Nyumba moja????? Fafanua,..
Jamani mnyonge mnyongeni haki yake apewe, hawa wafanyakazi hawajawahi kujihusisha na CCM ushahidi upo wakati wa kampeni yalitolewa mabasi kuwapeleka wafanyakazi katika kampeni kimsingi watu hawakukubali kupanda, pia jambo la muhimu tuelewe ni nani ayetoa digrii ya heshima hili huwa ni jopo la watu wachache sana tutawalaumu bure, mimi ninadhani tungefurahia huu moto unaozidi kuwawakia mafisadi na vibaraka vyaoHao na wanafunzi wao si ndo walikuwa wanampongeza Kikwete? Si ndo hao waliompa digrii ya heshima juzijuzi tu au ni wengine?? Si ndo hao walikuwa wanaeleza mafanikio ya UDOM kwa muda mchache kwa mbwembwe na kejeli kubwa ???? SIyo ninyi hao hao mnaowabeza vyuo vingine kwenye vyombo vya habari???? Leo mnageuka mgome ili nani awaunge mkono???
Well, mna haki ya msingi kudai na kushinikiza malipo yenu. Mkichelewa fedha zote zinaenda kwa DOWANS... mtakaa kwenye foleni hadi 2020!!
Salaam wana jamii forum! Taarifa za uhakika nilizozipata wakati huu kutoka kwa mdau muhimu katika Chuo kikuu cha Dodoma ni Kwamba walimu wameamua kuanza mgomo kushinikiza madai yao mbalimbali.
Walimu hao wamefanya mkutano wao leo hii kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili na nusu nao baada ya kupiga kura wote kwa kauli moja isipokuwa watu wanne tu waliamua kuanza mgomo ambao utaendelea mpaka pale madai yao yote yatakapotekelezwa.
Hili ni fundisho kwa uongozi wa kidikteta uliopo hapo chuoni.
Siku zote tunaamini kwamba haki ya mtu haipotei bali huchelewa tu , kimsingi wanaUDOM wamevumilia mengi tangu kuanzishwa kwa chuo mwaka 2007.
Hiki ni chuo pekee cha uma ambacho wafanyakazi wake wote hawajawahi kulipwa pesa ya kujikimu.
Hii ni Taasisi pekee amabayo wafanyakazi wanalipwa mshahara pungufu ya ule unaoonekana katika payroll kutoka hazina.
Hii ni taasisi pekee ambayo salary slip za wafanyakazi ni siri na uongozi wa chuo kuamua kujitengenezea salary slip zake, hali hii ya kugushi salary slip imemsababishia mwalimu mmoja kuwekwa mahabusu akituhumiwa kwamba ni tapeli baada ya kuonesha salary slip ambayo haitambuliki kisheria.
Hii ni taasisi pekee ambayo wafanyakazi wake 409 hawapo katika payroll ya hazina na matokeo yake wafanyakazi waliopo katika payroll inaaminika ndio wanajikikuta wanakatwa mishahara kugharamia wenzao.
Hii ni taasisi pekee ambayo kuna urasimu wa ajabu katika jambo lolote linalohusu pesa hata kama mtu anastahili.
Hii ni taasisi pekee ambayo mshahara mpya umekuja kutoka hazina toka novemba mwaka jana lakini mpaka sasa wanalipwa mshahara wa zamani ambao hata huo nao umechakachuliwa kwa mujibu wa viambatanisho na taarifa za siri amabazo walimu wanazo. Hata katika mwezi huu wameambiwa wasitegemee kupata mshahara mpya.
Siku zote niliamini kwamba UDOM ni bomu linalosubiria kupasuka kwani wakati wake wa kupasuka ndio huu sasa. Wahenga wetu walisema kimya kingi kina mshindo mkuu, wengi waliiangalia Udom kwa jicho la dharau na mabezo kutokana na ukimya wake wakati umefika mjusi amegeuka kuwa nyoka.
Ninakushukuru mdau kwa taarifa hii nyeti sana waandishi wa habari mnakaribishwa Chimwaga siku ya jumatatu asubuhi, kuanzia saa moja na nusu walimu wataendele na mikutano isiyoisha pasipo kuingia darasani huku wakweka mikakati, Taarifa zaidi zinapatikana kwa viongozi tu wa chama cha wanataaluma chuoni hapo kinachoitwa UDOMASA

Jamani mnyonge mnyongeni haki yake apewe, hawa wafanyakazi hawajawahi kujihusisha na CCM ushahidi upo wakati wa kampeni yalitolewa mabasi kuwapeleka wafanyakazi katika kampeni kimsingi watu hawakukubali kupanda, pia jambo la muhimu tuelewe ni nani ayetoa digrii ya heshima hili huwa ni jopo la watu wachache sana tutawalaumu bure, mimi ninadhani tungefurahia huu moto unaozidi kuwawakia mafisadi na vibaraka vyao
Ninachoomba tuzingatie ni haja ya kufanya utafiti kabla ya kufikia mahitimisho haya. Ninaamini wengi mna watu mnaowafahamu hapo udom hata na misimamo yao,Itakuwa ni kichekesho kuwaunga mkono, UDOM !! wasaliti wakubwa hao.