Mawazo ya Wadau wa Twitter Spaces ya JamiiForums kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali iliyosomwa 15/06/2023

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1686854964204.jpeg

Bajeti Kuu ya Serikali 2023/2024 imesomwa leo Juni 15, 2023. Baada ya tukio hili tutakuwa na Mjadala Maalumu kujadili iwapo Bajeti hiyo inagusa mahitaji na hali halisi ya maisha ikilinganishwa na Bajeti ya 2022/23

Usikose kujiunga nasi katika Mjadala huu pamoja na Wataalamu wa Uchumi, Juni 16, 2023, Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku, kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

Pia unaweza kuweka maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala

Kushiriki bonyeza: https://twitter.com/i/spaces/1OdKrzWMdRqKX

Karibuni

---

- Mjadala umeanza kushiriki gusa link hii hapa chini

https://twitter.com/i/spaces/1OdKrzWMdRqKX

Baadhi ya Mawazo yaliyotolewa na Wadau mbalimbali
1686929536879.png

Mwaitenda Ahobike (Mwanasheria): Kwa mwaka huu Tsh. Trilioni 23 zinaenda kwenye mambo ya utawala, ni Tsh. Trilioni 21 tu zinaenda kwenye huduma za maisha ya watu.

Unajiuliza watu wanaotaka waboreshe maisha ya watu, kama vijana zaidi ya laki 8 wanaingia kwenye ajira wanatengewa pungufu ya fedha tofauti na mwaka jana.

Ukitaka kuboresha maisha ya watu lazima uangalie mgawanyo, kwa mfano Tanzania watu zaidi ya 70% wapo kwenye kilimo na 5% wapo kwenye huduma.

Hoja yangu ni kuwa unavyotaka kuboresha maisha ya watu haitakiwi uhusiano usiwe na hasi ya kile ambacho umekipanga. Bajeti inakwenda kwenye kundi dogo la watu, unawaacha watu wengi kwenye wimbi la umasikini. Unaweza kuboresha huduma za afya na elimu, siyo bora bali zitakuwa zinapatikana bure.

Mwaitenda Ahobike (Mwanasheria): Uchumi wetu mwinginupo kwenye mazingiza ambayo hayana taarifa rasmi (informal data), mfano mtu yupo kijijini anafanya mambo yake ya kilimo lakini hakuna anayejua anavyozalisha kwa mwaka.

Ndiyo maana kupata taarifa inakuwa ngumu kwa kuwa 70% watu wapo kwenye mazingira hayo ambayo hayana taarifa rasmi.

Mwaitenda Ahobike: Katika hii bajeti ya Mwaka 2023/24 Serikali imeshindwa kuondoa tozo mbalimbali, hakuna vyanzo vingi vya kuingiza kodi, Bajeti inategemea vilevile ambavyo tumezizoea. Mfano, kukamatana mashati na wafanyabiashara na sijaona ubunifu wa Serikali kuingiza fedha

Mwaitenda Ahobike: Waziri ametutajia kwamba kuna ongezeko la Graduates lakini hajatutajia Kiwango cha Elimu inayotolewa nacho kimebadilikaje

Tumetoka kupiga kelele kwamba Vifaa vya Ujenzi vimepanda bei lakini Saruji imeongezewa bei hapo wakati tunasema tunataka kumboreshea Maisha Masikini

Kupandisha bei ya Mafuta nako Wanasema hilo ongezeko wanataka kupeleka kwenye Miradi mikubwa ndio ni jambo zuri lakini kunaenda kumuathiri moja kwa moja yule ambaye unasema unataka kumboreshea Maisha.

Mwaitenda Ahobike: Hatujatengeneza njia pana za kuongeza walipa kodi, kila Mwaka wanakuwa ni walewale wanabanwa.

Kitu kingine ni kuwa tunawabana Watu wenye nia ya kufanya Biashara na kuingizia pato Taifa-Mfano Mtu akitaka kuanzisha Biashara anaulizwa faida yako iatakuwa Tsh ngapi?

