Gongo la Mboto 2025: CHADEMA wadai mambo 2 tu kwenye Sheria ya Uchaguzi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Na. M. M. Mwanakijiji
1710948552964.png



Kwa wanaokumbuka na wale wasiokumbuka ni kuwa mimi ni mpinzani wa madai ya Katiba Mpya. Sijaona bado na sijashawishika kabisa kutambua mchakato wowote halali wa uandikaji wa Katiba Mpya. Nilitakaa na kupinga mchakato haramu ulioanzishwa na Rais Kikwete wa kuivunja Katiba ya sasa na kutaka kuwapatia Watanzania Katiba Bambikizi kupitia Tume Haramu ya Warioba. Sisemei nia mbaya au kuwa walilenga vibaya bali nilikataa kuwa Katiba ya sasa ilivyo haina sehemu yoyote inayoruhusu uandikaji wa Katiba Mpya bila kuivunja hii ya sasa.

Kwa maneno mengine, uandikaji au uanzishaji wa mchakato wowote wa Katiba Mpya Tanzania ni haramu kwa kila kiwango hadi pale Katiba ya sasa itakapofanyiwa kwanza mabadiliko katika Ibara yake ya 100. Nilichokisema kuanzia 2010 hadi sasa ni kuwa kinachoruhusiwa kufanyika - kwa wale wanaojitaja kuwa ni watetezi wa utawala wa Katiba (constitutional rule) ni kuwa mabadiliko katika ibara na vipengele mbalimbali vya katiba (constitutional amendments).

Siyo lengo langu kupitia hii hoja tena; ukitaka kuelewa kwa undani hoja hii tafuta humu JF kwa mada zilizoanzishwa nami zenye vichwa vya habari "Katiba Mpya" nimefafanua kwa kina hoja yangu ya kukataa mchakato wa Katiba Mpya jinsi ulivyoanzishwa, kuendeshwa na hatimaye kuja na ile Katiba Bambikizi ambayo tumshukuru Mungu haikupita na inatakiwa itupwe kwenye jalala lisilosahau la historia.

Lengo langu hata hivyo ni kudokeza vitu vichache tu kuelekea 2025.

1. Katiba Mpya inaweza kuja kama ajenda kuu ya Chama cha Upinzani. Ni makosa makubwa kwa chama cha upinzani, mashabiki na wapambe wake kukidai na kukiomba chama tawala kiwape Katiba Mpya. CCM ilijifunza mapema sana baada ya yaliyotokea Zambia na Malawi na hata Kenya. Kama chama tawala hakiwezi kuweka mafuta jikoni, kikaangio na viungo halafu kijitumbukize chenyewe na mwiko ushikwe na wapinzani! Ndio maana, kiliteka hoja ya Katiba Mpya ili kiisimamie kinavyotaka, kicheleweshe, kivuruge, na hatimaye uchaguzi mwingine uje chini ya Katiba hii hii ya sasa.

2. Ni kweli nimewasikia baadhi ya viongozi wa juu kabisa wa CCM wakiahidi kuwa uchaguzi ujao utakuwa mzuri (huru na wa haki) kwa vile wao safari hii wana mtu anayewaahidi watanzania kuwa utakuwa mzuri. Baadhi ya viongozi hawa wameonesha kuwa uchaguzi wa 2020 ulikuwa mbovu na kuwa ulivurugwa na mgombea wao wenyewe. Kwamba sasa, wanaenda kufanya uchaguzi wa kiungwana. Naomba kupendekeza kuwa CCM haina lengo, nia, mpango, kusudi, wala ndoto ya kuwa nje ya madaraka ya nchi yetu kwa kipindi chochote kijacho cha karibu au cha mbali.

3. Ili angalau kuwe na mwonekano wa uchaguzi mzuri (huru, wa wazi na wahaki) ili kwamba hata kama CCM ikishinda tena kusiwe na alama ya kuuliza basi naamini mambo matatu ni lazima yafanyike na kuwa upinzani uyadai haya badala ya Katiba Mpya. Kumbuka kuwa hoja ya 1 hapo juu inasimama. Wapinzani hawahitaji huruma ya CCM kupata Katiba Mpya bali wao waahidi Watanzania kuwa watakuja na mchakato wao bora wa Katiba Mpya kuliko ule ulioletwa na CCM ukashindwa.

