Magufuli, Jiuzulu kwa hiari yako

Ajiuzulu kwa ajili ya kupandisha Sh. 100? Hapo si sawa, ila kutokana na kauli yake inabidi aombe msamaha kwa wananchi maana yeye si malaika mpaka asijikwae. Halafu kuhusiana na matumizi ya serikali msiangalie tu posho za wabunge (Japo nami silikubali), pia kuna mambo mengi sana kama vile: ongezeko la wanafunzi vyuoni ambao wanahitaji mikopo, kuwepo kwa shule za kata ambapo inabidi wapewe ruzuku, mwezi huu walimu wanaanza kulipwa madai yao ya muda mrefu, kuna baadhi ya miradi ya barabara serikali imeingia gharama baada ya wafadhili kujitoa, n.k. Sometimes tuwe na huruma kwa serikali yetu, sio kila wakati kuiponda.

Wewe unataka tuwe na huruma gani wakati ni wenyewe waliowapangiwa wawekezaji katika migodi kulipa mrahaba wa 3% tu na zingine wawalipe viongozi kama 10%. Mbona nchi ndogo ndogo kama Botswana inaingia ubia wa 50% katika uwekezaji katika migodi yake?

Huruma gani unataka tuwe nayo wakati kiongozi uanaunda serikali kubwa yenye mawaziri lukuki wasio na kazi yoyote. Na hataki kuskia ushauru wa kuunda serikali ndogo ili kupunguza gharama.

Huruma gani wakati mkuu wa nchi anatumia magarii kati ya 20 hadi 40 kila mwisho wa wiki kuzuru miradi yake binafsi huko msoga Bagamoyo. Hizo ghrama za mafuta ya magarai na posho za watumishi zinazotumika kuhudumia miradi binafsi sizingetosha kuziba ongezeko la harama katika hivi vivuko?
 
mtoa mada, hata jina la waziri wa ujenzi haujui linaandikwaje

very low

shame !

I would say so too!
very simple logic. Unamchukia mtu hata kumtendea haki hutaki?
Haya umeshasema yote, kama kweli wewe ni Objective minded person, mention/list even one of his positive side as a minister.
 
Ajiuzulu kwa ajili ya kupandisha Sh. 100? Hapo si sawa, ila kutokana na kauli yake inabidi aombe msamaha kwa wananchi maana yeye si malaika mpaka asijikwae. Halafu kuhusiana na matumizi ya serikali msiangalie tu posho za wabunge (Japo nami silikubali), pia kuna mambo mengi sana kama vile: ongezeko la wanafunzi vyuoni ambao wanahitaji mikopo, kuwepo kwa shule za kata ambapo inabidi wapewe ruzuku, mwezi huu walimu wanaanza kulipwa madai yao ya muda mrefu, kuna baadhi ya miradi ya barabara serikali imeingia gharama baada ya wafadhili kujitoa, n.k. Sometimes tuwe na huruma kwa serikali yetu, sio kila wakati kuiponda.

You are a real a great thinker who is objective minded.
 
Wewe unataka tuwe na huruma gani wakati ni wenyewe waliowapangiwa wawekezaji katika migodi kulipa mrahaba wa 3% tu na zingine wawalipe viongozi kama 10%. Mbona nchi ndogo ndogo kama Botswana inaingia ubia wa 50% katika uwekezaji katika migodi yake?

Huruma gani unataka tuwe nayo wakati kiongozi uanaunda serikali kubwa yenye mawaziri lukuki wasio na kazi yoyote. Na hataki kuskia ushauru wa kuunda serikali ndogo ili kupunguza gharama.

Huruma gani wakati mkuu wa nchi anatumia magarii kati ya 20 hadi 40 kila mwisho wa wiki kuzuru miradi yake binafsi huko msoga Bagamoyo. Hizo ghrama za mafuta ya magarai na posho za watumishi zinazotumika kuhudumia miradi binafsi sizingetosha kuziba ongezeko la harama katika hivi vivuko?