Yaani hata Biashara hajaanza anaulizwa kuhusu faida atakayopata, ndio maana wengi wanakimbia kulipa.

Mwaitenda Ahobike: Kuna Mazingira mengi ya changamoto za kimfumo, unakuta Mtu unaenda kulipa kodi unaambiwa Mfumo upo chiniUnaweza kusubiri muda mrefu na hautapata Huduma, ndio maana unakuta Mtu anaondoka au anatafuta njia za mkato za kulipa hela anayodaiwa, matokeo yake ni kutengeneza Mazingira ya Rushwa.

Mwaitenda Ahobike: Mfumo wa kodi Kenya wapo tofauti, upo katika Mfumo mmoja na ule wa KRA ambayo ni kama TRA ya kuleHauna ulazima wa kwenda kujaza fomu ofisini, unaweza kufanya kwa njia ya Simu.

Mwaitenda Ahobike: Kwenye Bajeti hii kuna hoja ya kulipia Cheti cha Ubachela na kuna kulipia Cheti cha ‘Mchepuko’, sasa sijui ukishalipia nini kinafuata?Hata Talaka ilikuwa unalipia Tsh. 20,000 sasa hivi imepanda na kuwa Tsh. 40,000, nadhani haya mambo ya kijamii naona ni magumu

Mambo mazuri ya Bajeti kwa mujibu wa Mwaitenda Agobike

Mwaitenda Ahobike: Wamefanya jambo zuri upande wa kodi na inapotokea kwenye suala la malipo kuwe na mfumo mmoja tu. Badala ya kupoteza muda kuwa na mfumo wa kukusanya kodi kwa mambo mengi kama ilivyo sasa, hilo ni jambo zuri

Jambo lingine zuri katika Bajeti ni kuondoa afa kwa wale wanafunzi wa kidato cha nne wanaoelekea katika vyuo vya ufundi. Nashauri utaratibu huo unaweza kupelekwa pia katika ngazi ya elimu ya chini mfano wanaomaliza darasa la saba.
---

Mawazo yaliotolewa na Kapila Kavenuke (Mdau wa Twitter Spaces)
1686933605902.png
Kapila Kavenuke: Kawaida Bajeti ni lazima iongezeke ya mwaka iliyopita na inayofuata lazima iwe juu zaidi, pia Bajeti ni mipango unataka kutumia wapi na kwa sababu gani. Asilimia kubwa ya Watanzania wanahusika na Kilimo lakini bado hatuitendei haki kwa kuwa hatuweki fedha nyingi huko

Ukisema Bajeti iwe sawa kwa kila kitu hilo halitawezekana kwa kuwa ni vigumu kubalansi kugawa Fedha kwa kila WizaraNapongeza kupunguza baadhi ya tozo kama vile za kwenye Magari, Pia wanaangalia Miamaka ya Simu na nyingine kadhaa ambazo Watu walipiga kelele.

---
Mawazo yaliyotolewa na Maneshi (Mdau wa Twitter Spaces)
Maneshi: Nimeona wameongeza Tsh. 100 kwenye Mafuta licha ya kusema kuwa kuna ruzuku za Mafuta, ni sawa na kutoa kitu mkono wa kulia kupeleka wa kushotoSidhani kama kuna faida ya walichokifanya.

Kuna vitu ambavyo Serikali walitakiwa kufanyia utafiti kabla ya kupitisha, mfano hizo kodi na tozo ndogondogo, tunaumia ni kwa vile tu Watanzania tunapenda AmaniMfano, Serikali ingewekeza kwenye chakula, uhitaji wa chakula ni mkubwa. Wakate maeneo maalum kwa kilimo na kuwawezesha wakulima kisha wanatengeneza soko maalum la kilimo
---
Mawazo yaliyotolewa na Ray Paaul (Mdau wa Twitter Spaces)
Ray Paaul: Natamani kuwa na mashine ya EFD lakini nikifikiria gharama nakimbia, nina simu ya smart Phone, kwa nini nisiitumie hiyo kufanya shughuli za malipo

Kwa sasa tunalipia umeme, majini na mambo mengine kwa nia ya simu, kwa nini hiyo hali isiwe katika biashara nyingine ili kuongeza walipa kodi?

