Majina matatu tume ya kurekebisha katiba toka CHADEMA, nani awemo?

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,381
1,760
Wana CDM ungependa majina yapi kutoka chama cha CHADEMA waingie kwenye mchakato wa kurekebisha katiba.
Mi ningeanza na
1:J.Mnyika
2:T.Lisu na
3:V.nyerere
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa fursa kwa wananchi kupendekeza majina matatu yanayotakiwa kuwasilishwa na chama hicho kwa Rais kwa ajili ya kuunda tume shirikishi ya itakayoandaa rasimu ya Katiba mpya.

Katika hotuba yake ya kila mwezi, Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa vyama vya siasa na vya hiari, taasisi za kidini na kiraia zinazoshiriki katika mazungumzo ya kuandaa mazingira thabiti ya kuunda Katiba mpya, kila moja kumpelekea majina matatu.

CHADEMA kupitia Kamati Kuu jana ilitoa wito kwa wananchi kuwasilisha majina hayo kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa maandishi ama moja kwa moja kwa mkono au kwa rejista ya posta kupitia anuani S.L.P 31191, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Kamati Kuu, majina hayo yawasilishwe kabla ya Machi 11, 2012 yakionyesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapoishi kila muombaji au mpendekezwaji.

Maamuzi hayo yalifikiwa kwenye Mkutano wa Kawaida wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliofanyika kwa siku mbili Machi 3-4, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ice Age-Usa River katika Jimbo la Arumeru Mashariki-Wilaya ya Meru, mkoani Arusha.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ya chama hicho ilipokea na kujadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 iliyoundwa na Kamati Kuu Novemba 20, 2011, ambapo pamoja na masuala mengine, Kamati Kuu ilitaarifiwa kuhusu marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 yaliyofanyika katika Mkutano wa Sita wa Bunge Februari 10,2012.

“Kamati Kuu imezingatia kwamba marekebisho yaliyofanyika ni ya hatua ya kwanza ya kuwezesha kuundwa kwa tume shirikishi ya katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa ripoti na rasimu ya Katiba mpya,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati huohuo Kamati Kuu imesisitiza kwamba marekebisho mengine muhimu yanapaswa kufanyika katika awamu nyingine kuhusu Bunge Maalum la Katiba na hatua ya kutunga Katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Pamoja na hilo Kamati Kuu imeamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho kwa awamu nyingine kuhusu Bunge la Maalum la Katiba na kura ya maoni.

Kamati Kuu ya chama imeendelea kusisitiza kuwa CHADEMA iendelee kutekeleza azimio la kikao cha Kamati Kuu cha Novemba 20, 2011 la “kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi katika hatua zote.

Aidha imepitisha azimio la nyongeza kwamba utekelezaji uhusishe pia kutoa elimu juu ya Katiba ili kuwezesha umma kushiriki ipasavyo kutoa maoni kwa lengo la kuwa na Katiba mpya na bora.

Sanjari na hilo Kamati Kuu imeendelea kuwaagiza viongozi wote wa chama, katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mchakato wa kupata Katiba mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa Watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi.

Chanzo: TANZANIA DAIMA!
 
lissu na mbowe wasitie mguu kabisa wakiwapa pesa hawakawii kutujeuka.apo ni mnyika na Dr slaa
 
Wanachadema wenzangu habari za asubuhi. Tayari viongozi wetu wapendwa wameishatoa wito ili tutoe mapendekezo yetu kuhusu majina matatu yatakayoshirikishwa katika tume ya kutunga katiba. Kutoka moyoni mwangu nampendekeza Dr. Kitila Mkumbo ili atimaye jina lake liwasilishwe kwa rais tayari kushiriki katika tume tajwa hapo juu. Dr. Kitila Mkumbo amesoma Chuo Kikuu Cha D'Salaam amemaliza mwaka 1999. Alikuwa Rais wa Daruso enzi hizo kwa kweli ni kijana ambaye uongozi ulitukuka hakuna ambaye ameweza kuvunja rekodi yake ya uongozi si wanachuo, maprofesa na utawala wa chuo wote walimuheshimu. Hivyo, viongozi wangu Dr. Slaa na Mh Mb Freeman Mbowe nawaomba mpeleke jina hili kwani Dr. Mkumbo ni mtu uwezo wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.
Nawasilisha.
 
  1. Tundu Lissu- Mwanasheria mahiri ambaye amechangia kwa asilimia kubwa sana katika mchakato huu tulionao wa Katiba mpya.
  2. Prof.Baregu Mwesiga- Gwiji wa maswala ya Sayansi ya Siasa(Political Science).
  3. Prof. Abdullah Safari- Gwiji wa maswala ya Sheria na vilevile ataondoa zana ya udini ndani ya CDM kwamba ni chama cha Wachagga na Wakristo tu.

Hii listi itafaa sana kuiwakilisha CHADEMA kwenye hiyo Tume ya Rais ya Kuunda Katiba mpya ya JMT.
 
lissu na mbowe wasitie mguu kabisa wakiwapa pesa hawakawii kutujeuka.apo ni mnyika na Dr slaa
Je hao watu uliowataja wanahistoria ya kufanya vitendo ulivyovitaja au ni chuki binafsi au unaogopa umakini wao na jinsi wanavyopanga hoja zao
 
Hata mimi naunga mkono hoja Dr. Kitila ni mtu makini sana ninamkubali hofu yangu kama atapata baraka ya muajiri wake kupendekezwa kupitia CDM.

Pia ni vema mtui akapendekeza kwa kupeleka maoni pale ofisi za chadema kama kama kamati kuu ilipopendekeza siyo kuishia hapa JF.
 
Wana CDM ungependa majina yapi kutoka chama cha CHADEMA waingie kwenye mchakato wa kurekebisha katiba.
Mi ningeanza na
1:Babu Prof Shivji
2:T.Lisu na
3:Halima Mdee
 
Back
Top Bottom