Zanzibar 2001: Kulikuwa na umuhimu kutumia mabavu kiasi kile?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784

"Stop, O People, that I may give you ten rules for your guidance, in the battlefield. Do not commit treachery or deviate from the right path. You must not mutilate dead bodies. Neither kill a child, nor a woman, nor an aged man. Bring no harm to the trees, nor burn them with fire, especially those which are fruitful. Slay not any of the enemy's flock, save for your food. You are likely to pass by people, who had devoted their lives to monastic services, leave them alone" - Caliph Abu Bakr


Uungwana kipindi binadamu mwenzako anapitia changamoto ndicho kipimo kikubwa cha ustaarabu ambacho mwanadamu anaweza kukionesha. Huwa ni rahisi mno kujionea huruma, lakini ni nadra mno kuonesha huruma kwa binadamu mwenzako. Ukiweza kuonesha huruma kwa binadamu mwenzako hasahasa pale unapokuwa na uwezo wa kumdhuru basi umefikia hatua ya juu kabisa ya ubinadamu.

Katika falsafa ya sheria ya makosa na adhabu (Criminology & Penology), adhabu ni muhimu kutekelezwa lakini hakuwezi kuwa na haki ndani ya dola endapo watawala hawatafahamu kwamba HURUMA NI SEHEMU YA HAKI (Mercy is part of Justice). Nimefika umri huu, naanza kutafakari kwa kina kuhusu mauaji ya kutisha ya ndugu zetu wazanzibar mwaka 2001, naanza kusisimka mwili na kuogopa mno, maana nikiiweka Tanzania katika mizani ya ustaarabu na amani ambayo tunapenda kujisifia tunayo nahisi tunaishi maisha ya kuigiza.

Binadamu hawajaanza kupigana vita karne za 20 na 21, bali tangu maelfu ya miaka mingi iliyopita. Jambo ambalo utaliona kwa umakini endapo utasoma ni kwamba, jamii zote za kistaarabu tokea kipindi cha madola ya kale ya Umedi & Uajemi, Mekedonia, Rumi, Tang, Uingereza hadi kufika sasa, ziliamua kutengeneza baadhi ya kanuni na miongozi ya kufuata wakati wa vita na machafuko. Ndiyo maana nikaweka nukuu muhimu hapo juu mwanzoni, ili niweze kuzizungumzia hizo kanuni kwa urahisi kama ifuavyo;

Mosi, dola lolote lile duniani huwa lina nguvu za kisheria za kutumia mabavu (Monopoly of Violence) ili kuweze kutunza amani, kulinda raia na mali zao na mara nyingine hata kuvamia madola mengine na kuyatawala. Ila katika dunia yetu hii ya leo, dola lolote lile haliwezi kutumua mabavu bila kufuata kanuni za kisheria hasahasa zile za haki za binadamu.

Pili, endapo mabavu yatatumika basi ni lazima iwe katika hatua ya mwisho (Last Resort), baada ya kila mbinu ya kisiasa na kisheria ya kuleta suluhu imeshindikana. Hivyo ni lazima dola ifahamu fika kwamba hao inaoshughulika nao, hata wawe wabaya vipi ni raia wake ambao inatakiwa kuwalinda hata baada ya machafuko kuisha, maana hao raia ndiyo walipa kodi, wakulima na wafanyakazi.

Tatu, kuna ulazima wa kupima na kufahamu kiwango cha machafuko (The Threshold of Harm/Violence), endapo ni machafuko tu ya kisiasa (Civic and Sporadic Violence) ambayo hutokea duniani kote na hupita baada ya muda, AU machafuko yenye alama za ugaidi, uhaini na matumizi ya jeshi (Terrorism/Political Insurrection/Armed Struggle). Hili husaidia kufahamu ni aina gani ya vikosi vitatumika aidha polisi wa kawaida au wanajeshi, silaha aina gani zitatumika aidha zile kutuliza vurugu au silaha za moto, na mwishowe ni mbinu zipi za kijeshi zitatumika aidha kutawanya mkutano (Dispersion), kufunga mji watu wasitoke majumbani (Curfew), kufungwa kwenye kambi maalumu (Internment), kuwekwa kizuizini (Detention) au kuhamishwa kinguvu mpaka amani irudi (Forcible Deportation).