Hakuna mtu ambaye hapendi kulipa kodi ila mifumo ni mibovu, Serikali itengeneza mazingira mazuri watu wataipa kodi. Mimi nikifikiria kulipa Tsh. 600,000 kulipia mashine ya EFD naona mbona hiyo naweza kuitumia kama mtaji kabisa?
---
Mawazo yaliyotolewa na Geoffrey Nkambi (Mdau wa Twitter Spaces)
Geoffrey Nkambi: Kodi ndio inayosaidia maendeleo ya nchi lakini Wananchi wanalalamika sana kuhusu Mifumo ya KodiMfano, Marekani kuna Kodi na Mifumo yao ipo vizuri kiasi kwamba Mwananchi hawezi kulalamika, hapa kwetu watu wachache wanaamka tu na kaunzisha kodi ambazo zinakuwa juu kuliko uhalisia.

Mtu unaweza kufanya Miamaka lakini makato ni makubwa, Serikali inataka kupata kipato kikubwa kupitia njia chacheMitandaoni kuna biashara nyingi lakini Serikali haikusanyi kodi sehemu nyingi, ingeweza kukusanya huko kidogo kidogo na ingepata mapato mengi-Serikali inatengeneza mazingira ya Watu kukimbia kulipa kodi.

Elimu bila malipo ni jambo zuri lakini tuanagalie ubora wa Elimu husika. Tukiangalia Mtaani kuna kundi kubwa la wahitimu waliomaliza Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu lakini wote wanalia hawana AjiraTunaweza kutengeza Mfumo mzuri wa Elimu ambapo Wakihitimu wanakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe
---

Mawazo ya Thomas Sankara (Mdau wa Twitter Spaces)

Thomas Sankara: Bajeti yetu ina changamoto kama ambayo inatuchanganya Waafrika wengi, tunaamini tuna akili sana kuliko waliotutangulia kutoka mataifa mbalimbali ya nje ya Afrika.

Mataifa machanga kama Tanzania hatukuwa na haja ya kutumia akili nyingi kufika kwenye maendeleo, ilikuwa vizuri tungefanya kama kile waliochanga wenzetu.

Bajeti yetu zaidi ya 50% ya fedha zinazohusika zinaenda kulipa madeni, kile ambacho tunakikusanya ndicho tunakitumia kulipa madeni na katika matumizi mengine ambayo si ya msingi kama vile kununua magari
 
Nimefurahishwa na jambo la kutofunga biashara zote za halali za watu kwa sababu zozote zile , na kwamba zitungwe kanuni za adhabu kwa makosa mbali mbali badala ya kufungia biashara

Hili sikulitegemea kuwekwa kama maelekezo kwenye bajeti hii
 
Serikali itaanza kutoza kodi kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara mtandaoni wafanyabiashara ukiwauliza mambo ya siasa wanajifanya hawana habari nayo siku hiyo sheria ikianza kutekelezwa utasikia vilio kila kona " Mama Samia tusaidie! ! Mama tusaidie"
 
CCM imechoka hadi inatia uvivu kujadili mambo wanayosimamia. Tunawakumbusha kwasababu wapo serious na kubinafsisha basi wasisahau na Bunge kwenye sale list yao.
 
Kama itakuwa sawa! Naishauri serikali jambo hili

Serikali iweke bima ya afya ya msafiri kwa Vyombo vyote vya moto, mabasi, ndege, Meri na treni

Vyombo vyoote vinavyosafirisha Abiria mkoa kwa mkoa, serikali iweke Tsh 1,000 tu ya kila mtu anaposafiri kwenda mikoani, hii iwe kama kodi kwa abiria, kodi hiyo ielekezwe kwenye bima ya afya ya msafiri huyo!

Ikitokea chombo kimepata ajali, abiria aliyesafiri kwa siku hiyo, Bima hiyo itatumika kumtibu abiria huyo hata kama ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusafiri!

