Migomo Chuo Kikuu cha Dodoma na Maslahi ya Wahadhiri & Wanafunzi

Nimepewa taarifa tena wakati huu kuwa kuna mkutano wa menejimenti unaendelea mapaka wakuu wa skuli wametakiwa kuhudhuria, pia viongozi wa UDOMASA wameitwa. kimsingi walimu wqameamua na kamwe hawatarudi nyuma
 
Kama wataendelea na mgomo wao walioupanga kesho, basi nitaamini kweli UDOM wamebadilika na sasa wapo tayari kupigania masilahi yao na ya jamii inayowazunguka. Kama sikosei, mwaka jana wahadhiri wa vyuo vikuu vyote vya umma waligoma kwa siku kadhaa wakilalamikia mafao duni wanayolipwa na PPF na sababu nyinginezo ila UDOM iliwatenga na wala hawakutaka kugoma nao kama wao siyo waathirika kabisa katika hili. Hii labda itakuwa nafasi yao kuonyesha wameegemea upi
 
Wapi? hao hawathubutu kugoma hata kidogo hapo ndo kumejaa makada wa ccm kuliko hata mzumbe,yaani udom ni sawa na olevel wakati mzumbe ni primary chuo ni kimoja tu ambacho kina critical thinker
 
sitaki kuamini kama UDOM ni CCM.Hivi viongozi wachache wakiwa CCM ndiyo tuamini kuwa UDOM ni CCM mbona pale UDSM kuna akina Makada wengi tu wa CCM.Tatizo ni kwamba hao viongozi wanatumia UDOM kwa maslahi yao binafsi na kutokana na uchanga wa chuo chenyewe akuna anayeweza kuwakosoa kwani naamini japokuwa Mkandala ni CCM hawezi kutumia UDSM kwa manufaa yake binafsi maana watu watampinga kufuatana na taratibu,kanuni na sheria za chuo lakini UDOM haiwezi kutokea tuwaelimishe hao madogo wanawaaribia sifa ya chuo chao na hii ina Ipact sana hata mtaani Mtakumbuka Mzumbe.
 
Safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii udom. Vuta kamba, haki haletewi mtu kwenye kisahani akiwa amekaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!
 
Hizi ni propaganda za kawaida kuwa na sifa kufundisha elimu ya juu ni lazima uwe na GPA ya 3.8. hii ni kwa vyuo vya umma na ni kwa digrii ya kwanza na ukiikosa hii hata uwe na Phd hatakuwa na sifa. Mchakato wa kuajili unahusisha mambo mengi na unahusisha taasisi nyingi za serikali kama vile utumishi na hazina hivyobasi isingekuwa rahisi jambo hilo kujitokeza.

Kuhusu mambo ya kitaifa kama vile Mauaji ya Arusha na Katiba mpya yote haya yameyolewa tamko na kubandikwa katika mbao za matangazio Udom. kwa faida yako tu Wanataaluma wanalaani vikali mauaji hayo na kudai hatua kali zaichukuliwe dhidi ya polisi naviongozi wengine wa serikali wenye dhamana ya jeshi la polisi.

Katiba mpya wanaUdom wanaihitaji na utaratibu muafaka utumike ili katba yenye maslahi sahiihi ya taifa yazingatiwe. Kumbuka mgomo huu uanahalalishwa kwa kuhusisha maslahi ya moja kwa moja kati ya mwajiri na mwajiriwa.

good ndg yangu umewaeleza vizuri sana, tatizo hapa ni mtazamo wa wananchi wengi na wana JF kwamba Udom ni chuo cha ccm, what i knw kinaweza kuwa initiated na ccm bt waliomo ndani wakawa sio wana ccm,
wakuu mnapochangia msiangalie tu perception zenu za zamani bila kuangalia yanayoendelea sasa na mtazamo wa baadae. Mwanza zamani ilikuwa ngome ya ccm, lakini sasa upinzani upo juu sana, so msiihukumu Udom kwa mtazamo wa zamani angalieni muv zao zao za sasa.
Mchambuzi mzuri ni yule anaengalia nyuma, tulipo na tunapokwenda.
 