Nne, kanuni za kisheria lazima zizingatiwe na wale wafanya maamuzi ndani ya vyombo vya dola. Kanuni za kuzingatia ni :​
  • Kanuni ya umuhimu wa shambulio (Principle of Military Necessity), ambayo inamtaka afisa wa jeshi kufanya tathmini na kujiuliza endapo kuna umuhimu wa yeye kufanya shambulio la kijeshi wakati huo. Lazima aangalie mazingira yanayomzunguka pamoja na watu wanamzunguka, maana unaweza ukatumia nguvu halafu kukawa na raia ambao hawana silaha na hawahusiki ukawaumiza (Collateral Damage).​

  • Kanuni ya uwiano wa shambulio (Principle of Military Proportinality), ambayo hutaka afisa wa jeshi asitumie atumie nguvu inayoendana na hatari iliyopo. Aangalie kama huyo mtu wa mbele anatakiwa kupigwa kirungu, kumwagiwa maji ya kuwasha, kupigwa risasi za umeme, mabomu ya machozi, risasi za mpira au rasasi za moto. Ukimuona raia kashika silaha ambayo inatakiwa kukudhuru basi ni lazima askari ajilinde na kukakikisha yule raia anadhibitiwa. Lakini ukienda na kuanza kuua tu mtu anayeandamana ni makosa makubwa mno.​

  • Kanuni ya utanganifu (Principle of Distinction), ambayo hutaka afisa ajitahidi kutengenisha raia ambaye hahusiki moja kwa moja na uhalifu (Indirect Participation in Civil Strife) dhidi ya raia anayehusika moja kwa moja na uhalifu (Directly Participating in Civil Strife). Hapa ni muhimu kuzingatia kwamba, hii kanuni iliwekwa fika ikifahamu kwamba kuna raia wengine wanaweza kuhusika na machafuko kwa kufuta mkumbo (Herd Mindset) au wengine bila kufahamu kama wanatumika, Vladmir Lenin analiita hili kundi , The Useful Idiots. Ni muhimu kufanya hivi maana mara nyingine unaweza kukuta mzazi hahusiki ila mtoto wake anahusika, kiasili ni wajibu wa mzazi kutaka kumlinda kijana wake dhidi ya mkono wa dola japo wote watakuwa wanafanya makosa lakini ni lazima askari asimguse yule mzazi kama ambavyo atamgusa mtoto anayehusika moja kwa moja.​

  • Kanuni ya ubinadamu (Principle of Humane Treatement), kwamba baada ya kudhibiti machafuko na wahuni wanaoleta taharuki, sheria zichukue mkondo wake haraka na raia wasiguswe kabisa na mkono wa dola. Masuala ya kuadhibu kundi zima (Collective Punishment) ni ushetani ambao ni lazima uzuiwe. Mhalifu akishakamatwa basi atiwe nguvuni (Under Protective Custody) na sheria nyingine ndiyo zifuate, bila kuteswa au familia yake nzima kuanza kushughulikiwa, KGB huita hili, The Scarlet Letter. Unaweza kusema hili haliwezekani lakini kipindi cha KIFURUFUMBI baada ya Mzee Nyerere kukoswa na Uasi hili liliwezekana, ambapo polisi waliwakamata kina Hans Poppe na wenzake, halafu vijana wa USALAMA WA TAIFA wakataka kuwachukua kinguvu na kuwapeleka sehemu isiyofahamika. Mkuu wa kitua ambaye alikuwa anawashikilia wale wahaini hakutetereka na kuwakatilia maafisa usalama kwamba hawana mamlaka ya kuwaondoa watuhumika pale kituoni. USALAMA WA TAIFA walijaribu kila mbinu lakini yule mzee aligoma kabisaa, na wakaufyata na mwishoni haki ikatendeka, na wakahukumiwa kifungo cha jela.​
Sasa tukizingatia haya, nadhani kule Zanzibar ulifanyika uvunjifu mkubwa mno wa haki za binadamu kuwahi tokea hapa nchini, ukifuatiwa na ule wa MTWARA kipindi cha sakata la gesi. Nimeziangalia kumbukumbu ambazo ziko ASSOCIATED PRESS (AP), na kuona jinsi mambo ya ajabu yalikuwa yanafanyika. Polisi wanaingia nyumba hadi nyumba, wanaanza kupiga kila mtu bila huruma. Mashahidi wengine wanasema kwamba walishuhudia watu wanapigwa risasi bila huruma na hata kundi maalumu la wanawake na watoto kudhalilishwa, A thing that strikes a nerve to consciousness of any sentient being.