Hii itasaidia sana wasafiri kupata matibabu bule pindi inapotokea ajali
 
Bajeti haina jipya.
"SERIKALI HAINAGA HASARA" huu ni msemo maarufu kutoka kwa watumishi wa TRA na taasisi nyingi za serikali. Siku utakapobadilika na kila mtumishi akagundua matendo yake na aina ya utendaji wake wa kazi unaitia HASARA serikali, ile lialia ya waziri kuhusu walipakodi itaisha.
 
Bajeti Kuu ya Serikali 2023/2024 imesomwa leo Juni 15, 2023. Baada ya tukio hili tutakuwa na Mjadala Maalumu kujadili iwapo Bajeti hiyo inagusa mahitaji na hali halisi ya maisha ikilinganishwa na Bajeti ya 2022/23

Usikose kujiunga nasi katika Mjadala huu pamoja na Wataalamu wa Uchumi, Juni 16, 2023, Saa 12 Jioni hadi 2 Usiku, kupitia Twitter Spaces ya JamiiForums

Pia unaweza kuweka maoni yako kwenye uzi huu ambayo yatasomwa siku ya mjadala

Kushiriki bonyeza: https://twitter.com/i/spaces/1OdKrzWMdRqKX

Karibuni

---

- Mjadala umeanza kushiriki gusa link hii hapa chini

https://twitter.com/i/spaces/1OdKrzWMdRqKX

Baadhi ya Mawazo yaliyotolewa na Wadau mbalimbali
View attachment 2659809

Mwaitenda Ahobike (Mwanasheria): Kwa mwaka huu Tsh. Trilioni 23 zinaenda kwenye mambo ya utawala, ni Tsh. Trilioni 21 tu zinaenda kwenye huduma za maisha ya watu.

Unajiuliza watu wanaotaka waboreshe maisha ya watu, kama vijana zaidi ya laki 8 wanaingia kwenye ajira wanatengewa pungufu ya fedha tofauti na mwaka jana.

Ukitaka kuboresha maisha ya watu lazima uangalie mgawanyo, kwa mfano Tanzania watu zaidi ya 70% wapo kwenye kilimo na 5% wapo kwenye huduma.

Hoja yangu ni kuwa unavyotaka kuboresha maisha ya watu haitakiwi uhusiano usiwe na hasi ya kile ambacho umekipanga. Bajeti inakwenda kwenye kundi dogo la watu, unawaacha watu wengi kwenye wimbi la umasikini. Unaweza kuboresha huduma za afya na elimu, siyo bora bali zitakuwa zinapatikana bure.

Mwaitenda Ahobike (Mwanasheria): Uchumi wetu mwinginupo kwenye mazingiza ambayo hayana taarifa rasmi (informal data), mfano mtu yupo kijijini anafanya mambo yake ya kilimo lakini hakuna anayejua anavyozalisha kwa mwaka.

Ndiyo maana kupata taarifa inakuwa ngumu kwa kuwa 70% watu wapo kwenye mazingira hayo ambayo hayana taarifa rasmi.

Mwaitenda Ahobike: Katika hii bajeti ya Mwaka 2023/24 Serikali imeshindwa kuondoa tozo mbalimbali, hakuna vyanzo vingi vya kuingiza kodi, Bajeti inategemea vilevile ambavyo tumezizoea. Mfano, kukamatana mashati na wafanyabiashara na sijaona ubunifu wa Serikali kuingiza fedha

Mwaitenda Ahobike: Waziri ametutajia kwamba kuna ongezeko la Graduates lakini hajatutajia Kiwango cha Elimu inayotolewa nacho kimebadilikaje

Tumetoka kupiga kelele kwamba Vifaa vya Ujenzi vimepanda bei lakini Saruji imeongezewa bei hapo wakati tunasema tunataka kumboreshea Maisha Masikini

Kupandisha bei ya Mafuta nako Wanasema hilo ongezeko wanataka kupeleka kwenye Miradi mikubwa ndio ni jambo zuri lakini kunaenda kumuathiri moja kwa moja yule ambaye unasema unataka kumboreshea Maisha.

