ACT Wazalendo waitaka Serikali kusitisha Nauli mpya za Mabasi na Daladala, kushusha bei ya Sukari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
20240204_221002.jpg

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa Wananchi kwa kusitisha Nauli Mpya za Daladala na Mabasi zilizoanza kutumika Desemba 2023 pamoja na kushusha Bei ya Sukari inayolalamikiwa Nchi nzima.

Kupitia taarifa yake, ACT Wazalendo kimesema kitendo cha Serikali kuridhia maamuzi ya LATRA inaonesha wazi haiwajali Wananchi kwasababu nauli zimeangalia maslahi ya Wasafirishaji na si hali za wananchi wa kawaida.

Pia, kimeitaka Serikali kufanyia kazi madai ya Wasafirishaji kwa kurejesha ruzuku kwenye Mafuta pamoja na kuhimiza matumizi ya Gesi Asilia kwenye Vyombo vya Usafirishaji ili kupunguza gharama zinazotokana na Mafuta.

Aidha, kuhusu Sukari, Chama hicho kimesema Serikali ichukue hatua za haraka kuhakikisha Sukari inapatikana ili Wananchi wauziwe kwa Bei nafuu kwasababu hadi sasa kauli za Serikali hazijasaidia chochote.
 
Kila konda na nauli yake kwa njia hiyo hiyo.

Ikifika usiku ndiyo balaa.

Sehemu ya kwenda kwa 900/- unaambiwa 2 000/-
 
View attachment 2894657
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa Wananchi kwa kusitisha Nauli Mpya za Daladala na Mabasi zilizoanza kutumika Desemba 2023 pamoja na kushusha Bei ya Sukari inayolalamikiwa Nchi nzima.

Kupitia taarifa yake, ACT Wazalendo kimesema kitendo cha Serikali kuridhia maamuzi ya LATRA inaonesha wazi haiwajali Wananchi kwasababu nauli zimeangalia maslahi ya Wasafirishaji na si hali za wananchi wa kawaida.

Pia, kimeitaka Serikali kufanyia kazi madai ya Wasafirishaji kwa kurejesha ruzuku kwenye Mafuta pamoja na kuhimiza matumizi ya Gesi Asilia kwenye Vyombo vya Usafirishaji ili kupunguza gharama zinazotokana na Mafuta.

Aidha, kuhusu Sukari, Chama hicho kimesema Serikali ichukue hatua za haraka kuhakikisha Sukari inapatikana ili Wananchi wauziwe kwa Bei nafuu kwasababu hadi sasa kauli za Serikali hazijasaidia chochote.

Wangepifania ruzuku za vyama kufutwa ili kupunguza au kuondoa kodi kodi kwenye sukari na mafuta, bila shaka vingi vingeshuka bei ikiwamo nauli na hata sukari.
 
Kwamba ruzuku ni jambo jipya baada ya kuletwa tu nauli na sukari bei zikapanda???
 
Ruzuku si jambo la afya, halijawahi kuwa na halitakuja kuwa.

Kulikoni tulipie vyama? Kwamba ziko juu kuliko zinakopaswa kuwa tangia miaka hiyo hakuhalalishi kuendelea kuwa juu leo.

Au wewe huoni hivyo ndugu mjumbe?
 
Futeni ruzuku kwa vyama vya siasa badala yake vigharamiwe na wanachama wao!! Hivi sasa mzigo huu unabebwa na kila mlipa kodi hata wasio na vyama.
Mtindo huu unakipa nguvu chama tawala at the expense of other political parties na kuwa unfair to many citizens. Haufai.
 
CCM itaendelea kuwa na nguvu hata kama ruzuku itafutwa, wana vitega uchumi vingi walivyojitwalia toka enzi za chama kimoja.

Kama ikitokea ruzuku ikafutwa, na kuanza kutegemea michango ya wanachama, basi nina hakika upinzani nao utakufa natural death.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mawazo mazuri Kwa sirikali yetu pendwa lakini wanaotuamria bei na kutojua uchungu na ugumu wa maisha Kwa wananchi wengi wao ni wachumia matumbo Yao wengine tunaonekana mabogasi
 
Ukisikia UNAFIKI ndio kama huu sasa. Nauli hizi hazikuja tu kwa ghafla. Wasafirishaji waliomba kupandisha nauli, ombi lao likatangazwa kwenye magazeti, serikali kupitia LATRA, wakatangaza mkutano wa wadau kupokea maoni kuhusu maombi hayo. Watu hawakujitokeza wakati huo kuzipinga au hata kuandika kwenye anwani zilizokuwa zimetolewa za kupinga. Leo ndio wanaamka kutoa tamko!!!
 
Back
Top Bottom