Mkutano wa CCM Mbeya

ButolaHapa hatuko kubishana. Kama hii picha ya maandamano inaonyesha uchache wa Wanamagamba basi wewe tuletee hiyo ya UWANJANI YENYE NYOMI. Full stop!Sana sana watakuwa ni wale watoto wa shule na Wanavijiji walioletwa KWA MAFUSO TOKA VIJIJINI.
Mkuu nina wasiwasi kama ulikuwepo uwanjani na nina wasiwasi kama ulishuhudia maandamano na mwisho kama ulikaa mpaka mwisho unaweza kutuambia yale mafuso, malori, basi mbili, coaster kadhaa na pickup ziliondoka na nini na zilipeleka wapi
 
A13.JPG
hakuna kitu hapa! wanajifariji tu ....kwa hali ya sasa hakuna kitu cha kupigia makofi kutoka kwa CCM! Makamada mko wapi mtuongoze kuingia mitaani kupinga huu mgao?
 
Lengo la maandamano ni kwa wanaCCM wa Mbeya kuupongeza uamuzi wa NEC na Secretarieti mpya ya chama wa kuelekea kuijenga CCM katika mtazamo mpya, na Lengo la mkutano ni kuuelezea umma wa Mbeya zana nzima ya kujivua gamba na hatua zilizofikiwa mpaka sasa katika harakati za kukisafisha chama.Kwa wale waliokaribu na mji wa Mbeya, mkutano huo utarushwa Live na Radio Generation FM.
mbona lengo haliko kwenye mtiriko mzuri? Au umeamua kutoa lengo unarohisi au unalojisikia kutoa kutokana na hisia zako.
 
Nilikuwepo kwenye mkutano wa leo, nilikuwepo na ule wa Chadema Mwezi Mei. Hakika kwa idadi ya watu, mwitikio na hamasa, CCM na CDM ni kama Mbingu na ardhi. CCM hawakufikisha hata nusu ya uwanja wa Ruanda Nzovwe. Ikumbukwe mkutano wa CDM ulikuwa wa Jimbo/Wilaya ya Mbeya mjini wakti huu wa CCM ulikuwa wa Mkoa mzima. Walikuwepo wana CCM toka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya. Labda kwa upande wa sare na tu ndio CCM walifunika kwani wanachama wao walipendeza kwa kijani na njano. Nusu ya watu waliohudhuria hata hivyo walikuwa wanaguna tu kwa kila kinachosemwa pale japo Nape kajitahidi kuvutia na kurudisha imani kwa wana CCM wenzie
 
CCM hawakufikisha hata nusu ya uwanja wa Ruanda Nzovwe. Labda kwa upande wa sare na tu ndio CCM walifunika kwani wanachama wao walipendeza kwa kijani na njano. Nusu ya watu waliohudhuria hata hivyo walikuwa wanaguna tu kwa kila kinachosemwa pale japo Nape kajitahidi kuvutia na kurudisha imani kwa wana CCM wenzie

Duh..kweli upenzi mbaya sana, maana unaweza ukajipofosha macho usione, na kuziba masikio usisikie ili kuufariji moyo wako..., naona kwenye red ukaukubali kidogo ukweli mchungu na kumalizia kwa kutabiri ni Wana CCM wenzake...duh...

Niseme tu, leo CCM wamefanikiwa sana Mbeya, nimeuona uungwaji mkono mkubwa sana wa Wapiganaji wa CCM kutoka kwa makundi yote yaliyokuwepo uwanjani, hii ni ishara kuwa kazi bado mbichi sana hapa, hatuna budi kuukabili ukwelii, tusijifariji kwa kujifanya manabii na kuishia kujilisha upepo...
 
mh mbna mkutano umeisha hamja tutumia picha wala taarifa za kina kuhusiana na mkutano wao
 
Hao akina Sendeka na sita ndio wameonekana wana Mvuto!! Hadi Aibu, Ila wananchi ni Bora Wajue wenzao wamelipwa posho na sio Kuandamana bure!!!
 
Nahitaji picha zaidi kuona ukweli kama kweli CCM walikuwa na watu .Lakini kama ni hii picha tu basi hakuna kitu tukubaliane .Hebu wacha nione magazeti yanasemaje .
 
hakuna kitu hapa! wanajifariji tu ....kwa hali ya sasa hakuna kitu cha kupigia makofi kutoka kwa CCM! Makamanda mko wapi mtuongoze kuingia mitaani kupinga huu mgao?

inahitaji uwe mnafiki kujumuika na hili genge ninaloliona kwenye picha.
 
wao si waliwaambia wenzao wakubali ushauri wa kuandamana usiku, sasa wao mbona wanaandamana mchana??
 
Mungu tunaomba uisaidie nchi hii,Jamani hii ndio Tanzania,Kiukweli kwa hali nchi ilipofika ni mbaya hasa kiuchumi na huduma za jamii.Lakini mi binafsi nakishangaa chama cha ccm kimethubutu vipi kuendesha maandamano wakati chenyewe ndio chanzo?Pia nawashangaa watu waliohudhuria huo mkutano kama wana akili kweli.Sita,Sendeka,mwakembe,kilango njaa ndio inawatesa believe or not ni njaa tu na unafiki.Hivyo hao ni the gutters politician.Na tunawananchi wengi hapa tz ambao pia ni the gutters citzens,Kwa hili hamna maendeleo mpaka kiama.La sivyo mapinduzi ya haraka yanahitajika
 
Nape ameitoa kauli hiyo alipokuwa akitolea ufafanuzi wa dhana ya kujivua gamba, katika mkutano CCM uliofanyika jana Mbeya.

Kauli hii ya Nape Nnauye ni mfulululizo wa kauli zenye dharau kama si utusi ndani mwake zinazotolewa na viongozi wa CCM ambao wapo ktk NEC pia ni viongozi wa Serikali.

Nape anatakiwa kuwaomba msamaha watendaji wote wa serikali na umma wa watanzania.

Source: Gazeti la Mtanzania, 17-07-2011
 
Serikali ni ya wananchi!Ukiona Mtu anawalinganisha watendaji wa serikali na Wauza Duka Ujue Kafilisika Kisiasa na Hajui Analosema!
Watendaji wa serikali wanatakiwa wafananishwe na Moyo unaosukuma damu ktk mwili wa Kiumbe Hai!
 
Jamani hiyo ndo kazi ya Nape, propaganda na kueneza upupu na kugeuza uongo kuwa ukweli, sishangai kitu hapa kwani watu wengi wananjaa, CCM wana pesa na hii ndo kazi yake. Kwa chama chochote cha upinzani, lazima wawe makini na they must play more smarter than these guys. Hakuna linaloshindikana, kila kitu kinawezekana, CCM wako katika wakati mgumu sana saizi, kwa hiyo lazima watumie hela, kila aina mbinu kujaribu kuwawin watu warudi kwenye chama chao.
 
Mkuu umenena.
Unajua ni mtu mwenye kiburi au mlevi wa madaraka ndiye anaweza akatoa kauli ya utusi kama hiyo. Ni kugha picha yenye maana mbaya sana. Ninapomwangalia mwalimu, daktari, mhandisi, mhasibu, mchumi, askari, nk... ya kwamba ni wauza duka inakera sana.
 
Back
Top Bottom