Je, ni wakati sasa kwa serikali kuanza kupunguza mzigo wa kodi kwa Wananchi?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,912
Habari za wakati;
Hivi majuzi nilikutana na bandiko la TRA ambalo walikuwa wanaalika watanzania kutoa maoni kuhusu mifumo yetu ya KODI.Bandiko lile pamoja na kwamba lilikuwa halali la TRA lakini lilikuwa kama vile limefichwa fichwa(Mtazamo wangu) so sikulichukulia SERIOUS.

Nimekuwa Katika Biashara kwa zaidi ya Miaka 15 na nimekuwa nikila kodi za aina mbalimbali kama vile PAYE,PIT,Corporate Income TAX.Kwa uzoefu wangu wastani wa kodi ambayo MTanzania wa kawaida analipa ni kubwa sana.Kutokana na ukubwa wa kodi ambayo serikali inpoteza kodi kubwa sana na kutumia gharama kubwa sana kukusanya kodi hiyo na hivyo Mapato ya serikali yanakuwa chini kwa kulinganisha na uwezo wa kiuchumi wa Taifa na kasi ya kukuwa kwa uchumi wa Taifa.

Mpaka ninapoandika andiko hilo wastani wa makusanyo ya TRA kwa MWEZI ni kama Trilioni2 za Kitanzania.Makusanyo haya ni nje ya TOZO na ADA mbalimbali ambazo zinatozwa na mamlaka na IDARA nyingine za SERIKALI ambapo kwa makadirio yangu zinaweza kufika hadi 20% ya Makusanyo ya TRA ambayo kimsingi ndio kodi yenyewe.
Ukitazama makadirio ya Matumizi ya Serikali ni TRILION za Kitanzania 47.1 huku Mapato ya Serikali yakiwa ni kwa Mujibu wa TRA yakikadiriwa kuwa ni wastani wa TRILIONI 24 kwa mwaka.Hii ina maana kwamba serikali inapanga Kutumia Mara mbili ya Uwezo wake wa kukusanya Mapato.

Sasa swali la kujiuliza ni Je Pato la TAIFA ni kiasi gani?Na kodi ni Asilimia Ngapi ya Pato la TAIFA.Kwa mujibu wa Takwimu mbalimbali GDP ya Tanzania kwa sasa inaweza Kufika TRILION 191.2 za kitanzania.Ambapo Serikali inapanga kutumia 24% kwa Ajili ya Matumizi yake.Huku Makusanya ya TRA yakiwa yanakadiriwa kuwa wastani wa asilimia 12%.Idadi ya walipa kodi inakadiriwa kuweza kufikia milioni 7.Hawa ni walipa kodi ambao wanalipa kodi TRA moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Takwimu hizi ina maana kwamba.Katika Taifa lenye watu Milioni 60+ ni kadiri ya watu Milioni 7 tu ambao wamesajiliwa kulipa kodi ni sio wote ambao wanalipa kodi.Hivyo basi kwa watani kila Mlipa kodi aliyesajiliwa analipa Wastani wa Shilingi Milioni 3.5 kwa mwaka.Kiasi hiki cha Milioni 3.5 kwa ni iwapo walipa kodi wote wanalipa.Ila wote tunajua kwamba Bado katika hawa Milioni 7 kuna ambao hawalipi kabisa au wanalipa kidogo sana.

Tukiendelea kuchambua Mfumo wetu wa kikodi tutaona kwamba vyanzo vya kodi kwa miaka mingi vimekuwa ni MobilePhone,Cigarettes, Beer,Spirits, SoftDrinks,Bottled Water,pamoja PAYE inayotozwa kwenye Mishahara.Hata Hivyo idadi ya watu walioajiriwa ambao wanalipa PAYE ni ndogo zaidi ingawa mchango wa katika Kiwango cha Makusanyo unaweza kuwa Mkubwa zaidi.

Ukifuatili zaidi Mfumo wetu wa kikodi utaona kwamba kwa sasa hivi kodi na TOZO zimekuwa nyingi kiasi kwamba zinaathiri kabisa ubora wa maisha ya wananchi,kuongeza mfumuko wa BEI na kufanya MAzingira ya BIASHARA yawe Magumu hasa kwa wale ambao wanataka kufuata Taratibu zote za kisheria na kikodi.Matokeo yake Hali hii imesababisha serikali ipoteze mapato mengi halali kwa sababu ya Ugumu na Gharama za Kusimamia TOZO na kodi mbalimbali ambazo wakati mwingine zinahusisha Mamlaka na TAASISI nyingi ambazo hazimuongezei thamni mwananchi wala mfanya biashara lakini zinamuongezea mzigo wa TOZO na kodi.

Baadhi ya kodi unashindwa hata kuelewa ziliwekwa kwa RATIONALE GANI.Hata hivyo kwa sababu serikali lazima ikusanye Mapato naona wakati mwingine viongozi wetu ama kwa uvivu wa kufanya kazi ama kwa ulafi wanaamua kutafuta namna ya kuchukua/kuwapora wananchi kwa kisingizio cha kodi.Mbaya zaidi bado huduma nyingi za msingi kama elimu,afya,miundo mbinu n.k. ni ghali na zinatolewa kwa kiwango cha chini sana.Hali inapeleke tujiulize iwapo viwango hivi vya kodi ni halali au sio halali.