Serikali ya Mzee Mkapa (R.I.P) ingepambana na wanaume wanaohusika moja kwa moja (Directly Participating in Civil Strife) tungesema walau sawa, lakini WATOTO NA WANAWAKE ni kuvuka mstari mwekundu. Dola la Tanzania limejaza MASHUSHUSHU na MAJASUSI kule Zanzibar kuliko sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania, hivyo walikuwa wanafahamu kila kinachoendelea kwenye vikao vya siri huko Misikitini, Mahotelini na hata vile vilivyofanyika OMAN. Haikuwa na ulazima wowote ule kufanya mauaji kiasi kile na kuwatesa raia na kuwaachia jeraha kubwa rohoni ambalo liliongeza ufa mkubwa kwenye MUUNGANO.

Kuthibitisha hili, MASHEIKH WA UAMSHO walipoanza harakati zao, ramani zao zote na vikao vyao vyote vilikuwa vinafahamika na serikali ya Raisi Jakaya Kikwete. Kama huamini hili jiulize, Mzee Nyererer alifahamuje kuhusu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi miaka ya 80's ilhali yeye yuko humu bara ? Hivyo, nachelea kusema kabisa, hakukuwa na haja ya kutumia nguvu kiasia kile.

Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila (R.I.P), alitoa tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa kipindi hicho, Balozi Adad Rajabu kwamba alihusika na kuchukua baadhi ya Wazanzibar na kuwapeleka Misri (RENDITION) ili wakauwawe huku wakikusishwa na mambo ya Ugaidi. Iwe ni kweli au uzushi, kilichofanyika Zanzibar kinadhihirisha kwamba mambo mabaya yalifanyia.

INGEKUWA NI MWAKA 2024, yale mauaji ndiyo yamefanyika basi fahamu fika kingetokea kama kilichotokea nchini Kenya baada ya machafuko ya 2007-2008, ambapo watu muhimu walishitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC). Tungeshuhudia Raisi Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Sumaye, Waziri wa mambo ya ndani Mohammed Khatib, Mzee Apson Mwang'onda (DGI-TISS), General Robert Mboma (CDF), Inspector Omar Mahita (IGP), Balozi Adad Rajabu, na makada wengine wa CCM na CUF wangekuwa wameshitakiwa kwa aidha makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu (Crimes Against Humanity), AU mauaji ya kimbari (Genocide).

Tena mbaya zaidi ni kwamba Zanzibar has Homogenous Population (Predominantly Muslims) na walioshambuliwa sana ni kabila la Wapemba ambao ni machotara, kesi ingeweza kuthibitisha kwamba kulikuwa na lengo la kuliumiza hili kabila na mambo yakawa mabaya. Hivi jiulize, kama nia ilikuwa ni kudhibiti vurugu, kwanini jeshi la polisi na makachero wake waliamua kuja na mapipa yaliyajaa kinyesi na kuanza kumwaga kwenye visima vya maji, ambavyo watu hutegemea kuendeshea maisha yao ya kila siku ?

