Majina matatu tume ya kurekebisha katiba toka CHADEMA, nani awemo?

Kwa mujibu wa sheria,wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani hawawezi kuteuliwa kuwa wajumbe wa tume. Ila wanasiasa wengine wote ambao hawana hivyo vyeo wanaweza kuteuliwa. Hivyo, majina kama ya Lissu, Mnyika, Mdee, tayari sheria imewaweka kando.
 
Nawapendekeza wafuatao.

1. Prof. Baregu
2. prof. Safari
3. Dr. mkumbo
 
Ingekuwa wabunge wanaruhusiwa ningesisitiza sana lissu achaguliwe na mdee bt stil wapo watu makini i suggest
1.mabere marando
2.prof.safari
3.dr.kitila mkumbo
 
Hata mimi naunga mkono hoja Dr. Kitila ni mtu makini sana ninamkubali hofu yangu kama atapata baraka ya muajiri wake kupendekezwa kupitia CDM.

Pia ni vema mtui akapendekeza kwa kupeleka maoni pale ofisi za chadema kama kama kamati kuu ilipopendekeza siyo kuishia hapa JF.
Kwa vile ni kazi ya serikali mwajiri atampa likizo ay secondment
 
  1. Tundu Lissu- Mwanasheria mahiri ambaye amechangia kwa asilimia kubwa sana katika mchakato huu tulionao wa Katiba mpya.
  2. Prof.Baregu Mwesiga- Gwiji wa maswala ya Sayansi ya Siasa(Political Science).
  3. Prof. Abdullah Safari- Gwiji wa maswala ya Sheria na vilevile ataondoa zana ya udini ndani ya CDM kwamba ni chama cha Wachagga na Wakristo tu.

Hii listi itafaa sana kuiwakilisha CHADEMA kwenye hiyo Tume ya Rais ya Kuunda Katiba mpya ya JMT.

Majina kuwa waislamu au mkristo haina maana. Hata hivyo angalia waislamu wana uwezo gani wakufanya kaz za kitaifa au maendeleo zaidi ya kuwaza ukristo tu? Wachache sana wanaweza suala la maana hapa si uislamu bali kazi zao ni zipi wakati wameajiliwa kuhudumia umma wanawaza ukristo
 
napendekeza PR Safari, kitila mkumbo, na Mabere Marando kwani wabunge wana nafasi ya kushiriki kwenye bunge la katiba hivyo mawazo yao wana nafasi ya kuyatoa kipindi cha bunge la katiba.
 
Kwa mujibu wa sheria,wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani hawawezi kuteuliwa kuwa wajumbe wa tume. Ila wanasiasa wengine wote ambao hawana hivyo vyeo wanaweza kuteuliwa. Hivyo, majina kama ya Lissu, Mnyika, Mdee, tayari sheria imewaweka kando.

Umeona eeeh! Hivi ni vitu amabvyo tayari great thinkers wangekuwa wamevisoma, ile sheria wala haikuwa ndefu hivyo kwa great thinkers kushindwa kuisoma kuisoma. Hii inatia mashaka hata namna ya uchangiaji maoni utakavyokuwa. Tusiwe wavivu wakusoma na kutegemea kina fulani watatufikishia mawazo yetu.

Kama nilielewa vizuri hii ilikuwa njia ya kuepuka siasa kuingizwa kwenye mchakato huu.
 
  1. Tundu Lissu- Mwanasheria mahiri ambaye amechangia kwa asilimia kubwa sana katika mchakato huu tulionao wa Katiba mpya.
  2. Prof.Baregu Mwesiga- Gwiji wa maswala ya Sayansi ya Siasa(Political Science).
  3. Prof. Abdullah Safari- Gwiji wa maswala ya Sheria na vilevile ataondoa zana ya udini ndani ya CDM kwamba ni chama cha Wachagga na Wakristo tu.

Hii listi itafaa sana kuiwakilisha CHADEMA kwenye hiyo Tume ya Rais ya Kuunda Katiba mpya ya JMT.

Ndugu,

Ni vizuri sana ila iwe hivi;
1. Tundu Lissu;
a) Waziri (kivuri) wa sheria na katiba
b) Mwanasheria mahiri aliyeongoza jitihada za kudai marekebisho makubwa bungeni
c) Mchango wake ni mkubwa katika mchakato wa kudai katiba mpya.

2. Prof. Baregu Mwesiga;
a) Gwiji wa maswala ya Sayansi ya Siasa (Political Science).
b) Muelewa wa mambo mengi mbali mbali ya kijamii
c) Hana misukosuko na shughuli nyingi za kisiasa
d) Mzoefu wa muda mrefu

3. Prof. Abdullah Safari;
a) Gwiji wa maswala ya Sheria na lugha
b) Muelewa wa mambo mengi mbali mbali ya kijamii
c) Hana misukosuko na shughuli nyingi za kisiasa
d) Mzoefu wa muda mrefu

NB: 1. Licha ya uzoefu wa washiriki katika suala la sheria /Katiba ni watu wazima wanaoeshimika si tu katika jamii bali pia katika fani zao.
2. [Wilson M. Raphael, Ubungo Makuburi (38)]
 
1.Shibuda
2.Nyambari Nyangwine
3.Maxence Mello au kama atakuwa busy basi BUJIBUJI

Msiniulize source...hayo ndo majina yangu nayoyatuma chadema
 
Wana CDM ungependa majina yapi kutoka chama cha CHADEMA waingie kwenye mchakato wa kurekebisha katiba.
Mi ningeanza na
1:J.Mnyika
2:T.Lisu na
3:V.nyerere

Kwa CDM watoke hawa

1. Shibuda
2. Zitto
3. Prof. Safari
Hawa ni watu makini na wenye uelewa wa siasa za kitanzania

Back
Top Bottom