Sasa kama huyo hajajiuzulu kuna haja gani ya kupoteza nguvu zetu na energy kutaka Dr. Pombe ajiuzulu?
Wengine wote si wanatekeleza viapo vyao vya utiifu kwa raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Sishangilii kuongezwa kwa nauli lakini pia siungi mkono hoja kwamba Maghufuli kujiuzulu eti kwa sababu kaongeza bei za kivuko. Bei ngapi zimeongezeka na hakuna waziri aliyeambiwa ajiuzulu. Bei za mafuta zinaonmgezeka kila siku hakuna waziri aliyeambiwa ajiuzulu, bei za vyakula na sukari zinaongezeka kila siku lakini hatujasema waziri ajiuzulu. Hivi kati ya kupanda kwa bei ya vyakula/sukari na kupanda kwa bei ya kivuko ni bei ipi inawaumiza wa Watanzania?

Naanza kuona muandamo wa Maghufuli wenye vimelea vya kisiasa!!

Kama kawaida yetu watz, hatujui hata mambo ya msingi ya kupigia kelele: we can not think outside the box. Mtu anaumwa malaria, baada ya kutibu malaria anang'ang'ania kunywa dawa za kutapika: side effects ya malaria.
 
Hivi hawa wabunge wanaopinga ongezeko la nauli ya kivuko kwa kudai eti wana huruma na wapiga kura wao mbona wanapokea ongezeko la posho pasipo kuwa na huruma kwa wananchi wao na pesa hizo wanazopokea ndio zingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Wanatakiwa watoe boriti machoni mwao kabla ya kutoa kibanzi machoni kwa wengine

Labda wanajua hizo posho zimetoka kwa mungu, na sio kodi ya wananchi hao hao na wengine wote wanaponunua sukari, mafuta ya taa, viberiti, chumvi, maji, sabuni, diesel and petrol, nguo, chakula, nauli za daladala na mengine mengi. Kila ukitumia centi moja, unachangia kulipia hilo ongezeko la posho.

Kwa mtaji huo, nani hasa wa kujiuzulu?
 
Magufuli kweli kituko, kwenye mia mbili kakomaa kweli na small guys, mpaka kawatolea kauli za kijeuri wakati yeye akivuka na hiyo pantoni hatoi hata cent tano nyekundu, tena anavuka na yupo ndani ya vx v8 lake. haya tuache hayo, mbona alivyopigwa mkwara na wakuu wake asibomoe nyumba tena kwake hakufurukuta mpaka leo kanyweaaaaaaaaaaaaaaa, imekuja mia mbili kaonyesha ujeuli wake mwanzo mwisho, mboooooooooooooooooooooofu.
 
BADALA YA KUMWAMBIA MAGUFULI AJIUZURU ni vema kuwaomba wananchi waandamane ili kushinikiza matumizi adilifu na yenye tija kwa rasilimali za umma. Hii ni pamoja na kupinga ongezeko la posho za wabunge, safari zisizo na tija za viongozi, na mambo kama hayo Nionavyo mimi, Magufuli yupo sahihi, maana sh mia moja ya sasa ni kidogo mno! Jiulize kama kivuko kingekuwa mali binafsi huu ulalamishi ungekuwa wapi? Na kuna habari zisizo rasimi ambazo watu wanasema pale hela nyingi za kivukoni huishia kwa wakati tiketi. Mi ninadhani hata hiyo mil 18 amesema imeongezeka ni kidogo sana. Je wakata tiketi wanataka kutuambia kama hapo awali makusanyo yalikuwa sh mil 9 kwa siku ktk bei ya sh 100 kwa mtu kwa trip moja. Je ina maana hakuna walioamua kuacha kusafirikwa kuwa nauli ya kivuko imepanda? Sisemi hapa ule utani wa Magufuli kuwa wapinge mbizi, ila kwa mtu mwenye kufanya uchambuzi utagundua mambo mengi ya ubadhirifu ktk ukusanyaji wa mapato. Jambo ambalo sielewi ni kwa nini serikali imengangania mambo ya zamani? Mbona we are not going digital? Kwa nini hatuwezi kuwa na eletronic ticket ili iwe rahisi ku-monitor? Kwa nini tusiwe na mfumo wa kuweka camera/mashine ambayo inaweza kuhesabu kila mtu anayeingia kivukoni ili iwe rahisi kujua wapi tumepigwa changa la macho? Ninapenda ushauri wake pia...kuwa endapo waheshimiwa wabunge wanaona nauli imekuwa kubwa, basi wao waombe ili waendeshe kivuko!
Maisha yanazidi kuwa magumu. Gharama za maisha zinapanda kila siku. Maghufuli kaamua kuongezea gharama za maisha kwa WTZ. Serikali inatakiwa ikate matumizi ili kuwa na kuwa na balance budget nzuri kwa nchi.

