Tanzania Inategemea Wahisani Kuendesha Bajeti ya Fedha

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2023/2024 ni Tsh trilioni 44.38, sawa na $17.6 bilioni. Mafungu makubwa mawili ya fedha zilizotengwa ni ulipaji madeni na uendeshaji wa shughuli za utawala.

Bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2023/2024 Katika fedha hizo Tsh trilioni 6.31 zitatumika kulipa deni la taifa, huku Tsh trilioni 11.89 zitapelekwa kutoa huduma ya utawala. Hizo ni Tsh trilioni 18.2.

Katika mpango wa bajeti ya mwaka 2024/25 serikali ya Tanzania imeeleza bungeni kwamba; washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Tsh trilioni 4.29 na mikopo ni Tsh trilioni 8.3. Bajeti TEGEMEZI.

Bajeti inayopitishwa na bunge haifanani na bajeti inayotekelezwa na serikali. Makadirio ya mapato ni makubwa kuliko mapato halisi. Bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni TEGEMEZI.

Matumizi ya kawaida ni makubwa kuliko mapato ya serikali. Mapato ya ndani hayachangii miradi ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea misaada na mikopo kutoka nje ya Tanzania.

Serikali ya Tanzania inakusanya asilimia 12.3 ya pato la Taifa kama kodi (mapato ya serikali). Serikali ya Tanzania inategemea zaidi misaada ya wahisani kwa asilimia 40 katika bajeti zake za mwaka wa fedha.

Kitendo cha serikali ya Tanzania kutegemea bajeti za nchi wahisani ni aibu kubwa na ndiyo msingi wa bunge la Ulaya kuwa na nguvu ya kupiga kura kuamua mambo ya Tanzania. Kwa kuwa wanatoa fedha zao.

Tanzania ni nchi tajiri kwa rasilimali na malighafi. Ni ajabu sana kuwa tegemezi kwa wakoloni. Serikali inafikiri njia pekee ya kukusanya mapato ni kuongeza tozo na kodi na kwenda kwa wakoloni kukopa.

Benki ya Dunia (WB) katika mpango wake wa The Global Program on Sustainability (GPS) wanachangia fedha katika bajeti kuu ya Tanzania kuipa Tanzania katika kupambana na msukosuko wa uchumi.

Kulipa madeni ya nje si kazi rahisi. Na kadiri unavyozidi kuwa na deni kutoka nje ndivyo utakavyokuwa umefungwa katika malengo yako ya ukuaji. Tsh trilioni 6.31 zitatumika kulipa deni la taifa

Kama wakoloni wanakupa fedha kila bajeti ili kusaidia kuokoa uchumi wako, utawakataza wasiingilie mambo yako ya ndani na kupiga kura za maamuzi? Thomas Sankara: “he who feeds you, controls you”

Mwalimu J.K. Nyerere alisisitiza, ukitaka kuwa huru jitegemee. “Uhuru ni kujitegemea”. Tanzania kama Taifa linahitaji kutumia rasilimali zake zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya watu wake, siyo watawala tu.

Kuanzia miradi ya maji, shule, hospitali, barabara unajengewa na wakoloni. Vifaa tiba, taa za barabarani unapewa na wakoloni. Utawazuia vipi wasikupangie mambo yako? Wakoloni wataendelea kuwatawala.

Unatembea au kuendesha gari yako katika barabara ambayo kwa asilimia 90 imejengwa au kufadhiliwa na fedha za watu wa Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Korea, Norway na bado unapata ufahari?

Unapokuwa tegemezi kwa watu wa nje, basi tarajia kudhibitiwa kiuchumi. Huwezi kuwa huru tena. Fedha zako, mipango yako. Ukiwa huwezi kujiendesha kwa fedha zako za ndani, wakoloni watakupangia tu.

Kwa mantiki hiyo, huwezi kuwazuia kuingilia masuala ya ndani na kupiga kura kuwatetea Maasai ambao Serikali ya Tanzania inawahamisha katika makazi yao ya asili, Ngorongoro na kuwapeleka Msomera.
Chanzo:

Brigedia Mtikila, MMM.
 
Kila kitu huhitaji akili, maarifa na uadilifu. Vyote vimekosekana kwa watawala wa Tanzania. Wanachowaza wakati wote ni kuiba maamuzi ya wananchi ili waendelee kutawala na kuiba.
 
Mungu wabariki Wazungu
 
Back
Top Bottom