Wapi? hao hawathubutu kugoma hata kidogo hapo ndo kumejaa makada wa ccm kuliko hata mzumbe,yaani udom ni sawa na olevel wakati mzumbe ni primary chuo ni kimoja tu ambacho kina critical thinker
Usiongee utadhani wewe peke yako unafahamu mazingira ya vyuo vyote. Inaelekea haujui hata taratibu za mgomo, kimsingi hatua zote za awali zimekamilika ikiwepo na wanajumuiya kutoa azimio la kugoma kuanzia kesho asubuhi . subiri ujionee mwenyewe
 
Unafikiri usipowaunga mkono utawapunguzia chochote? wao wameshadhamiria kugoma ili watimiziwe madai yao na wala hawakuombi wewe ridhaa ili wagome. Wewe unafikiri utawaunga vipi mkono wakati wao wanagoma kuingia madarasani, wewe ni miongoni mwa watu wengi wanaojiita great thinkers wakati uwezo wao wa kufikiri uko below average. Wewe great thinker na akili zako unawweza ukaamini kwamba wanafunzi wa chuo kikuu na walimu wao ni wafuasi wa CCM?????????? Great thinker mzima unayumbishwa na propaganda za kisiasa zinazotumiwa na ccm kuuaminisha umma kwamba wana UDOM ni wafuasi wa CCM. Unaamini kwamba wanafunzi wa UDOM walimchangia kikwete pesa za kuchukulia fomu za uraisi na pia unaamini wanafunzi wa udom walilaani walkout ya wabunge wa chadema dhidi ya kikwete!!! Wengine wanaenda mbali na kulaani wanafunzi na waalimu wa udom kumpa kikwete digrii ya heshima, wanashindwa kuelewa kwamba digrii ya heshima inatolewa na baraza la chuo ambalo kwa asilimia kubwa linaundwa na wateule wa rais kikwete na hivyo walikua wakilipa fadhila. Nawashauri walimu wa udom waendelee na harakati zao za mgomo tena waende zaidi ya hapo na kutafuta wana habari makini kama kubenea ili wafichue uozo uliopo pale maana nasikia pesa nyingi za walimu na wafanyakazi wengine zimefanyiwa UFISADI wa hali ya juu na uongozi wa chuo ambao tangu jana na leo juma pili umekua ukifanya vikao kuona jinsi gani watauzima mgomo na kuficha skendo inayowakabili.
 
UDOM Poleni, kwa vyovyote vile, hata kama ni wanafiki, au ni wa sisiem, au ni mradi mkubwa kwa nchi maskini kama Tanzania na mengine mengi yaliyosemwa, nawaomba UDOM wafanye kweli na wala wasirudi nyuma, kama ni mgomo gomeni mpaka, kieleweke, kwani mkiandamana tu, mtapigwa risasi.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kuwa Serikali inasimama waziwazi na kusema kuwa ina pesa za kuilipa Dowans, wakati member wengine wa Serikali hiyohiyo pamoja na Bunge lililopita, walisema kuwa ni Kampuni zenye utata kama si za (Mafisadi), halafu serikali hiyohiyo inakosa pesa za kuwalipa wafanyakazi wa UDOM, watu wanaofanya kazi za kufuta umasikini kwa watanzania. Kwa kweli enough is enough. UDOM gomeni mpaka mlipwe, naona sasa hii serikali inataka kuwafanya watanzani wote ni mbumbumbu.
 
well said Magafu, kweli wakichelewa kidogo tu hizo pesa zote zinakwenda kwa DOWANS,duh tz kuna kazi wala sio ndogo
Hao na wanafunzi wao si ndo walikuwa wanampongeza Kikwete? Si ndo hao waliompa digrii ya heshima juzijuzi tu au ni wengine? Si ndo hao walikuwa wanaeleza mafanikio ya UDOM kwa muda mchache kwa mbwembwe na kejeli kubwa ? SIyo ninyi hao hao mnaowabeza vyuo vingine kwenye vyombo vya habari? Leo mnageuka mgome ili nani awaunge mkono?

Well, mna haki ya msingi kudai na kushinikiza malipo yenu. Mkichelewa fedha zote zinaenda kwa DOWANS... mtakaa kwenye foleni hadi 2020!!
 