Mambo Upinzani Uyadai Sasa Kisheria na Kiutawala

a. Tume ya Uchaguzi iruhusu vyama na taasisi mbalimbali kuwa na vituo vyao vya kujumlisha matokeo ya kura (tallying centers). Kwa vile matokeo yote ya uchaguzi yanatangazwa kwanza vituoni baada ya kujumlishwa kila kituo na baadaye jumla yake kuu kupelekwa Makao Makuu ya Jimbo (Halmashauri) basi vyama na taasisi mbalimbali visikatazwe kuchukua jumla hiyo hiyo. Kwa vile hesabu za kujumlisha hazijali unaannzia wapi ni wazi kuwa kwenye uchaguzi huru na wa haki jumla ikijumlishwa na CCM, Chadema, Azam TV na kwingine haiwezi na haipaswi kuwa tofauti.

15 + 20 + 40 + 60 ni sawa sawa kabisa 40 + 20 + 60 + 15. Haijalishi nani anaanza kujumlisha na anaanzia wapi kujumlisha kama wote wanajumlisha namba zile zile zilizoko vituoni basi jumla haiwezi kuwa tofauti. Jumla ya Tume ya Uchaguzi haiwezi na haipaswi kuwa tofauti na ile ya CCM au CHADEMA, au vyombo vya habari.

b. Tume ya Uchaguzi ianze kuruhusu vyombo vya habari kutangaza wanaoelekea kushinda uchaguzi - iwe Udiwani, Ubunge au Urais. Kwa sababu ya (a) hapo juu ni wazi kuwa asilimia wa waliojiandikisha kupiga kura na waliopiga kura inajulikana basi matokeo ya kura halali zote inaweza kulinganishwa na kutupa picha ya nani anaelekea kushinda uchaguzi (projected winner). Kama kwenye jimbo A waliopiga kura ni asilimia 80 ya wale waliojiandikisha na kura zinaonesha kuwa mgombea X,Y amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa basi vyombo vya habari viruhusiwe kumtangaza projected winner (Anaelekea Kushinda) au ameshinda kwani hata kura zilizobakia zikipewa wagombea wengine wote haziwezi kumuondolea ile asilimia 50+1 ya ushindi.

c. Kutokana na hoja ya (a) na (b) hili la kutangaza projected winner liwe kweli pia kwenye matokeo ya Urais. Lakini hapa kuna moja liliminywa 2010 wakati wa Dr. Slaa na lilitokea 2015 wakati wa Lowassa dhidi ya mgombea wa CCM. Kwa wanaokumbuka 2010 matokeo ya uchaguzi yalipoanza kuonesha Dr. Slaa anaongoza kwenye baadhi ya majimbo vyombo vya habari vilikatazwa kuanza kuonesha matokeo ya uchaguzi hadi yatangazwe na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Ikumbukwe kuwa sheria yetu ya sasa inataka matokeo ya kura za Urais ni lazima yatangazwe (yawekwe hadharani yanapoweza kuonekana) kwenye kile jimbo KABLA ya kutangaza yale ya Ubunge na Udiwani. Sijui nilipigwa vipi maana sheria ya uchaguzi ya 1984 ilikuwa vizuri kwenye hili kuliko mabadiliko yaliyofanyika baadaye. Kwa hiyo, wapinzani na taasisi za habari na zisizo za kiserikali wanaweza kwenda kwenye kila jimbo na kukusanya matokeo yaliyobandikwa hadharani na kuyajumlisha kwa kanuni ya hapo (b).

Majumuisho hayo yanaweza kutoa picha ya nani anaelekea kushinda uchaguzi wa Urais lakini yakizingatia kanuni ya (b) hapo juu ni wazi kuwa HAYAWEZI, HAYAPASWI, NA HAYATAKIWI kuwa tofauti na yale yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi.

Kwa misingi hii hapo juu, CCM na serikali yake wanaweza kufanya uchaguzi ujao uaminike zaidi na kukubalika na kuondoa makadokado ya kuwa tume ya uchaguzi sio huru. Kwa utaratibu ulivyo sasa unaweza kufanya uaminike zaidi. Lakini kuna jambo la mwisho ambalo likitokea kuelekea 2025 litasaidia zaidi kuwa na uchaguzi huru, wa wazi na wa haki. Jambo hili ni kubwa zaidi na upinzani ulidai kutoka kwa viongozi wa CCM waliseme hadharani.

4. CCM Itangaze Hadharani Kuwa kwa vile imeahidi kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki mwakani na hakutakuwa na uvurugaji wowote kwa vile Rais Samia amekusudia kuhakikisha hilo linakuwepo; basi, iseme kuwa itakuwa tayari kukubali kukabidhi madaraka kwa njia ya amani kwa chama kingine endapo kitashindwa uchaguzi mkuu mwakani. Na kuwa Rais Samia atakuwa tayari kumkabidhi yule atakashinda na wao watakuwa tayari kuwa wapinzani.

