Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024 | Tanzania Independent Electoral Commission Act, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Sheria hii inabainisha muundo, majukumu, utaratibu wa upatikanaji wa Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na sifa za Mkurugenzi wa Uchaguzi, kuweka utaratibu wa uendeshaji wa vikao vya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuweka masuala mengine yanayohusiana na hayo.

Kwa mujibu wa Sheria hii, Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo pia itajulikana kama “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi”.

Tume hii itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa
na Rais. Aidha, Rais atateua wajumbe wa Tume kama ifuatavyo:
  • Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Kamati ya Usaili kwakuzingatia masharti ya Ibara ya 74(1)(a) na (b) na (2) ya Katiba na kanuni zitakazotengenezwa chini ya Sheria hii; na
  • Wajumbe wengine wa Tume kutoka miongoni mwa majina yatakayowasilishwa na Kamati ya Usaili baada ya kufanyiwa usaili.
  • Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi watashika madaraka
    mara baada ya kuapishwa na Rais.
  • Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
  • Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu na Mtendaji Mkuu wa Tume.
Tume itakuwa ni chombo huru na kinachojitegemea na uamuzi wake hautaingiliwa na chombo chochote au kulazimika kufuata maagizo ya mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au maoni ya chama chochote cha siasa.
 

Attachments

  • SHERIA YA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YA MWAKA 2024.pdf
    272.5 KB · Views: 7
Nashangaa nguvu haipelekwi kwenye mfumo wa wazi wa kuhesabu kura kidigitali na kuonwa na watu (ziwe displayed online) kwa kila kituo.

Kila chama kiruhusiwe kuwa na mwangalizi ndani ya kituo naye asaini kukubali matokeo kabla ya kutangazwa na kama kunakwere ziwe solved, tusileteane uhuni kwenye kuhesabu kura na kutoa matokeo katika kiiila kituo!!
 
Nashangaa nguvu haipelekwi kwenye mfumo wa wazi wa kuhesabu kura kidigitali na kuonwa na watu (ziwe displayed online) kwa kila kituo.
Kila chama kiruhusiwe kuwa na mwangalizi ndani ya kituo naye asaini kukubali matokeo kabla ya kutangazwa na kama kunakwere ziwe solved, tusileteane uhuni kwenye kuhesabu kura na kutoa matokeo katika kiiila kituo!!
Kuchagua M/kiti mkutano Mkuu wa CCM Dodoma wenye wajumbe zaidi ya 1200 ;upigaji,uhesabuji ,utangazji na usimikaji wa mshindi hauchukui zaidi ya dakika 90,tume huru iachane na huu utaratibu wa timu iliyokuwa si huru uchaguzi wa kata yenye wapiga kura chini ya 1000 kuchukua siku kibao ndipo mshindi atangazwe.chukueni mwarobaini ccm.
 
Back
Top Bottom