Ninapoandikka andiko hili nafahamu kwamba Bado serikali inakopa ili kuendesha nchi,Bado viongozi wetu wanatumia nafasi zao kula urefu wa kamba zao,bado wananchi wengi hawamudu gharama za maisha na Bado serikali haijweza kuweka Mifumo mizuri ya kuwawezesha wananchi.

Sasa kabla sijajikuta ninapoteza Msingi wa Hoja Napendekeza Serikali Ipunguze Viwango vya Kodi Kwa namna Ifuatavyo:

  1. Kwanza kabisa serikali Ishushe kiwango cha kodi ya VAT iwe single DIGIT kwa sababu hii ni consumer TAX ambayo inatozwa kwa Final Consumer.Ninaamini kabisa Kwa kushusha kodi hii kuwa singe Digit,Kutaungaza Kasi ya ULIPAJI na kiwango cha Makusanya ya VAT na kuwapunguzia wananchi Ukali wa Maisha.
  2. Pili Serikali Ishushe Kiwango cha Kodi ya mapato kwa watu Makampuni ambacho kwa sasa kinafikia hadi 30% kishushe hadi 18 Yaani kiwango cha VAT ndio kiwe kiwango cha Kodi ya Mapato Hii itaongeza Kasi ya Ulipaji na Idadi ya Walipaji na Wawekezaji.
  3. Vile vile serikali ipunguzi kodi ya Mapato ya Mtu Binafsi ambayo nayo hufikia Viwango vya 30% ishuke hadi 22 kama Maximum huku kwa wakati huo huo wakipandisha Threshold ya Exempt Income Kufika Milioni 10.Hii itahamasisha zaidi watu binafsi kulipa kodi hiyo kwa wingi.
Ili kuhakikisha Hili haliathiri utendaji wa Serikali,Serila Ipunguze Matumizi yasiyo ya lazima kama ifuatavyo:
  1. Pia serikali Ifute au Kuungansha Baadhi ya Agencies za serikali ambazo hazina TIJA lakini zina TOZO kwa wananchi ili kupunguza Mzigo wa TOZO kwa WANANCHI.Zibaki zile TOZO na TAASISI ambazo zina TIJA ya MOJA kwa MOJA kwa Wananchi.
  2. Serikali iondoe kabisa vyeo,wizara na idara ambazo hazina TIJA kwa wananchi na nyingine ziunganishwe ili kupunguzo mzigo wa gharama kwa wananchi.Ni muhimu sana TUWE na serikali NDOGO lakini ambayo ni effective.Hili Tutaweza Kufanikisha Kwa KUONDOA KABISA VYEO ambavyo havina TIJA yoyote kwa wananchi kama VILE CHEO cha MKUU WA WILAYA NA KATIBU TAWALA wilaya.Vibaki vyeo va Wakuu wa MIKOA na Makatibu Tawala wa MIKOA.Ninaamini kabisa kazi zao zinaweza kufanywa na ma RC wakishirikianana Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na wakurgenzi wa Halmashauri bila shida kabisa wakati tukiwa tunaendelea na UJENZI wa TAIFA na mchakato wa KATIBA MPYA.
  3. Pia Serikali Ipunguze Matumizi yasiyokuwa ya Lazima Ikiwamo Ununuzi wa Magari ya Kifahari.Iwapo Cheo cha Mtumishi kinahitaji Magari ya Kifahari basi Apewe Mkopo kama inavyofanywa kwa wabunge ila Magari yawe ya kwao.Magari ya Serikali yawe Machache na Ukubwa wa Misafara Ipunguzwe.Viongozi wajifunze na wazoee kusafiri na wananchi wengine hali ambayo itawawezesha kutokupoteza ukaribu na wananchi na kusahau wajibu wao wa msingi wa Kutumikia Wananchi.
Kuna maeneo mengine ambayo naona yanahitaji maboresho ya wazi na ya moja kwa moja ila kwa leo nichokoze mada hii ili tujadili,tukosoane,tuvutane.Takwimu mbalimbali nilizotoa sio TAKWIMU RASMI za serikali na wala hakuna sehemu moja ambapo utazipa TAKWIMU hizo na wala SIO TAKWIMU HALISI bali ni makadirio tu ambayo nimeyatumia kwa kuangalia vyanzo mbalimbali vilivyo rasmi na visivyo rasmi.Iwapo kuna makosa ya kitakwimu basi unaweza kuboresha kwa kuweka TAKWIMU rasmi.Na ukiweka TAKWIMU RASMI TAFADHALI WEKA NA CHANZO KABISA ili kulipa ANDIKO HILI NGUVU ZAIDI.

Karibuni TUJADILI ZAIDI KWA MAENDELEO YA TAIFA
 
Makusanyo kwa mwezi hayawezi kuwa bilioni 2, ni ndogo sana kabda ulitaka kumaanisha Trillioni 2?
 
Back
Top Bottom