswala la msingi yanayohusu maslahi ya taifa(refer mgomo wa madaktari).
Kwa upande wangu haya ni maneno ya kawaida na yalipaswa kueleweka kwa maana na si kwa intonation kwa maneno hayo yalivyosemwa na kaka mkubwa Myika.
Tunahitaji wataalamu wa kiswahili watafsiri maneno haya: uzembe, upuuzi na dhaifu alafu tupime kama ni matusi au la!!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Zomba wewe ni sawa tu Msukule.Usitishe watu na wala usimtishe Mnyika na Mdhaifu wako huyo.Kama unataka kupima reaction ya ujinga wako kwa jambo ili ni kwamba wewe na wana magamba wote ni dhaifu na goigoi.Mnyika atishwi kwa uchawi wa Mlingotini Bagamoyo wala wapi maana Yeye amefunikwa kwa damu ya kristo na mtetezi wake yu Hai siku zote.
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

we kibatari kweli
 
Do we know our limitations? I think that could give us wisdom to trade our life with care. Kutishiana ni sign ya weakness kubwa individuals waliyonayo. Ukiona mtu akiambiwa ukweli anaanza kutishia wenzake just know he has got low security inside him/herself...We have a lot that we do not know and in fact, the only power that the national has is
the mandate of Tanzanians. Do we know that the power we are seeking is earned and not given for free as most of the politicians would like to?
Madaraka yasitudanganye kwamba we are untouchables...yanakuja na kwenda and what matters today could probably be not important tomorrow. Tuwatumikie watanzania kwa wakati muafaka wataamua nani awe nani na hukumu yao itakuwa ni ya ukweli mtupu. Mhhh...what a weakness!!
 
sina mengi sana ya kusema na subiri tuone utakacho mfanya mnyika maana wewe unaongea mambo ambayo wana ccm hawawezi kuongea kwani unajua madhara yake.

Sasa mi nasema tusubiri maneno yako yatimie tuone utamfanya nini mnyika wewe!
Unakataa nini wewe jk ni dhaifu unatokwa povu zaidi ya riz na mwanaasha.

Unatatizo gani wewe kwni huoni kama jk ni dhaifu,basi mnyika kauona.

Hahaa amechemka huyo zomba anatoa vitisho utadhani amepanga kwenda kwa Sheikh Yahya
 
Last edited by a moderator:
alaah!,we kweli ni zomba,yaani unataka kujustify udhaifu wake kuwa ni sawa kwa kuwa viongozi wengine nao walikuwa dhaifu kama yeye kwa hiyo tuchukulie poa tu badala ya kumshauri ajirekebishe,daaah,nina shaka na upeo wako zombiiiiiii
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Kwa nini zomba, au madhabahu yake imeshiba.
 
Mnyika ameharibia watoto wetu wanaofuatilia kwa makini Bunge kwa lengo la kujifunza jinsi wawakilishi wetu wanavyoongea na kuijadili bajeti.

Pamoja na kufurahia bunge, watoto pia wanajifunza jinsi watakavyoongea wakikua iwapo wataamua kuingia kwenye siasa.

Walichojifunza kwa huyu mpuuzi Mnyika ni jinsi ya kuwatukana baba zao hadharani.

Aibu sana, nimewapiga marufuku wanangu kuangalia kipindi cha Bunge ....until further notice.

Unaweza kuwazuia watoto wako wasiujue ukweli lkn huna jitihada za kuwafanya wasiwe dhaifu kama baba yao, hapo ndio unaponishangaza.
Ngoromwiko, mtu mzima akijamba mbele za watu, halafu mtoto akasema 'baba' kajamba, aliyefanya kosa hapa si mtoto aliyesema, bali ni baba aliyejamba mbele za watu.

Be reasonable and fair, mtukanaji ni aliyefanya upuuzi na sio aliyesema fulani ni mpuuzi.
 
Last edited by a moderator:
Mnyika hana Mashindano wala Vita yoyote na Kikwete ametumia haki yake ya msingi kueleza yale anayoyaamini kuwa ni sahihi.Hayo ambayo wewe unayasema na uliyoyaona ni mtazamo wako na una haki kufanya hivyo!
 
Back
Top Bottom