Chalamila: Dkt. Janabi alisema sukari ni hatari kwa afya, tumieni fursa ya upungufu huu kuachana nayo msipate magonjwa mbeleni

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Chalamila asema ukimsikiliza Dr. Janabi anasema ulaji wa sukari nyingi unasababisha maradhi mengi, kwahiyo wakati huu ambako sukari imeadimika tuachane nayo kabisa ili usiweze kupata matatizo ya afya hapo baadaye.

Kwahiyo serikali imeshindwa kabisa kutatua changamoto hii ya upatikaji wa sukari sasa wanatafuta 'justification' ya ukosefu huo?

Bashe ilibidi uwajibike kwa kushindwa kutatua hili hadi hali imekuwa mbaya hivi.

Pamoja na haya yote bado viongozi mnakula kwa kama zenu na hutasikia posho za wabunge zimepungua, ama wamechukua 'initiatives' za kubana matumizi ili kupunguza makali haya kwa wananchi.

Bure kabisa!
 
Wakati Changamoto ya uhaba wa sukari ikizidi kushika Kasi, viongozi wamekuwa wakinukuliwa kusema watu waachane na matumizi ya Sukari Kwa sababu sio salama kiafya kama ambavyo Mkuu wa Mkoa wa Dar Albert Chalamila amenukuliwa.

Hii ni Kauli ya pili ,ya kwanza ilitoka Kwa Prof.Janabi na kuungwa mkono na Waziri wa Afya.

Swali.Je huu ndio msimamo wa Serikali au msimamo binafsi wa Chalamila na wengine?
 
View: https://www.instagram.com/reel/C3h-6T4NtiU/?igsh=MTBiMDVwcGM2aW9nZg==

Swali.Je huu ndio msimamo wa Serikali au msimamo binafsi wa Chalamila na wengine?

Watuleteee sukari wasikwepe uwajibikaji
 
Tangu lini amekuwa Dr. bingwa wa magonjwa yanayo sababishwa na matumizi ya sukari?

Je, yeye na familia yake hawatumii hiyo sukari kwenye matumizi yao ya kila siku? Mfano kwenye vyakula na vinywaji wanavyo tumia kila siku?

Unafiki siyo mzuri hata kidogo.
 
Chalamila asema ukimsikiliza Dr. Janabi anasema ulaji wa sukari nyingi unasababisha maradhi mengi, kwahiyo wakati huu ambako sukari imeadimika tuachane nayo kabisa ili usiweze kupata matatizo ya afya hapo baadaye.

View attachment 2909161

Kwahiyo serikali imeshindwa kabisa kutatua changamoto hii ya upatikaji wa sukari sasa wanatafuta 'justification' ya ukosefu huo?

Bashe ilibidi uwajibike kwa kushindwa kutatua hili hadi hali imekuwa mbaya hivi.

Pamoja na haya yote bado viongozi mnakula kwa kama zenu na hutasikia posho za wabunge zimepungua, ama wamechukua 'initiatives' za kubana matumizi ili kupunguza makali haya kwa wananchi.

Bure kabisa!
Jamaa ni kichwa maji Sana huwa anawaza nini ?

USSR
 
Ikianza kupatikana kwa wingi atasemaje?
Kunyweni chai kwa wingi ili kujenga uchumi wa nchi
 
Sasa hivi Tanzania Kuna wagonjwa wengi maradhi Yao Wala hayajasababishwa na Sukari,Wala nyama Wala wanga waliyapata wanakojua wenyewe na Wao wanajua mia Kwa mia

Lakini baada ya kuyakwaa hayo maradhi moja ya masharti waliyopewa ni Kuwa waepuke Sukari,Wanga,Nyama wanga nk kama wanataka kuendelea kuishi

Sasa Hilo Kundi la wagonjwa ndie limegeuka kuwa wapiga yowe ohh watu msitumie Sukari,smile wanga chakula Cha kutia nguvu mwilini ,epukeni Mafuta ya kupigia kuleni chukuchuku ,Msile nyama nk

Hao wagonjwa badala ya kuwaambia watu waache kula hivyo vyakuka ni vizuri wajikite kuimeza dawa walizoelekezwa na wahangaike na tiba za maradhi Yao wawaache wasukuma na wakulima waendelee kula Ugali wao,Masai waendelee kula nyama zao Kwa wingi na watu wa pwani waendelee kunywa chai Yao yenye Sukari kibao

Wagonjwa waache kusumbua watu walio wazima hayo maradhi wanayo chanzo Chakr sio Sukari,Mafuta ,wanga Wala nyama

Wabaki wodini kutibiwa waache kelele
 
Kwaiyo tutegemee mwezi unaokuja wa Ramadhani sie waislamu tutumie chumvi mbadala wa sukari kuadimika......huyu akilala leo kesho gari linaloandikwa RC DSM halitomfata nyumbani kwake tena
 
Back
Top Bottom