CCM wakiahidi hili mapema basi Tanzania tutakuwa tunakaribia kuwa nchi ya kidemokrasia.

(inaruhusiwa kuchapa wazo hili popote bila kulibadilisha).

Niandikie: klhnews@gmail.com
 
CCM hii haiwezi kutupa katiba itayorahisisha safari yao ya kuondoka madarakani kwa njia ya amani.

Pia, wanaweza kutangaza kukabidhi madaraka kwa chama kitachoshinda, lakini kamwe hawawezi kutekelleza hilo.

Yoyote mwenye nia ya kukabidhi madaraka kwa upinzani (kama yupo) usalama wake utakuwa ni mdogo sana.
 
CCM hii haiwezi kutupa katiba itayorahisisha safari yao ya kuondoka madarakani kwa njia ya amani.

Pia, wanaweza kutangaza kukabidhi madaraka kwa chama kitachoshinda, lakini kamwe hawawezi kutekelleza hilo.

Yoyote mwenye nia ya kukabidhi madaraka kwa upinzani (kama yupo) usalama wake utakuwa ni mdogo sana.
Labda waamuke siku hiyo wakiwa wamechanganyikiwa na hawajielewi. Lakini wakiwa na akili timamu hawawezi kudiriki hata kuwaza hivyo. Ni sawa na kujitia kisu kooni
 
Katiba Mpya ni muhimu sana kufanikisha mabadiliko mbalimbali tunayopigania. Nguvu za Viongozi wa CCM na hata katika kulitumia Jeshi la Polisi Kisiasa inatokana na ubovu wa Katiba ya Sasa
 
Kuna wakati nahisi labda Watanzania walio wengi wala hawahitaji katiba mpya!

Wao wanataka tu Rais wa CCM aliyepo madarakani asifokee watu. Asiwe mkali. Na aongee kwa lugha ya upole.

Ni hivyo na watu hao wanaridhika kabisa hata kama hawana maji ya kuoga.
Ndiyo kinachoendelea..yaani mambo mengine ukiyafikiria yanaumiza kichwa.
 
Nikisoma mawazo kama haya huwa nabaki najichekea tu. Kuna watu wakongwe humu lakini kila wanapoiongelea CCM ni kama vile ukongwe wanauweka kando, hawaijui CCM.

Jamani CCM ni zaidi ya watu wengi wanavyofikiria. Hebu fikiria CCM inayoweza kuhimiza na kusherehekea kauli mbiu ya kazi iendelee huku hii awamu wakiita ya sita badala ya tano!

Hebu fikirieni tena hali hii...hakukuwa na uchaguzi, aliyerithi Urais ndiye alikuwa makamu, Wazi Mkuu ni yule yule, seriali ni ile ile, Wabunge ni wale wale. Awamu ya sita? Are we serious?

CCM ina mengi na kukaa CCM madarakani kunasetiri hayo mengi. Wenye CCM wako tayari kwa lolote mradi wanabaki madarakani kwani, nje ya madaraka, hakuna CCM wala kivuli chake.

Nawatakia mjadala mwema.
 
Nikisoma mawazo kama haya huwa nabaki najichekea tu. Kuna watu wakongwe humu lakini kila wanapoiongelea CCM ni kama vile ukongwe wanauweka kando, hawaijui CCM.

Jamani CCM ni zaidi ya watu wengi wanavyofikiria. Hebu fikiria CCM inayoweza kuhimiza na kusherehekea kauli mbiu ya kazi iendelee huku hii awamu wakiita ya sita badala ya tano!

Hebu fikirieni tena hali hii...hakukuwa na uchaguzi, aliyerithi Urais ndiye alikuwa makamu, Wazi Mkuu ni yule yule, seriali ni ile ile, Wabunge ni wale wale. Awamu ya sita? Are we serious?

CCM ina mengi na kukaa CCM madarakani kunasetiri hayo mengi. Wenye CCM wako tayari kwa lolote mradi wanabaki madarakani kwani, nje ya madaraka, hakuna CCM wala kivuli chake.

Nawatakia mjadala mwema.
Mzee mwenzangu.
Nimefurahi kukuona...ndiyo maana sijawahi kuiita "awamu ya sita". Na demokrasia yetu haijapimwa bado...hadi CCM ipoteze Urais au Bunge.
 
Back
Top Bottom