ISRAEL, pamoja na KIBURI, UBABE na JEHURI yake yote mwaka huu utakuwa mgumu mno kwao kwasababu ya GAZA. Afrika Kusini wamefungua kesi (ICJ) dhidi ya Israel, ambayo ni ngumu mno kwasababu imejaa ushahidi wa kutosha kuonesha uhalifu mkubwa unafanyika dhidi ya WAPALESTINA. Tayari hukumu ya kwanza ya ICJ imeshatoka (Initial Judgement), na tunasubiria hukumu rasmi ambayo itasema kama kuna mauaji ya kimbari (GENOCIDE) au lah.

ISRAEL, ilishambuliwa vibaya mno na kundi la HAMAS, lakini huwezi kuniambia kwamba kulikuwa na ulazima wowote ule wa kuua watoto na wanawake wasiokuwa na hatia kisa tu unasema ni wahusika. It just appalling and defies the common precepts of descency. Ukweli Israel kama taifa wana haki ya kulinda raia wao, lakini siyo vile. Hii hukumu inaweza ikapuuzwa, lakini siku za mbeleni itakuja kuwaletea matatizo makubwa mno viongozi wa ISRAEL. Hata lile ambalo hawalitaki na kuliogopa, (THE STATE-HOOD OF PALESTINE) linaweza kutokea. Haikuwa na haja ya kutumia nguvu kubwa vile.

NAMALIZA NA HUU MFANO MUHIMU, wakati nasoma chuo tulifanya tathmini kuhusu sheria za Uingereza kipindi cha VITA YA PILI YA DUNIA 1939-1945. Ambapo zilipitishwa sheria kali dhidi ya raia wa Uingereza ambao walionekana kufanya biashara na nchi adui (Trading With Enemies Act), ambapo biashara zote zilifungwa. Bahati mbaya sana raia wengi wa Uingereza wana asili ya Ujerumani (Anglo-Saxons), hivyo ilikuwa ni jambo la kawaida kukuta Muingereza ana familia na biashara nchini Ujerumani.

Sasa mashirika ya kijasusi na jeshi likaanza kukamata watu hovyo na kuwaweka kizuizini wakihusishwa na kushirikiana na maadui (Collaborating with enemies), ukweli wengine walihusika na shughuli za kijasusi na hujuma dhidi ya Uingereza lakini siyo kila aliyekuwa ana asili ya kijerumani basi alitakiwa kuuwawa na kufungwa. Bunge la Uingereza (House of Commons), liliunda sheria ambayo ilimruhusu Waziri kumkamata mtuhumiwa yoyote bila kupita mahakamani wala kupewa haki ya kusikilizwa.

Baadaye wakafahamu kwamba mbali na vita, kama wataruhusu huu UDIKTETA ukajengeka kuwa UTAMADUNI basi hata baada ya vita kuisha nchi inaweza kugeuka kuwa ya kidikteta na wakaja kujuta mno. Hivyo wakaheshimu THE BILL OF RIGHTS, na kutunga sheria nyingine kwamba mbali na kumruhusu Waziri kukamata wahusika, basi watengeneze mahakama maalumu (Special Security Tribunal) ambayo itafanya kazi ya kupima maamuzi ya Waziri na kuhakikisha haki za raia hazivunjwi wakati wote wa mtu kuwekwa kizuizini.

Hili alilofanya UINGEREZA liliwashinda kabisa MAREKANI, ambapo baada ya JAPAN kulipua Pearl Harbour mwaka 1941, Raisi Franklin Delano Roosevelt alisaini amri maalumu (Executive Order 9066) ambayo ilihakikisha kwamba raia wa Marekani 120,000 wenye asili ya JAPAN wanahamishwa kinguvu na kupelekwa kwenye kambi maalumu (CONCENTRATION CAMP) bila kuruhusiwa kutoka. Muigizaji maarufu wa Kimarekani mwenye asili ya Kijapan, Bwana George Takei alikumbwa na hili janga akiwa mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata miaka 10.

==================================================================
UZURI NI KWAMBA, hili andiko langu linapata uhalali dhidi ya wale wahafidhina wataofikiri kilichofanyika kilikuwa ni halali. Raisi Benjamini Mkapa (R.I.P) kabla ya kufariki, kwenye kitabu chake amekiri kwamba ZANZIBAR ni DOA KUBWA lililowahi kutokea kupindi cha utawala wake. Ni jambi jema kama anaonesha majuto, maana kama alichokifanya kingekuwa kizuri na muhimu kwa USALAMA WA NCHI sidhani kama angejutia kwamba ni DOA KUBWA.

Mauaji yale yalichochea hisia mbaya ambazo zimebaki hadi leo, kwamba Raisi Benjamini Mkapa alifanya vile kwasababu alichukia WAISLAMU. Wengine walienda mbali na kusema kwamba kuna viongozi wa KANISA KATOLIKI/MAASKOFU ndiyo walimchochea afanye vile kama ilivyokuwa MWEMBECHAI. Iwe KWELI au UZUSHI, kilichofanyika kilitosha kuweza kuibua hisia mbaya za utengano ndani ya nchi. Vipindi kama hivi ni vya kuwa makini sana kwa watawala kuweza kutuliza hisia na kutulia maana wanaweza kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuwapa adui upenyo wa kufanya PROPAGANDA ZA UZUSHI ambazo zinaweza kuligawa taifa.

===================================================================

RAI YANGU: Mwaka huu 2024 kuna UCHAGUZI MDOGO na mwakani 2025 kuna UCHAGUZI MKUU. Ukizingatia hali ya siasa ilivyokuwepo hapa nchini tokea mwaka 2021 baada ya kifo cha Raisi John Pombe Magufuli (R.I.P), tunapita kwenye kipindi cha UTULIVU WA MUDA (A Calm Before The Storm) ambapo mambo hali ya kisiasa nchini, hasahasa SUALA LA BANDARI, MGAO MKALI WA UMEME na MFUMUKO WA BEI, yameligawa mno taifa KIDINI na KIMUUNGANO kuliko kipindi chochote kile naanza kuelewa siasa.

WATANZANIA tulitoleana maneno ya kasfha za KIDINI na KIKANDA ambayo yalileta hisia mbaya mpaka sasa, bila SERIKALI kuchukua hatua za kukemea kwasababu ilinufaika kisiasa na hali hiyo. Hivyo basi, ndani ya CCM kuna makundi makubwa mno ambayo kwenye msimba wa Mzee Edward Lowass (R.I.P) na ujio wa PAUL MAKONDA yameanza kujionesha kwa wale wenye macho ya ziada ya kufuatilia siasa.

CHONDE-CHONDE WATAWALA, hakikisheni KAULI ZENU mtakazozitoa majukwaani, AMRI ambazo mtawapa maafisa wa vyombo vya dola ziwe na staha. Nashauri mapema kabisa, undeni chombo huru (TUME)na maalumu cha kuwakemea viongozi na wanasiasa wanapotoa kauli hatarishi. TUME hii ipewe kazi ya kusimamia mwendendo wa VIONGOZI na WANASIASA kipindi chote cha CHAGUZI, maana bila kufanya hivyo tunaweza kufika pabaya, maana wanasiasa wanapokuwa kwenye POLITICAL HEAT OF PASSION, huweza kutoa amri au kusema neno ambalo hata hamaanishi ili mradi tu ashinde kwa wakati huo.

VYOMBO VYA DOLA, hakikisheni mnapitia TRAINING MANUALS za maafisa wenye nafasi za juu (Commanding Officers) na kuandaa Terms of Reference (ToRs), ambazo zitahakikisha wanazingatia mambo muhimu na ya msingi kipindi chote tunaelekea chaguzi (2024-2025). Maafisa wafundishwe mambo ya msingi na wawekewe kabisa SPECIAL LEGAL COUNSEL mwenye utaalamu wa LAW ENFORCEMENT, ili kuwaongoza kwenye maamuzi nyeti ambayo yanaweza kuleta taharuki ndani ya nchi.