Mwaitenda Ahobike: Hatujatengeneza njia pana za kuongeza walipa kodi, kila Mwaka wanakuwa ni walewale wanabanwa.

Kitu kingine ni kuwa tunawabana Watu wenye nia ya kufanya Biashara na kuingizia pato Taifa-Mfano Mtu akitaka kuanzisha Biashara anaulizwa faida yako iatakuwa Tsh ngapi?

Yaani hata Biashara hajaanza anaulizwa kuhusu faida atakayopata, ndio maana wengi wanakimbia kulipa.

Mwaitenda Ahobike: Kuna Mazingira mengi ya changamoto za kimfumo, unakuta Mtu unaenda kulipa kodi unaambiwa Mfumo upo chiniUnaweza kusubiri muda mrefu na hautapata Huduma, ndio maana unakuta Mtu anaondoka au anatafuta njia za mkato za kulipa hela anayodaiwa, matokeo yake ni kutengeneza Mazingira ya Rushwa.

Mwaitenda Ahobike: Mfumo wa kodi Kenya wapo tofauti, upo katika Mfumo mmoja na ule wa KRA ambayo ni kama TRA ya kuleHauna ulazima wa kwenda kujaza fomu ofisini, unaweza kufanya kwa njia ya Simu.

Mwaitenda Ahobike: Kwenye Bajeti hii kuna hoja ya kulipia Cheti cha Ubachela na kuna kulipia Cheti cha ‘Mchepuko’, sasa sijui ukishalipia nini kinafuata?Hata Talaka ilikuwa unalipia Tsh. 20,000 sasa hivi imepanda na kuwa Tsh. 40,000, nadhani haya mambo ya kijamii naona ni magumu

Mambo mazuri ya Bajeti kwa mujibu wa Mwaitenda Agobike

Mwaitenda Ahobike: Wamefanya jambo zuri upande wa kodi na inapotokea kwenye suala la malipo kuwe na mfumo mmoja tu. Badala ya kupoteza muda kuwa na mfumo wa kukusanya kodi kwa mambo mengi kama ilivyo sasa, hilo ni jambo zuri

Jambo lingine zuri katika Bajeti ni kuondoa afa kwa wale wanafunzi wa kidato cha nne wanaoelekea katika vyuo vya ufundi. Nashauri utaratibu huo unaweza kupelekwa pia katika ngazi ya elimu ya chini mfano wanaomaliza darasa la saba.
---

Mawazo yaliotolewa na Kapila Kavenuke (Mdau wa Twitter Spaces)
View attachment 2659901
Kapila Kavenuke: Kawaida Bajeti ni lazima iongezeke ya mwaka iliyopita na inayofuata lazima iwe juu zaidi, pia Bajeti ni mipango unataka kutumia wapi na kwa sababu gani. Asilimia kubwa ya Watanzania wanahusika na Kilimo lakini bado hatuitendei haki kwa kuwa hatuweki fedha nyingi huko

Ukisema Bajeti iwe sawa kwa kila kitu hilo halitawezekana kwa kuwa ni vigumu kubalansi kugawa Fedha kwa kila WizaraNapongeza kupunguza baadhi ya tozo kama vile za kwenye Magari, Pia wanaangalia Miamaka ya Simu na nyingine kadhaa ambazo Watu walipiga kelele.

---
Mawazo yaliyotolewa na Maneshi (Mdau wa Twitter Spaces)
Maneshi: Nimeona wameongeza Tsh. 100 kwenye Mafuta licha ya kusema kuwa kuna ruzuku za Mafuta, ni sawa na kutoa kitu mkono wa kulia kupeleka wa kushotoSidhani kama kuna faida ya walichokifanya.

