Tusome kidogo Bajeti ya Serikali yetu ili tunapodai uwajibikaji na haki tujue tunadai nini

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,912
Ni Jumatatu Nyingine Mahususi kabisa ambayo ni ya kwanza kwa mwezi huu wa February wa mwaka 2024.Nikiwa hapa Ofisini kwangu na mshahara ukiwa bado haujatoka. Pamoja na andiko hili naambatanisha link ya ukurasa ambao utakupatia vitabu vya Bajeti vya Serikali yetu ili tujue Pesa yetu inapelekwa wapi? Nasisitiza kwamba ni Pesa zetu hivyo basi ni muhimu tuone kama PESA zetu zinatumika namna tunavyotaka.

Hii ni link: Budget Books 2023/2024 | MoF - Ministry of Finance

Najua wengi watajiuliza kwa nini ninaleta Mjadala huu? Ukweli ni kwamba muda sio mrefu tutaanza kusikia Habari za ripoti ya CAG mara tutasikia maandalizi ya Bajeti ya 2024/25. Haya maamuzi yanayofanywa na serikali yana athari za moja kwa moja katika maisha yako. Hivyo basi ni muhimu uelewe na ufuatiliaje. Baada ya andiko hili nitawaalika wale ambao wanaweza waende katika ofisi za Kata zao na Halmashauri na Hata Ofisi za Mkoa waombe Taarifa za Mapato na Matumizi ili wajue PESA zinazoingia ni kiasi gani na zimetumikaje na kwa watakaoweza wafuatilie mpaka kwenye miradi husika ili kufahamu iwapo kweli PESA yetu Imetumika kama inavyotakiwa.

Sasa Nirudi kwenye Mjadala wa msingi.

Kwa kawaida Bajeti ya Serikali ya Tanzania huenda sambamba na mwaka wa fedha wa serikali ambao huanza Julai 1 hadi Jun 30 Mwaka unaofuata.Kwa mfano mwaka wa fedha 23/24 Utaisha Juni 30 2024 Kisha tutanza mwaka wa fedha wa 24/25. Ripoti ya CAG tutakayopatiwa Mwaka huu ni ya mwaka wa Fedha 22/23 ambao uliisha Juni 30 2023.

Bajeti ya Serikali ya Tanzania Huandaliwa katika Makundi mawili ambayo ni Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Bajeti ya Maendeleo. Hivyo Basi Vitabu Vya Bajeti navyo huwa katika Makundi hayo. Katika Vitabu Hivi Kila eneo la matumizi hupewa VOTE number ambayo ni namba inayotambua eneo ambalo PESA itatumika ambapo kila idara wizara, kitengo na mamlaka inakuwa na VOTE yake.Kwa Mfano.VOTE ya mkoa wa Dar es Salaam ni VOTE 88 na Kiasi cha Pesa kilichotengwa kwa ajili ya Maendeleo kwa mwaka huu wa fedha yaani 23/24 ni kama Bilioni 697.14 za kitanzania. Sasa hii namba ni makadirio tu ambayo yameruhusiwa kwa hiyo Basi Mkoa wa Dar es Salaama Umetengewa Kiasi hicho ila kwa kutegemea Makusanyo mbalimbali kiasi hicho kinaweza kufikiwa.

Ili kufahamu zaidi fuata hio link hapo juu upakue vitabu vya bajet ili uone Kodi yetu inatumikaje? Ili ufurahie zaidi, Tafuta taarifa za makusanyo ya TRA, Halmashauri yako na ukiyasoma kwa Pamoja unaweza pata uchungu ukiona Pesa zinatumika ndivyo sivyo.

Usisahau kuzungumza na Diwani wako iwapo kuna mambo huyaelewi
 
Back
Top Bottom