Leo ktk TZ tunaona vinyume kabisa. Serikali inaonngeza matumizi yao, posho zao. Matokeo yake, Wananchi ndiyo wanatakiwa walipe hizo gharama za matumizi ya kijinga ya serikali. Tunapandishiwa Kodi, Nauli, ili maisha ya Vigogo yaendelee.

Hii siyo society nzuri. Tunaomba Waziri Maghufli awajibike kwa kujiuzulu kwa sababu ya kuendeleza mpango huu wa serikali bila ya manufaa ya Wananchi.

Kwanini WTZ walipishwe gharama kubwa za nauli kufidia matumizi ya kijinga(posho) ya Serikali? Kwa nini tuwalipie ili tubalance budget ya serikali? Kwa nini WTZ? Kwa nini tusikate matumizi?

Nakubali kwamba Maghufuli unatekeleza mpango huu ili uwafurahishe Vigogo wa nchi,ndiyo maana hata Dewji kaamua hadharani kukusuport. Tunakuoma Ujiuzulu; hii ni Kashfa kwa nchi yetu.
 
sijapata kuona upupu huu jf, maghufuli ajiuzuru kwani yy rais? kama unazungumzia serikali unamaanisha jk na sio watoto deal na baba
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani haufahamua hata jiografia ya jiji hili achi mbali ya nchi yako. Nani kakuambi kuwa wakazi wote wa Kigamboni hutumia usafiri wa kivuko kufika makwao? webgi baada ya kuvuko kwa pantoni hutumia mabasi ya daladala, pikipiki na teksi kufika katika vitongji vyo mbali mbali.

Je hao wakazi wa maeneo uliyoyataja hulip kiasi gani kuvua madaraja yaliyojengwa katika abarabara za huko? Kama hawalipi kitu chochote basi na wakazi wa Kigamboni hawastahili kulipa chochote katika vivuko kama ilivyo Kenya. nchi amabyo haiana madini na raslimali kama Tanzania.

Nadhani wewe ndiyo huelewi Mkoa wa Dar es Salaam ulivyo!

Kwa mkazi wa Bunju B anayafenya kazi/Biashara CBD:
1. Anapanda BodaBoda mpaka Kituo cha daladala Bunju @ 1,000/- [Anaweza kutembea kama hana 1,000/-]
2. Anapanda Daladala Mpaka Mwenge @ 400/- [huwezi kutembea]
3. Anapanda Daladala mpaka Posta/Kariakoo/e.t.c @ 300/-

kwahiyo minimum ni 700/-

Vivyo hivyo wa Kitunda, Goba, Kimara Mwisho, Pugu Kajungeni, Buza, to name a few!!!

Acheni kulalama - Ukweli upo wazi!
 
Umeteleza sana mzee!
Huna hoja ya msingi ya kumtaka waziri Magufuli ajiuzuru. Nauli ya sh. 100 imedumu kwa miaka karibu ya 10 sasa. Unaweza kutumbia kwa kipindi hicho gharama za mafuta zimepanda mara ngapi? Nauli za mabasi unajua zimepanda mara ngapi kwa miaka hiyo yote? Gharama za vipuri na mishahara ya wahudumu wa vivuko unajua zimepanda kwa kiasi gani kwa kipindi cha miaka karibu kumi? Ni kweli kuwa vigogo wanajilipa posho nyingi na wana matanuzi makubwa, lakini si kwa sababu ya sh. 100 za kivuko. Ipo mianya mingi ambayo fedha za serikali zinatumika ovyo na pia zipo fursa nyingi za serikali kuinua uchumi wa watu wake kwa kutumia vizuri rasilimali za nchi hii! Tatizo ni uongozi wa Taifa hili hususani uliopo kwa sasa!