Kuna vitu ambavyo Serikali walitakiwa kufanyia utafiti kabla ya kupitisha, mfano hizo kodi na tozo ndogondogo, tunaumia ni kwa vile tu Watanzania tunapenda AmaniMfano, Serikali ingewekeza kwenye chakula, uhitaji wa chakula ni mkubwa. Wakate maeneo maalum kwa kilimo na kuwawezesha wakulima kisha wanatengeneza soko maalum la kilimo
---
Mawazo yaliyotolewa na Ray Paaul (Mdau wa Twitter Spaces)
Ray Paaul: Natamani kuwa na mashine ya EFD lakini nikifikiria gharama nakimbia, nina simu ya smart Phone, kwa nini nisiitumie hiyo kufanya shughuli za malipo

Kwa sasa tunalipia umeme, majini na mambo mengine kwa nia ya simu, kwa nini hiyo hali isiwe katika biashara nyingine ili kuongeza walipa kodi?

Hakuna mtu ambaye hapendi kulipa kodi ila mifumo ni mibovu, Serikali itengeneza mazingira mazuri watu wataipa kodi. Mimi nikifikiria kulipa Tsh. 600,000 kulipia mashine ya EFD naona mbona hiyo naweza kuitumia kama mtaji kabisa?
---
Mawazo yaliyotolewa na Geoffrey Nkambi (Mdau wa Twitter Spaces)
Geoffrey Nkambi: Kodi ndio inayosaidia maendeleo ya nchi lakini Wananchi wanalalamika sana kuhusu Mifumo ya KodiMfano, Marekani kuna Kodi na Mifumo yao ipo vizuri kiasi kwamba Mwananchi hawezi kulalamika, hapa kwetu watu wachache wanaamka tu na kaunzisha kodi ambazo zinakuwa juu kuliko uhalisia.

Mtu unaweza kufanya Miamaka lakini makato ni makubwa, Serikali inataka kupata kipato kikubwa kupitia njia chacheMitandaoni kuna biashara nyingi lakini Serikali haikusanyi kodi sehemu nyingi, ingeweza kukusanya huko kidogo kidogo na ingepata mapato mengi-Serikali inatengeneza mazingira ya Watu kukimbia kulipa kodi.

Elimu bila malipo ni jambo zuri lakini tuanagalie ubora wa Elimu husika. Tukiangalia Mtaani kuna kundi kubwa la wahitimu waliomaliza Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu lakini wote wanalia hawana AjiraTunaweza kutengeza Mfumo mzuri wa Elimu ambapo Wakihitimu wanakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe
---

Mawazo ya Thomas Sankara (Mdau wa Twitter Spaces)

Thomas Sankara: Bajeti yetu ina changamoto kama ambayo inatuchanganya Waafrika wengi, tunaamini tuna akili sana kuliko waliotutangulia kutoka mataifa mbalimbali ya nje ya Afrika.

Mataifa machanga kama Tanzania hatukuwa na haja ya kutumia akili nyingi kufika kwenye maendeleo, ilikuwa vizuri tungefanya kama kile waliochanga wenzetu.

Bajeti yetu zaidi ya 50% ya fedha zinazohusika zinaenda kulipa madeni, kile ambacho tunakikusanya ndicho tunakitumia kulipa madeni na katika matumizi mengine ambayo si ya msingi kama vile kununua magari
Bajeti hii haina tofauti na zilizopita kwa kuwa utayarishaji wake na uwasirishi Bungeni ni ule ule. Zifuatazo ni hoja zangu:

1) Mapato na Matumizi: kuna taarifa kuwa kiasi kinachopangwa kwa matumizi, hasa miradi ya maendeleo huwa akitolewi chote. Bajeti haijaeleza sababu za kutokufikia malengo ya mapato na ni sehemu zipi ziliathirika kwa mgao wa bajeti pungufu.

2) Ulianzishwa utaratibu wa kila Wizara kusoma bajeti yake na ikapitishwa na Bunge kabla ya Bajeti kuu. Bajeti hiyo haijaonesha ni kwa kiasi gani Bajeti za Wizara zinarandana na Bajeti au mipango ipi katika bajeti za kila Wizara hazikutengewa fedha au fedha kidogo na kwa sababu gani.

Natumaini Wabunge watakaporejea kujadili hiyo bajeti watatilia maanani hoja zangu
 
Back
Top Bottom