Makosa tunayotakiwa kurekebisha kama nchi

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,817
21,791
makosa tunayotakiwa kurekebisha Kama nchi, kwa baadhi, ni kama ifuatavyo:

1. kutokuwa na mfumo rasmi wa kiuchumi.

Katiba yetu ya mwaka 1977, ibara ya 3 (1) inaitambua Tanzania Kama nchi yenye mfumo wa kijamaa. Hivyo Tanzania kisheria inafuata mfumo wa kiuchumi wa kijamaa, lakini ukija kwenye uhalisia Tanzania ipo katikati, ujamaa nusu na soko huria nusu.

Ni muhimu kuwa na mfumo rasmi Kikatiba wa kiuchumi na sio kujiendea kiholela. katiba inasema kivingine kiuchumi sisi tunakwenda kivingine kiuchumi. Tutaendelea kupiga mark time.

2. Mfumo wa vyama vingi wenye maneno na sio matendo.

Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye ibara ya 3 (1) imeitambua Tanzania Kama nchi inavofuata mfumo wa vyama vingi. unaposema mfumo wa vyama vingi inamaanaisha uwanja uwe na haki sawa kwa vyama vyote na sio kwa chama kimoja kinachotawala.

Hivyo basi, Mashirika ya Umma ya utangazaji Kama TBC yavitangze vyama vyote bila upendeleo na pia vyombo vya Dola visionee vyama vya upinzani na kukipendelea Cha kinachotawala. Kwa mfano Ni kosa kubwa sana, CCM inapompitisha mgombea urais , ghafla anaanza kulindwa na TISS hata kabla hajachukua fomu ya kugombea urais NEC. kwa kifupi TISS wanatuambia ya kuwa huyu ndiye Rais wenu mkubali au mkatae. Kwenye mfumo wa vyama vingi hiki sio sahihi.

Niseme ukweli, kwa Tanzania tumeufuta mfumo wa vyama vingi kimaneno na sio kivitendo.Ni Bora tuache unafiki, tuamue moja tunataka mfumo wa vyama vingi au chama kimoja. Kama tunataka mfumo wa vyama vingi basi tuweke mazingira sahihi na sio kubahatisha. Tutunge sheria zetu kwa kufuata mfumo wa vyama vingi kuanzia ajira, elimu, jinai, uchaguzi, etc. .

3. Kuruhusu wanasiasa kuwa wakurugenzi kwenye Halmashauri za wilaya, miji na manispaa.

Kwa Sasa kwenye nchi yetu, tumeamua ya kwamba mgombea yeyote wa chama tawala au mkereketwa wa chama tawala au mwanachama wa upinzani aliyehamia chama tawala anaposhindwa kwenye chaguzi basi anapewa fadhila ya kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri bila hata kuwa na uzoefu. mwisho wa siku ni ufisadi na uongozi mbovu kwenye Halmashauri zetu.

Nashauri ya kwamba kwenye mambo yahusuyo ukurugenzi wateuliwe watumishi waandamizi kutoka kwenye idara za Halmashauri husika waliofanya kazi kwenye Halmashauri kwa muda mrefu na sio wanasiasa.

Kama Hilo haliwezekani, basi waajiriwe wasomi waliobobea kwenye mambo ya utawala na Wana uzoefu wa kutosha kwenye kuongoza taasisi kubwa za kibinafsi kwa mafanikio.

4. Mikopo ya Elimu ya Juu.

kwa Sasa serikali inatoa mikopo kwa Elimu ya Juu. Nadhani kwa Hali ilivyo kwa Sasa hatuhitaji kutoa mikopo kwa ajili ya Elimu ya Juu Bali tutoe ruzuku kwa vyuo vinavyopokea wanafunzi na kuwapa wanafunzi msaada wa masomo kwa maana nyingine ufadhili. Yani , serikali ijitolee kwamba itaweza kusomesha wanafunzi kadhaa na hapo itawapa ufadhili wa masomo bila kuwadai watakapo maliza masomo.

Hii ni kwa sababu kwa Sasa suala la ajira limekuwa gumu Sana. Hivyo wanaokopeshwa hawana uhakika wa ajira na kurejesha mkopo. Hivyo ni muhimu kuweka mfumo wa kuwafadhili wanafunzi wa idadi Fulani bila kuwapa mkopo. Kama serikali imechagua wanafunzi 40,000. Basi itawadhili wanafunzi hao tu kwa kiwango chote bila kuwapa nusunusu.

Hili litawezekana kwa serikali kuamua kuchukua asilimia tano ya mapato ya utalii au madini kwa mwaka na kufadhili wanafunzi kwenye elimu ya juu. Bila hivyo serikali itapata hasara maana mikopo haitarudi na pia wanafunzi waliokopeshwa watapata shida wakati wa makato ya kulipia mkopo kwa serikali kutokana na gharama za maisha kuwa juu.

5. Kutegemea mikopo kuendesha uchumi.

Kuna kipindi mwaka Jana Rais wa Nchi alidai kwamba ilibidi serikali ikope nje ili kulipa mishahara wafanyakazi. Ni ukweli mikopo haikwepeki ila tusiitegemee mikopo kiasi cha kulipia mishahara wafanyakazi wetu.

Nashauri tuanzishe mpango mkakati wa kujinusuru na madeni ya nje. Tuweke mpango ambapo tutakuwa kila mwaka tunapunguza kukopa kiasi Fulani nje na kuongeza uzalishaji wa bidhaa kwenda nje ya nchi.

Pia tunaweza kuanzisha akina ya Fedha za gesi na madini, ambako asilimia Fulani itawekwa hapo kwa muda wa miaka ishirini bila kuguswa. Fedha hizi zaweza kusaidia kupunguza Deni kwa kiasi Fulani na kutupelekea kwenye kujitegemea.

Ni hayo tu kwa Sasa
 
Hopeless Viongozi wetu wengi ni Low IQ na haina tiba ni Genetics.

Nchi hii itabaki onazunguka hapo hapo kama Dung Beetle.
 
beetlesusedu.jpg
SKNP-3-2.jpg
scarab-2490586_960_720.jpg
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%. Kutokuwa na sera imara za kiuchumi kunaturudisha nyuma sana. Tunapoteza muda, fedha na nguvu nyingi kwa kung'ang'ania mifumo isiyo na tija.

Badala ya kuendelea na mfumo wa serikali kumiliki na kuendesha mashirika nashauri uanzishwe mfuko wa uwekezaji ambao utakuwa unaweka fedha kwenye miradi ya kimkakati yenye lengo la kuzalisha ajira na kuuza products nje ya nchi ili kuongeza mauzo ya nje.

Kwa mfano pesa zote ambazo zinatumika kuwapa vikundi vya vijana, wanawake, wavuvi na makundi mengine ambazo kimsingi hazileti tija na nyingi hupotea zingeingizwa kwenye mfuko wa uwekezaji. Then kila mwaka mfuko wa uwekezaji uanzishw miradi mikubwa miwili au mitatu kwa kushirikiana na wawekezaji, ambapo serikali itamiliki hadi hisa 30% na nyingine zikauzwa wa Wawekezaji wa ndani na nje.
 
Back
Top Bottom