Wabunge wa dar wanaendekeza siasa hata kwenye mambo yasiyo na msingi ndio maana Masaburi aliwapa KUBWA!

Big Up Magufuli!
 
Du wabongo noma yamepanda bei mafuta kimya,nauli za daladala kimya,vyakula vimepanda kimya,umeme unapanda kimya ss hiyo panton ipo nchi ipi gharama zake zibaki hivyo hivyo au kuambiwa asiyekuwa 200 apige mbizi jaribu kupanda daladala bila nauli uone konda atakufanya nn acheni mambo hayo.
 
Jamani kiasi fulani tunadekezwa ndio maana hakuna Maendeleo, tangu lini ukasikia bei haiongezwi kwa muda wa miaka 14 tunadekezwa kweli kwanini, na ikibomoka tunataka inanze kazi mara moja hata kama vipuri vinaagizwa nje ya nchi

Lazima watu wa kigamboni waelewe wapo dunia gani naja Faustine Dugulile anajua hayo amesafiri nje ya nchi na anajua matatizo ya nchi sijui kwanini analilia hiyo bei ibaki shilingi 100.00
 
BADALA YA KUMWAMBIA MAGUFULI AJIUZURU ni vema kuwaomba wananchi waandamane ili kushinikiza matumizi adilifu na yenye tija kwa rasilimali za umma. Hii ni pamoja na kupinga ongezeko la posho za wabunge, safari zisizo na tija za viongozi, na mambo kama hayo Nionavyo mimi, Magufuli yupo sahihi, maana sh mia moja ya sasa ni kidogo mno! Jiulize kama kivuko kingekuwa mali binafsi huu ulalamishi ungekuwa wapi? Na kuna habari zisizo rasimi ambazo watu wanasema pale hela nyingi za kivukoni huishia kwa wakati tiketi. Mi ninadhani hata hiyo mil 18 amesema imeongezeka ni kidogo sana. Je wakata tiketi wanataka kutuambia kama hapo awali makusanyo yalikuwa sh mil 9 kwa siku ktk bei ya sh 100 kwa mtu kwa trip moja. Je ina maana hakuna walioamua kuacha kusafirikwa kuwa nauli ya kivuko imepanda? Sisemi hapa ule utani wa Magufuli kuwa wapinge mbizi, ila kwa mtu mwenye kufanya uchambuzi utagundua mambo mengi ya ubadhirifu ktk ukusanyaji wa mapato. Jambo ambalo sielewi ni kwa nini serikali imengangania mambo ya zamani? Mbona we are not going digital? Kwa nini hatuwezi kuwa na eletronic ticket ili iwe rahisi ku-monitor? Kwa nini tusiwe na mfumo wa kuweka camera/mashine ambayo inaweza kuhesabu kila mtu anayeingia kivukoni ili iwe rahisi kujua wapi tumepigwa changa la macho? Ninapenda ushauri wake pia...kuwa endapo waheshimiwa wabunge wanaona nauli imekuwa kubwa, basi wao waombe ili waendeshe kivuko!

Wana jeuri? wabunge wenyewe wote si watu wa mitaani, there is none of them who can make changes!!!
 
Unapoteza muda bure wa kulalamika maghufuli ajiuzuru wakati mkuu wa nchi anafurahia kupanda kwa nauli ili apate pesa za kufanyia matanuzi. Mbona Pinda hajasema chochote. Mbona mkuu wa nchi amekaa kimya. Mwacheni maghufuri yeye ametumwa kutekeleza.

Hilo ndilo tatizo la viongozi wetu. Wamewekwa madarakani kutekeleza amri za vigogo. Basically, zinatafutwa fedha za kucover matumizi makubwa ya serikali. Kwa kuongezwa kwa nauli, baadaye tutasikia vitu vingine vinapandishwa bei kama kawaida.

Serikali za Elite ndizo zinavyoendeshwa duniani. Hapa Maghufuli kachemsha. Kaonesha dhahiri kwamba hayupo madarakani ktk kutetea maslahi ya WTZ; bali yupo pale kuendeleza sera za Vigogo.
 
Back
Top Bottom