Setuba Noel
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 426
- 210
Mh! Hapa umetuingiza chaka, hili tukio halijapata kutokea katika historia ya Mwalimu. Kansa yake iligunduliwa 1998, mwaka mmoja baada ya ile birthday yake maarufu ya 75 (mwaka 1997) ambako katika hotuba alikuwa amesema "....nitapiga makumi mawili manne, NINA HAKIKA! Nitamwona rais wetu wa nne, NINA HAKIKA" akimaanisha alikuwa na uhakika wa kuishi miaka zaidi ya themanini na kuchagua hadi rais wetu wa nne.Kwa wale tuliokuwa watu wazima 1989 tunakumbuka Jinsi Mwalimu alivyolazwa Uingereza kwa matibabu ya Kansa (Saratani) ya damu ambayo hatimaye ndiyo ilikuja kumuua.
Hizi tabia za kusahau mambo ya msingi ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Toka 1989 hadi leo 2012 imepita miaka 23 huyu Vincent alikuwa wapi kutuambia kwamba Mkapa amempa Mwalimu Sumu itakayokuja kumuua? Kama amejua siku za hivi karibuni ni nani aliyemwambia? Hivi mwaka 1989 wakati Mwalimu anafanyiwa Opresheni ya kuzuia kansa kusambaa mwilini mwake Mkapa alihusikaje?
Na hiyo kansa alidumu nayo mwaka mmoja tu na kufariki akiwa na miaka 77, maskini hakuifikia ile 80 aliyokuwa amesema ana uhakika "angepiga"! Na wala hakuwahi kufanyiwa operesheni, haiko kwenye rekodi za maisha yake. Kama unazungumzia bone marrow biopsy hiyo ni diagnostic procedure, na wala siyo huo mwaka wa 1989, ni 1998 alipogunduliwa na Chronic Lymphocytic Leukemia.
Hakuna taarifa kuwa Mwalimu aliwahi kufanyiwa bone marrow transplant ambayo ni mojawapo ya tiba za uhakika za CLL, na hii ingefanana na operation, na ingemwezesha kuishi miaka isiyopungua 10 bila leukemia. Lingine ni kuwa prognosis ya CLL siyo mbaya kama ilivyotokea kwa Mwalimu Nyerere ambaye alidumu nayo kwa mwaka mmoja tu.