Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa Fedha unaokuja 2024/2025 ni kuwa bajeti ya Matumizi ya Kawaida kufikia ukomo wa Shilingi tilioni 33 na bajeti ya Maendeleo kufikia ukomo wa tilioni 15.
Sababu zinazofanya bajeti ya matumizi ya kawaida iwe kubwa.
1. Uchaguzi wa Serikali za Mtaa unaofanyika mwaka huu. Ili kila Mtanzania apate haki yake ya Kikatiba fedha zinahitajika kufanikisha zoezi hili katika mandalizi.
2. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Asilimia 95 ya mandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 maandalizi yanabebwa na Bajeti ya 2024/2025.
3. Maono na Mtazamo wa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan kupunguza mikopo ya nje na ndani na kuongeza jitihada za kulipa madeni ambayo Taifa linadaiwa (madeni haya ni ya kuanzia awamu zilizopita).
4. Kwa kuwa Tanzania tunategemea pia kuwa mwenyeji wa AFCON, ukiachana na Fedha za Maendeleo za ujenzi wa Viwanja etc..ili kufanikisha jambo hili maandalizi yake yataanza mapema sana ambapo ni lazima Serikali itenge fedha ya matumizi ya kawaida kwa ajili ya hili.
N.B Ni muda sahihi sasa kwa Wizara ya Michezo kuhamasisha wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye Viwanja vya mpira hata kama ni kwa kuweka punguzo zaidi na msamaha wa kodi katika hili.
5. Itaendelea.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania