Mkutano wa CCM Mbeya

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
62,204
128,020
kama kuna mtu yuko mbeya naomba atujuze kinachondelea kwenye maandamano na mkutano wa CCM. tupia hapa habari tujadili bandugu.
 
Nipo njiani kuelekea kwenye mkutano, nitarushia picha mkutano ukiisha kwani simu yangu ya mchina haitasaidia
 
Nipo njiani kuelekea kwenye mkutano, nitarushia picha mkutano ukiisha kwani simu yangu ya mchina haitasaidia
Mkuu unaenda kwenye mkutano au maandamano, maana wanaanza na maandamano...usiache kutupa live updates, na pichaz usisahau ujumbe wa kwenye mabango, maana hadi sasa hawajasema nia ya maandamano maana hawakawii kuyaita maandamano ya kulaani "maandamano ya vurugu" ya chadema
 
Naomba tu wasisahau picha za mabango. Hawa ccm sijui watapataje watu maana hawasemi lengo la maandamano. Sijui wamewapa polisi taarifa gani maana wanatakiwa waseme na lengo la maandamano kwenye taarifa yao. Au kama huko mby wanatangaziwa watutaarifu na sisi!
 
Lengo la maandamano ni kwa wanaCCM wa Mbeya kuupongeza uamuzi wa NEC na Secretarieti mpya ya chama wa kuelekea kuijenga CCM katika mtazamo mpya, na Lengo la mkutano ni kuuelezea umma wa Mbeya zana nzima ya kujivua gamba na hatua zilizofikiwa mpaka sasa katika harakati za kukisafisha chama.

Kwa wale waliokaribu na mji wa Mbeya, mkutano huo utarushwa Live na Radio Generation FM.
 
taarifa zilizotufikia sasa hivi ni kwamba wameenda kuchukua watu kutoka vijijini na walipofika mjini mbeya gari yao moja imegonga mtu na kumwua,
nimeongea na ndugu yangu yuko mbeya sasa hivi!
 
taarifa zilizotufikia sasa hivi ni kwamba wameenda kuchukua watu kutoka vijijini na walipofika mjini mbeya gari yao moja imegonga mtu na kumwua,
nimeongea na ndugu yangu yuko mbeya sasa hivi!

inamaana hapo mjini hamna watu? CCM mbona wanalazimisha mambo? kizuri chajiuza kibaya cha jitembeza
 
Inakumbusha yale yakukusanya madawati ilimkalie wakati kiongozi anakuja alafu akisha pita mnaendelea kukaa chini kwenye mawe! Yaani ni kujidanganya mwenyewe.
 
Back
Top Bottom