Hakikisheni, kila maamuzi yanayofanywa na maafisa yanaandikiwa MUHTASARI (Minutes) na kusainiwa na SPECIAL LEGAL COUNSEL, ili mwishoni likitokea tatizo lolote muwepo kwenye mikono salama. Kisheria kuna kitu kiitwacho COMMAND RESPONSIBILITY ambapo, kiongozi wa juu wa jeshi na Mwanasiasa huwajibishwa kwa makosa ya maafisa wao wa chini. Hivyo ili kuhakikisha kwamba uzembe wa maafisa wa chini hauwakuti Maafisa (Commanding Officers) na Wanasiasa (Decision Makers) wa ngazi za juu ni lazima kila amri isainiwe na kuoneshwa kwamba iliridhiwa na SPECIAL LEGAL COUNSEL kwamba ni amri halali isiyovunja sheria na taratibu za haki za binadamu na sheria za usalama.

Kama alivyosema Mzee Cleopa David Msuya, kila MTU ABEBE MZIGO WAKE. Kama ni Raisi wa nchi ndiye atakayetoa amri ya kuua watu basi liwekwe kwenye MUHTASARI ili yakitokea mabaya tufahamu. Kama ni DGI-TISS, IGP au CDF watafanya hivyo basi lazima tufahamu kwenye MUHTASARI. Kama ni MAKADA WAJUAJI WA CCM watafanya hivyo basi tuwafahamu. Kitu kisifanyike bila kuandikwa kwenye MUHTASARI ambao umeridhiwa na SPECIAL LEGAL COUNSEL.

Hatutaki serikali nzima iingie kwenye matatizo na izame kama kule RWANDA 1994 au YUGOSLAVIA 1990's kisa makosa ya watu wachache wenye KIU YA DAMU (BLOOD THIRSTY) na UCHU WA MADARAKA (POWER HUNGRY), ambao wako radhi kufanya lolote lile kwa manufaa yao binafsi, nadhani wakianikwa basi inaweza ikawa hatua ya kwanza katika hatua nyingi ambazo tunatakiwa tuzichukue ili kufika tunakotaka.


AHSANTENI SANA
=============​
 
Mkapa ameshafariki, alichokitanguliza ameshakutana nacho. Pengine kwa Imani ya dini yake kuwauwa waislamu ni jambo jema. Mimi sina ujuzi hapo.

Kuna huyu Bahoseni wa Zanzibar, yeye ni Muislamu, yaliyofanyika ili yeye ashike Dola anayafahamu.


Inasemekana ni sehemu ya makubaliano yake na Maalim (kwa mujibu wa Othman Masoud) kwamba waathirika walipwe fidia, wakati huu ni golden chance kwake kujisafisha na kujipatia kukubalika (political milage) kwa kulipa haki za watu, lakini anakwepa.

Nae akimaliza muda wa uongozi wake au akishakua na cancer or any other chronic condition ndio aje aseme anajuta au anaomba radhi...
 
Mkapa aliomba radhi kwa yaliyojitokeza.
Ishapita kama alijua kosa ,sema hii inaleta picha mbaya na chuki za ndani kutoka kwa wazanzibar ...Sidhani kama wataweza kusahau maana ishu kidogo wanaleta hii ishu public.
 
Shekh eleweka unawatetea wale magaidi kutoka pemba waliokuwa wanapanga njama za kuchinja watu? Tena wakipanga misikitini?

Au israeli kujilinda dhidi ya magaidi ya palestine ni kosa?

Tunapoweka hoja tuweke udini pembeni
 
Shekh eleweka unawatetea wale magaidi kutoka pemba waliokuwa wanapanga njama za kuchinja watu? Tena wakipanga misikitini?

Au israeli kujilinda dhidi ya magaidi ya palestine ni kosa?

Tunapoweka hoja tuweke udini pembeni
Hata Masheikh wa UAMSHO walitishia kuchinja watu, lakini hakuna sehemu ambako Raisi Jakaya Kikwete aliamua kuwahusisha Wazanzibar wote kwa makosa ya wachache. Naamini hujasoma makala yangu yote, hata kama umeisoma basi hujaielewa!​
 
Back
Top Bottom