Sio chuo bomu kama unavyosema japokuwa nakuunga mkono kwamba DVC-PFA prof SHABAN MLACHA ndio chanzo kikuu cha matatizo pale UDOM. J amaa amekiharibu kabisa kile chuo na amekifanya kama chuo chake eti kisa watu wanadai ameoa mji mmoja na JK!!!!!!!!! Hata huo mgomo wa jumatatu chanzo ni huyo jamaa na kutokana na kiburi chake anawaambia walimu wengine eti wamepelekwa na njaa zao UDOM.
 
Hakuna lolote!waliomchangie hela ya 4rm kina nani?c wanafunzi?chuo cha uma anachotembelea jeykey ni kipi?zaid ya UDOM?hko chuo kuanzia wanafunz had wahadhri hasa wale wa utawala ni politicianz,mcpoangalia mtaajiriwa na serikali 2,

Hakuna ukweli hapo!!!waliomchangia hela za 4m ni wanasisiem wenzake waliopo udom!!kumbuka Tanzania yetu haimzuii mtu kufanya jambo ilimradi asivunje sheria!ONDOENI fikra finyu kwamba Udom wote ni politician wenye mlengo wa sisiem!kuna wanamapinduz wa ukweli UDOM kama hao walimu na wanafunzi pia!Tuwaunge mkono kuliko kutetea ufsad!!
 
Hakuna lolote!waliomchangie hela ya 4rm kina nani?c wanafunzi?chuo cha uma anachotembelea jeykey ni kipi?zaid ya UDOM?hko chuo kuanzia wanafunz had wahadhri hasa wale wa utawala ni politicianz,mcpoangalia mtaajiriwa na serikali 2,
Jeykey anatembelea UDOM mara nyingi kwa sababu kuna vibaraka wake pale!hau ndo hawatakiwi pale au laa wabadirike!!Jamani tushirikiane kutokomeza ufisadi na unyanyasaji Tanzania!!Tuondokane na fikra finyu eti Udom ni ya sisiem!!hawana chuo hao,UDOM ni ya umma wote wawaTanzania!
 
Hao na wanafunzi wao si ndo walikuwa wanampongeza Kikwete? Si ndo hao waliompa digrii ya heshima juzijuzi tu au ni wengine? Si ndo hao walikuwa wanaeleza mafanikio ya UDOM kwa muda mchache kwa mbwembwe na kejeli kubwa ? SIyo ninyi hao hao mnaowabeza vyuo vingine kwenye vyombo vya habari? Leo mnageuka mgome ili nani awaunge mkono?

Well, mna haki ya msingi kudai na kushinikiza malipo yenu. Mkichelewa fedha zote zinaenda kwa DOWANS... mtakaa kwenye foleni hadi 2020!!

Umenisemea yote yaliyo kuwa moyoni kwangu
 
Hakuna lolote!waliomchangie hela ya 4rm kina nani?c wanafunzi?chuo cha uma anachotembelea jeykey ni kipi?zaid ya UDOM?hko chuo kuanzia wanafunz had wahadhri hasa wale wa utawala ni politicianz,mcpoangalia mtaajiriwa na serikali 2,
Jeykey anatembelea UDOM mara nyingi kwa sababu kuna vibaraka wake pale!hau ndo hawatakiwi pale au laa wabadirike!!Jamani tushirikiane kutokomeza ufisadi na unyanyasaji Tanzania!!Tuondokane na fikra finyu eti Udom ni ya sisiem!!hawana chuo hao,UDOM ni ya umma wote wawaTanzania!
 
Hakuna lolote!waliomchangie hela ya 4rm kina nani?c wanafunzi?chuo cha uma anachotembelea jeykey ni kipi?zaid ya UDOM?hko chuo kuanzia wanafunz had wahadhri hasa wale wa utawala ni politicianz,mcpoangalia mtaajiriwa na serikali 2,
Jeykey anatembelea UDOM mara nyingi kwa sababu kuna vibaraka wake pale!hau ndo hawatakiwi pale au laa wabadirike!!Jamani tushirikiane kutokomeza ufisadi na unyanyasaji Tanzania!!Tuondokane na fikra finyu eti Udom ni ya sisiem!!hawana chuo hao,UDOM ni ya umma wote wawaTanzania!
 
UDOM bwana! Haya tuonyesheni musuli wa kuigomea sirikali. Labda mtatu-convince akina Tomaso.

Mwaka juzi tu mlitususia sisi tuliopanga kudai mafao bora ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom